Ni wengi wetu tumekuwa tukitamani kutengeneza tovuti,iwe ni kwa ajili ya kibiashara au biinafsi.Ingawa siku hizi suala la kutengeneza website limekuwa rahisi zaidi kutokana na kuwepo kwa programu na CMS nyingi,ila msingi ni muhimu ili kuweza kutumia hizo programu na cms kwa ufanisi zaidi. Hivyo ungana na timu ya AfroIT kila Jumanne na Jumamosi saa kumi kamili ya Tanzania kwenye mafundhisho hayo ya hatua kwa hatua tena yakiwa live,kama upo darasani vile.Unapata wasaa wa kuuliza na kuchangia.
Mtoa mada: Mkata Nyoni(hatua ya kwanza)
Muda: Kila jumanne na Alhamisi,saa kumi jioni,1600hrs(kwa saa za afrika ya mashariki)
Link: Hapa
Idadi ya wanafuunzi:10
Level: Kwa wanaojua kutumia browser na internet kwa uchache wake
Ufafanuzi:Tembelea
Hapa
Utaratibu wa mafundisho
Tutaanza mwanzo kabisa,tutatumia mtindo wa project ili kuhakikisha inakuwa na maana zaidi,sio kusoma tu halafu huoni kinachotokea.
Kwenye mafundisho haya ya moja kwa moja(Live),tutakuwa wote katika kutengeneza AfroIT Movie Store.Utaweza kujionea na kujifunza hatua baada ya hatua mbapo hadi unamaliza mafundisho,basi utaweza kutengeneza website yako ya kawaida.
Baada ya hapo,utajiunga na mkufunzi mwingine ambaye ataiendeleza AfroIT Movie Store kwa kuweka manjonjo na mididi zaidi(Advanced).
Katika hatua ya Mwisho(tatu) ndipo mutajiunga na wataalam ambao wataichukua website ya hatua ya pili na kuifanya kuwa dynamic ambapo kutakuwa na makundi mawili,moja ni wale wa PHP na lingine ni wale wa .NET.