Live Star TV: Mwana CHADEMA David Kafulila

Live Star TV: Mwana CHADEMA David Kafulila

Huo ndio utofauti nnao usema ambao ni lazima mbinu za kukabiana na aina hii ya utawala ziendane na si kutoka nje ya bunge tena, na mbinu nyingine ambazo kwa sasa hazina athari kisiasa
Usipotoka wakapitisha tutasema walikuwepo ikipitishwa bora sasa tunajua waliopitisha ni ccm tu
 
Soma fact zinazotolewa na Kafulila alafu toa hoja m'badala.
Kafulila anaongea fact ila kwanza watz wangapi wanazipata hizi fact?
watz wangapi wanazielewa hizi facts?
mwisho ni kwamba maneno bila matendo ni sawa na kujiangalia kwenye kioo na pindi tu ukikiondoa kioo utakuwa ushajisahau namna ulivyo
 
Naangalia kipindi, Kiukweli David Kafulila ni mkweli na yuko very right kuwa serikali yetu inadanganywa na wataalamu.

Waziri wa Nishati Prof. Muhongo amelidanganya taifa kuwa kufikia 2020 kila kijiji kitakuwa na umeme wa uhakika ni uwongo, hatuwezi kufikia huko kwa sababu hadi sasa hatuna umeme wa uhakika na hii miaka mitatu iliyobaki haiwezi kutosha kuelectrify nchi nzima hivyo ahadi ya Prof. Muhongo ni uwongo wa mchana kweupe.

Amesema Tanesco kwa hivi ilivyo na mitambo chakavu na jinamizi la IPTL na mchwa wa Simbion, Agreko etc haiwezi. Labda Tanesco ifumuliwe yote tuanze upya.

Kiukweli namkubali sana huyu Kafulila kwa hoja zake.

Paskali
Kuweka kumbukumbu sawa, sio wewe tu bali na wananchi jimboni kwake walimkubali sema tu 'michakato' ndiyo ilimuangusha!
 
Mwanachama wa CHADEMA Mh. David Kafulila yupo Star TV katika kipindi cha Tuongee Asubuhi. Mada ni Imani ya wananchi katika maendeleo ya Taifa. Ameanza kuzungumza mbunge wa CCM Bukombe Deo Biteko huyu anazungumza kama waziri, yeye ni kusifia tu hana cha kushauri.

Anasema watu wana imani na serikali, sasa hivi hakuna upendeleo katika ajira (sijui anazungimzia ajira gani huyu)

Karibuni kumsikiliza na kumtazama Kafulila.


Fanya kazi wewe, muda wa kazi, unaperuzi chaneli za TV? Hizi Siasa zitawatia Ujinga na Umaskini!
 
Ni kweli, mimi niliwalaani Chadema tangu walipomtimua! .

Mimi sina chama ila Chadema ni chama chenye matumaini mazuri ila kinakabiliwa na udhaifu mkubwa sana ya kukosa viongozi wenye busara na kuna vichaa mule wanasikilizwa sana. Kama wasinge timuana timuana combination ya team work ya Zitto, Kafulila na JJ. Nnyika, J. Shonza, Mdee kule Bungeni, moto ungewaka na huku nje ya Bunge, nyasi zingewaka moto. Baada ya kutoka Zitto, Mdee, Mnyika wanapwaya, Zitto nae anapwaya, Shonza nae japo kaingia Bungeni lakini hakuna kitu kabisa! .

Kuna watu wanaperform wonders kwa simbiosis relationships za team work, wakiwa independently they are nothing.

Paskali
Kaka Pascal , wakati mwingine sisi binadamu kuvumiliana huwa inakuwa ngumu sana. Hawa watu wametawanyika , labda kwa sababu ya udhaifu wa kibinadamu. Kadri siku zinavyosogea wanakuja kugundua kuwa wote wanahitajiana. Hao uliowataja kweli wakikaa pamoja , kazi yake siyo ya kitoto.
 
Naikubali chadema ila nahisi imefika mwisho wa kufikiri maana wanatumia mbinu walizokawa wanatumia kwa JK. Kwa utawala wa JPM ambao ni tofauti kabisa na wa JK kiitikadi,falsafa na mtizamo kitu ambacho hadi sasa chadema(ukawa) wanafeli

Wanaanza kufanya siasa wakati harakati bado haijawaweka pazuri
Wanafeli
IPI ni itikadi, falsafa na dhamira ya Mh Magufuli?

Pengine ikasaidia kujua namna ya kuenda na mikakati mbadala ya kuleta maendeleo
 
Mkuu unachokisema ni kweli kua mhongo anamdanganya rais na anatudanganya watanzania.

Lakini pia kuweka kumbukumbu sawa kama sikosei Tanesco kwa sasa hawana mkataba na Aggreco na symbion maana mikataba yao ilipoisha mwaka jana haikurejeshwa.

Lakini bado wanaidai Tanesco mabilioni ya shilingi ambayo muhongo amesema hatutalipa kupitia nyongeza ya bei ya umeme bali serikali itakopa ili kuyalipa.

Maana yake ni kwamba muhongo anaona kutupunguzia ugumu wa maisha ni kutokulipa madeni kupitia kununua umeme bali tutayalipa kwa kodi zetu nyingine.
Symbion huwajui wewe, Obama alivyokuja kuzindua vinu vya kufua umeme wa gas pale ubungo ndio Symbion ile. Ukivuka ng'ambo ya Tanesco kuja huku ubungo mataa kama unaenda ubungo maziwa ile mitambo inyopoza na kuongeza umeme ndio hao wengine aggreco.
 
Back
Top Bottom