Live: Kutangazwa kwa mchezaji bora wa soka Afrika

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Leo,katika jiji la Abuja nchini Nigeria atatangazwa mchezaji bora wa soka wa Afrika. Atatangazwa mchezaji bora kwa wachezaji wa nje ya Afrika na yule anayechezea ligi za ndani za Afrika

Katika wachezaji wa nje ya Afrika,wamo akina Mane,Mahrez na Aubemayang Kwa wachezaji wa nje,kati yao yuko Mganda Dennis Onyango wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini

Muda huu,Rais wa CAF Issa Hayatou anahutubia.

Rais wa CAF amemaliza hotuba yake. Kuna burudani inaendelea toka kwa Rising Stars.

========
  • NIGERIA: Mchezaji wa timu ya taifa ya Algeria na klabu ya Leicester City, Riyad Mahrez ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika(2016) katika tuzo zilizotolewa usiku wa kuamkia leo katika Jiji la Abuja.

    Washindi wengine wa tuzo katika vipengele mbalimbali ni pamoja na Dennis Onyango(Mchezaji bora wa ndani), Uganda(Timu bora ya mwaka), Nigeria(Timu bora wanawake), Mamelodi Sundown (Klabu bora), Kelechi Ihenacho(Mchezaji bora chipukizi Mwenye kipaji), Alex Iwobi(Mchezaji bora chini ya miaka 23), Pitso Masimane(Kocha Bora), Bakary Papa Gassama(Muamuzi bora), Asisat Oshoala(Mchezaji bora kwa Wanawake)

    Aidha katika utolewaji wa tuzo hizo msanii wa kimataifa kutoka Tanzania,Diamond Platinumz alipata nafasi ya kutumbuiza wimbo wake wa Salome.
https://www.instagram.com/p/BO6WZVmlyIN/?taken-by=jamiiforums&hl=en#
 
Timu bora ya taifa ya Wanawake ya mwaka 2016 ni timu ya Taifa ya Wanawake ya Nigeria aka Super Falcons
 
Mchezaji bora chipukizi na mwenye kipaji Afrika wa mwaka 2016 ni Kelechi Ihenacho wa Nigeria na timu ya Man City
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom