Lissu na lowassa wakiteta!

Lissu na lowassa wakiteta!

Aloyce mk

Member
Joined
Nov 10, 2014
Posts
76
Reaction score
33
LISSU NA LOWASSA.jpg
 
Lissu anapenda kujipendekeza sana
 
Ilikuwa ni mazishi ya Komba au mtoto wa Nyerere
 
Makamanda hao...soon wiki ijayo mtaona moto wao....!!
 
mleta mada kama kuongea pamoja ni dhambi basi chambua ile picha ya Kikwete akiwanadi kina Lowasa.Mramba Na Chenge 2010,onyesha pia mchango wa Chenge Na Uandishi Wa Katiba
 
LOWASA KUHAMIA UKAWA ATAZUI GOLI LA MKONO:

Nadhani ni mwandishi wa kimarekani Cristoper Dikens kama sijakosea jina, wakati Marekani ikijiandaa kuishambulia Iraq ili kumuondoa Sadam madarakani mandishi huyu aliandika makala "The perils of victory" Kwa Kiswahili unaweza kusema “hatari za ushindi”. Kwenye makala hii alitahadharisha mambo ambayo yangetokea baada ya ushindi wa kijeshi wa marekani dhidi ya Sadam. Alitabiri karibu kila kilichotokea baadaye kuanzia the cilivil war hadi kugeuka kwa Iraq kuwa a save heaven kwa magaidi.

Si lengo langu kuijadili makala ile, nimechukua kichwa cha makala ile vile kinawiana sana na yanayoelekea kutokea kwenye siasa za Tanzania kwa sasa. Kuna fununu kwamba kada wa CCM Mh Edward Lowassa anaelekea ku hama chama chake na kujiunga na chama kikuu cha upinzani (CDM) na labda akapitishwa kugombea uraisi kupitia UKAWA.

Uchambuzi wangu kuntu unaniambia uwezekano wa Lowassa kushinda uraisi kupitia UKAWA ni mkubwa. Kwa nini! Wengi wanafikiria juu wa watu walioko nyuma yake lakini sidhani kama hilo ndilo lenye umuhimi wa kwanza. Kuna mambo kadhaa yanayompa Lowassa na UKAWA nafasi nzuri ya kuiangusha CCM.

CONNECTIONS ZA LOWASSA NDANI YA SYSTEM NA CHAMA Kushinda uchaguzi ni zaidi ya kuungwa mkono na watu, ni zaidi ya kupigiwa kura za kutosha. Uchaguzi ni kama vita na unapojipenyeza kwenye ngome ya adui yako na kujua anachopanga kufanya hakika una nafasi nzuri zaidi ya kushinda. Lowassa ana watu ndani ya system na CCM. Kuna watakaotoka naye iwapo atatoka (wana CCM) na kuna watakaobaki na kuendelea kumtumikia kichini chini wakiwa CCM, kuihujumu CCM toka ndani. Watu wake ndani ya system watasaidia sana kukabili juhudi wa system kuuhujumu upinzani. CCM na system iliyoko nyuma yake italazimika kupigana vita mbili kwa wakati mmoja, vita na upinzani wa wan je upande mmoja na upande wa pili itakuwa vita dhidi ya upinzani wa ndani. War on two fronts is the last thing strategist would wish for.

RASILIMALI FEDHA Ni wazi kuwa nyuma ya Lowassa kuna massive financial resources kulinganisha na kile ambacho CDM/UKAWA inaweza ku mobilize bila Lowasa. Rasilimali fedha ni muhimu sana kushinda uchaguzi, huu ni mchakato ghali sana ambapo uwezo wa kifedha una nafasi yake katika kuleta matokeo.

ORGANISATION Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, 4u movement ilikuwa the best organised campaign within CCM, ilikuwa movement iliyoazima mbinu nyingi za kibiashara kufanya siasa, kosa kubwa lilikuwa ni kutokuweka msisitizo wa kutosha kwenye siasa yenyewe, siku nikiwa na nafasi nitalieleza hili kwa kina. Sasa organisation hii ikijumlishwa naya UKAWA itakuwa ni kikosi mahiri kabisa na tutaona mambo mapya kwenye kampeni za kisiasa. Sioni namna gani CCM inaweza kutengeneza timu ya kushindana na hii hapa.
 
mleta mada asibezwe,sio lazima iwe kweli lakini maneno yaliyopo mtaani,ukimya Wa kumtangaza mgombea na hizi picha sio dalili njema kwa sisi wapenda mabadiliko.lowasa atatuumiza zaidi, chadema mpokee,mkalishe ajifunze uzalendo siyo mumuuzie chama.kama kweli tulianza na Mungu na kwamba tutamaliza na Mungu kama mgombea ni lowasa inabidi tuhoji Uungu Wa Mungu atakayekuwa anatajwa maana lowasa sio msafi ambaye Mungu halisi anaweza kumtanguliza.
 
Jamani naomba namba ya Lowassa jamaa akihama na akagombea kura yangu anayo kwa ujasiri wake
 
LOWASA KUHAMIA UKAWA ATAZUI GOLI LA MKONO:

Nadhani ni mwandishi wa kimarekani Cristoper Dikens kama sijakosea jina, wakati Marekani ikijiandaa kuishambulia Iraq ili kumuondoa Sadam madarakani mandishi huyu aliandika makala "The perils of victory" Kwa Kiswahili unaweza kusema “hatari za ushindi”. Kwenye makala hii alitahadharisha mambo ambayo yangetokea baada ya ushindi wa kijeshi wa marekani dhidi ya Sadam. Alitabiri karibu kila kilichotokea baadaye kuanzia the cilivil war hadi kugeuka kwa Iraq kuwa a save heaven kwa magaidi.

Si lengo langu kuijadili makala ile, nimechukua kichwa cha makala ile vile kinawiana sana na yanayoelekea kutokea kwenye siasa za Tanzania kwa sasa. Kuna fununu kwamba kada wa CCM Mh Edward Lowassa anaelekea ku hama chama chake na kujiunga na chama kikuu cha upinzani (CDM) na labda akapitishwa kugombea uraisi kupitia UKAWA.

Uchambuzi wangu kuntu unaniambia uwezekano wa Lowassa kushinda uraisi kupitia UKAWA ni mkubwa. Kwa nini! Wengi wanafikiria juu wa watu walioko nyuma yake lakini sidhani kama hilo ndilo lenye umuhimi wa kwanza. Kuna mambo kadhaa yanayompa Lowassa na UKAWA nafasi nzuri ya kuiangusha CCM.

CONNECTIONS ZA LOWASSA NDANI YA SYSTEM NA CHAMA Kushinda uchaguzi ni zaidi ya kuungwa mkono na watu, ni zaidi ya kupigiwa kura za kutosha. Uchaguzi ni kama vita na unapojipenyeza kwenye ngome ya adui yako na kujua anachopanga kufanya hakika una nafasi nzuri zaidi ya kushinda. Lowassa ana watu ndani ya system na CCM. Kuna watakaotoka naye iwapo atatoka (wana CCM) na kuna watakaobaki na kuendelea kumtumikia kichini chini wakiwa CCM, kuihujumu CCM toka ndani. Watu wake ndani ya system watasaidia sana kukabili juhudi wa system kuuhujumu upinzani. CCM na system iliyoko nyuma yake italazimika kupigana vita mbili kwa wakati mmoja, vita na upinzani wa wan je upande mmoja na upande wa pili itakuwa vita dhidi ya upinzani wa ndani. War on two fronts is the last thing strategist would wish for.

RASILIMALI FEDHA Ni wazi kuwa nyuma ya Lowassa kuna massive financial resources kulinganisha na kile ambacho CDM/UKAWA inaweza ku mobilize bila Lowasa. Rasilimali fedha ni muhimu sana kushinda uchaguzi, huu ni mchakato ghali sana ambapo uwezo wa kifedha una nafasi yake katika kuleta matokeo.

ORGANISATION Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, 4u movement ilikuwa the best organised campaign within CCM, ilikuwa movement iliyoazima mbinu nyingi za kibiashara kufanya siasa, kosa kubwa lilikuwa ni kutokuweka msisitizo wa kutosha kwenye siasa yenyewe, siku nikiwa na nafasi nitalieleza hili kwa kina. Sasa organisation hii ikijumlishwa naya UKAWA itakuwa ni kikosi mahiri kabisa na tutaona mambo mapya kwenye kampeni za kisiasa. Sioni namna gani CCM inaweza kutengeneza timu ya kushindana na hii hapa.

nyie watu Wa lowasa hamshibi hela,baada ya mweleka Wa Dodoma sasa mnaichukia ccm yenu jamani ili mle pesa yake.kumbuka tuliichukia ccm kwasababu ya ufsadi na mafsadi ambao kinara wao ni lowasa huyuhuyu,hajarudisha alichoiba na wala hajatubu ili tujue kazaliwa upya.ccm wamemkata Leo mnakuja Naye kwetu,hatumtaki.mtawanunua akina mbowe siyo sisi.kama ccm wamemtoa panya kwenye MTUNGI wao na panya huyohuyo akahamia kwenye MTUNGI wetu,sisi hayo Maji hatunywi tutaenda kuomba Maji hata kwa kina Nape maana MTUNGI wao hauna panya
 
Back
Top Bottom