Mechi ya kirafiki baina ya timu ya Toto ya jijjini Mwanza na mabingwa wa Tanzania bara Simba sports club ya jijini Dar es Salaam inaendelea hivi sasa katika uwanja wa CCM Kirumba na hadi naandika ni dakika ya 37, timu ya Simba inaongoza kwa goli moja lililofungwa na Uhuru Selemani dakika ya 29.
Updates:
Matokeo ya mwisho Simba wameibuka kidedea kwa ushindi wa magoli mawili huku goli la pili likifungwa na kiungo Salum Kinje ambaye amesajiliwa toka timu ya AFC Leopards ya nchini Kenya.
Kesho mabingwa hao wa Tanzania wanatarajia kucheza na Mabingwa wa Uganda The Express huko mjini Shinyanga katika uwanja wa Kambarage.