Live on Star TV: Makocha wazalendo na soka la Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Live on Star TV: Makocha wazalendo na soka la Tanzania

Discussion in 'Sports' started by Paul Mabuga, Oct 3, 2012.

 1. P

  Paul Mabuga Verified User

  #1
  Oct 3, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari waungwana! Mjadala Mkuu Jumatano ya leo ni:

  Je, uwekezaji katika soka Tanzania una tija? Rasilimali zinazowekezwa kwa maendeleo ya soka dhidi ya hali halisi ya vilabu vyetu. Karibuni mchangie.

  Kumbukeni kuwa leo ni siku ya Big Match -- Simba na Yanga.

  Kwa majadala mwepesi: kati ya saa 12 as hadi saa moja asubuhi;

  Je Makocha wazalendo wakilipwa mshahara wa shilingi milioni 20 kwa mwezi soka la Tanzania litakuwa kama Ulaya?

  Tafadhali anza kuchangia
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Soka la bongo likipata rasilimali (fedha, viongozi wenye utashi, vipaji, mashabiki na wapenzi) nyingi zaidi linaweza kuendelea mfano mzuri ni Azam sababu wana uwezo wa kifedha na utashi wamefika hapo walipo wana 4 yrs lkn wana uwanja, timu za vijana, wamekuwa 1 runner up ktk kila mashindano waliyoshiriki msimu uliopita wa ligi kwa hyo kwa mfano wa azam ni wazi kuwa mafanikio katika soka la bongo yanawezekana.

  Tukija upande mwingine soka letu liko kimizengwemizengwe sana hata professionalism inashindikana u-Simba na u-Yanga uko sana kuanzia TFF, marefa, waandishi viongozi wa serikali wote wana usimba au uyanga na still timu hizi 2 kubwa bado nazo zinaongozwa kiujanjaujanja hawana mission wala vision.

  Athari za u-Simba na u-Yanga hizi timu zimekuwa zikipendelewa sana na marefa na TFF mfano ni lile zengwe alilopigwa Moro Utd ile iliyokuwa inafadhiliwa na Balabou.

  Hata mashabiki mikoani wamekuwa wakisaliti timu zao pindi zinapocheza na hizo timu.

  Mimi ni mdau wa timu ya AFC Arusha, kuna kipindi tulikuwa tunacheza ligi kuu na tulikuwa ktk ukata mgumu na msaada umetafutwa haukupatikana then Yanga walikuja washabiki walichanga laki 3 on the spot kwa Yanga ambayo tayari ina wadhamini na vitega uchumi huku wakijua timu yao ya nyumbani ni fukara....

  Kwa upande wangu; ili soka letu liendelee kabla ya kuwekeza fedha na vitu vingine tuondoe usimba na uyanga sawa ni vilabu vikubwa na vitabakia kuwa hivyo ila unazi upungue ili kutoa fare playground kwa wote
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Kwa upande wa soka la Bongo, hadi makocha na wadhamini wengine wana unazi wa u-simba na u-Yanga. Unakuta timu haina sababu ya kupoteza mchezo unakuta kiongozi wao anawashawishi wachezaji wapoteze mchezo ili tu Simba au Yanga iwe mbali.

  Kwa kusema makocha wazalendo walipwe mamilioni ya shilingi ndio tufike mbali hakuna kitu kama hicho! Tutafika mbali kama uongozi mzima wa soka Tz utabadilika na kufuata misingi ya maendeleo. Mfano; African Lyon toka mwaka jana wamepata udhamini lakini TFF wanaukatalia udhamini huo halafu wanajifanya wanataka soka likue.

  Kuendelea kwa soka Bongo ni pindi pale unazi wa kishamba utakapoisha..

  Ahsanteni.
   
 4. T

  Tanzania1960 JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pukudu

  Samahani kwa kusema wachezaji wetu wa kitanzania ndio wanajiangusha wenyewe na makocha wazawa.

  Kwa mfano:
  Mimi nafikiri ukichukulia kocha kama Minziro au Kilinda au Tegete utaona wanawapa wachezaji kila kitu kwa sababu na wao wanatafuta ile sifa nzuri ya kuheshimiwa na mabosi wao pamoja na mashabiki lakini wachezaji wanaweka fedha kwanza na heshima baadaye kwa hiyo timu ikifungwa analaumiwa kocha kwanza....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...