LIVE: Man UTD vs Arsenal...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Uwanja tayari umefurika hapa.
Washabiki ni wengi kutoka kila pembe ya Dunia wamekuja kujumuika ili kushuhudia moja kati ya mitanange mitamu wikiendi hii.

Kila upande ninao uangalia uwanjani hapa umefurika watu huku washabiki wa timu zote wakiwa ni wenye furaha na kujiamini.

Manchester UTD wapo nyumbani, kikubwa wanajoweza kujivunia na kinaweza kuwasaidia hii leo ni rekodi ya kocha wao Jose Mourinho ambae katika mechi 15 alizowahi kupambana na kocha Arsene Wenger basi kocha huyu hajawahi kupoteza mpambano hata mmoja.

Arsenal wapo ugenini, wanahitaji ushindi ili kwanza kumfutia aibu kocha wao, na pili kuendelea kujiweka sawa pale kileleni kwenye msimamo wa ligi.

Hakuna timu iliotoa malalamiko ya kutokuwa na imani na waamuzi, hivyo basi jambo hili linamaanisha kuwa muda utakapo taradad basi kabumbu litaenda kuanza.

NB: kuna mashabiki nawasikia kwa mbaali wanaimba "zamu ya nani leo" sijajuwa ni wa timu gani na nini haswa wanakimaanisha...

Basi nawarudisha kwenye TV zenu kwa ajili ya kufuatilia matangazo ya moja kwa moja kutoka hapa jiji la Manchester.
 
mimi narudi kutafuta treni ili niweze kuwahi jiji la Milan hio kesho ambapo kuna patashika nyingine inayofahamika kwa jina la Della Madoninna...
 
Jose Mourinho anaendeleza utabe kwa Wenger,
Man Utd 1 - 0 Arsenal
Juan Mata 68'
2016-11-19T140122Z_122565682_MT1ACI14675831_RTRMADP_3_SOCCER-ENGLAND-MUN-ARS.JPG
 
Back
Top Bottom