Lissu amlima barua Shibuda

cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka

we akili huna,kama ni ndoto subiri muda ufike.
 
Shibuda ni mjinga hajui siasa,chadema wamtimue tu mtu mwenyewe hana malengo.
 
Shibuda ni korokoro, ukiweka mawe ndani linatoa kelele, ukiweka maji hayakai, ukilitunza ndani wenye akili wanalitupa nje, hata watoto hawalihitaji kwa kuchezea. Ni zaidi ya mzigo, ni kero.
 
Anayofanya Shibuda yanamdhihirisha hakuingia cdm kwa nia thabiti na imani ya mabadiliko bali kuupata tu ubunge. anachokifanya ni hatari sana kwa harakati za cdm. naamini wahusika watalishughulikia inavostahili kwa taratibu zilizopo
 
CHADEMA lazima ifanye maamuzi magumu. Imwandikie barua kali ya kukiuka maadili ya chama na impe nafasi ya kujieleza. Kama maelezo yake hayatoshelezi, imfukuze uanachama. Uchaguzi ukirudiwa hata CCM wakishinda jimbo hilo bado CHADEMA itabaki kuwa na majority Bungeni na kubaki kuwa chama kikuu cha upinzani.

Ila Tundu Lissu amenoa kwa kutoa maneno mengi kwa waandishi wa habari. Angesema kuwa hili jambo linashughulikiwa na chama na tutatoa taarifa kwa umma kama tukifikia uamuzi wowote. Haikuwa na haja na kusema anamwandikia barua Shibuda na yuko tayari afukuzwe.

Funzo kwa Tundu Lissu, no need to display CHADEMA's dirty linen in public.
 
hawa lazima wasambaratike, kila mmoja wao anataka kuwa Raisi Shibuda atatoka na kutoa uharo wote wa CHADEMA. Zitto anafatia baada ya Shibuda.. nyie mtaona.
 
Kama amekiuka katiba ya chama chake kwa makusudi, fukuza tu
 
Mambo anayoyafanya Shibuda ni tofauti kabisa na maagizo na taratibu za chama,hastahili kabisa kuwa mwana cdm,hafai kabisa,na kama chama hakitachukua maamuzi magumu kuhusu huyu jamaa,atawamaliza!Fukuza kungali bado asubuhi,msisubirie mchana
 

Hili swala hujalifuatilia vizuri mkuu toka awali, Lengo la Chama ni kushinikiza serikali iondoe hizo posho kwahiyo mpaka zitakapo ondolewa ina maana taifa litafaidika na kupungua kwa gharama za uendeshaji na matumizi ya serikali ambayo hayana umuhimu, kufanya hivyo aina maana kuwa wametumwa Bungeni kugoma bila hoja na tija! mawazo yako yana maanisha hivyo, kitu ambacho hatutegemei kufanywa na wabunge na viongozi sio wahuni wale ni viongozi wa Taifa hili.

Kila mbunge ana haki ya kupokea Posho hizo hadi pale serikali itakapo zifuta kama ambavyo CDM wameshauri, wapo Bungeni kwa ajili ya kurekebisha kanuni na sheria mbovu kama hizo, husidhani kuwa CDM wanaposema kufanywe overhaul ya katiba kuwa hivyo sasa wasiheshimu hii katiba iliopo!? hiyo siyo sheria na sheria haitafsiriwi hivyo, wataiheshimu hii katiba iliopo hadi pale itakapo patikani hiyo ambayo Watanzania tuliowengi tunaililia.

Kama umezaliwa wakuto elewa hauta elewa, maana hata darasa wapo wanakesha kujisomea lakini bado wana-fail mitihani. Jitahidi kuisoma na kuisoma nimejaribu kuweka kwa lugha rais sana.
 
Ukuta ukishindikana kwa langi choka haiwezi cdm msipende vyakuokoteza huo mfupa ccm ilishidwa kuutafuna pamoja na kuunga limau komaeni naye
 
Tuko radhi Shibuda atimuliwe-Lissu

Na Grace Michael, Dodoma
Majira


SAKATA la Mbunge wa Maswa Magharibi, Bw. John Shibuda na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limechukua sura mpya baada ya wabunge wa chama hicho kuweka msimamo kuwa wako tayari kumfukuza uanachama na kurudi kwenye uchaguzi endapo Kamati Kuu itaridhia na kuona kuwa hafai kuwa katika chama hicho.

Msimamo huo ulitolewa jana mjini hapa na Mnidhamu wa Kambi ya Upinzani, Bw. Tundu Lissu baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari kuhusu hatua wanazotarajia kuchukua dhidi ya mbunge huyo baada ya kutangaza vita na chama hicho.

"Tuko tayari kuachana naye na kurejea kwenye uchaguzi... hatuwezi kuvumilia tabia ya namna hiyo ambayo ameifanya wazi ya kupingana na sera ya chama na muda huu ndo namwandia barua rasmi ya kumtaka ajieleze ni kwa nini anakwenda kinyume na msimamo wa chama," alisema Bw. Lissu na kuongeza kuwa:

"Hatua ambayo tunaweza kwa upande wetu hapa ni kumtaka ajieleze lakini baadaye suala hili litajadiliwa katika na Kamati Kuu ya chama ambayo ina mamlaka makubwa zaidi yakiwemo ya kumfukuza uanachama na katika hili halina visingizio kwa kuwa amelifanya wazi na msimamo wetu tuko tayari kurudi kwenye uchaguzi...na kama anaweza arudi alikotoka," alisema Bw. Lissu.

Alipohojiwa kuhusu kauli ya Bw. Shibuda ambaye alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema yuko tayari kuanza kuhubiri mabaya ya CHADEMA na viongozi wake akiwemo, Bw. Freeman Mbowe na Bw. Zitto Kabwe, Bw. Lissu alisema kuwa hana jipya la kuhubiri dhidi ya chama hicho kwa kuwa hana anachokijua.

"Hivi Shibuda atahubiri nini kibaya cha CHADEMA? Ni muda gani aliotumia katika kuyajua hayo anayodai? Kwanza hata vikao sidhani kama kuna vikao zaidi ya vitano ambavyo amehudhuria tangu ajiunge na chama, hivyo hana jipya zaidi ya kusema matapishi ambayo yamekuwa yakihubiriwa kila siku kuwa CHADEMA ni chama cha wachaga," alisema Bw. Lissu.

Mtafaruku huo wa Bw. Shibuda na chama chake ulitokana na msimamo wake aliouonesha wiki iliyopita bungeni wakati akichangia hotuba ya Waziri Mkuu ya bajeti ya 2011/2012 ambapo aliiomba serikali kuongeza posho za vikao hadi sh 500,000 kutoka sh 70,000 kwa siku badala ya kuziondoa kama CHADEMA kinavyotaka.

Bw. Shibuda pia alipendekeza kubadilishwa kwa jina la posho na kuitwa ‘ujira wa mwia' ili kuondoa mawazo mabaya yanayotokana na neno posho hizo.

Hatua hiyo ya Shibuda ilikwenda kinyume na msimamo wa Kambi hiyo ya Upinzani hasa CHADEMA ambao tayari wametoa msimamo wao kutosaini posho hizo, endapo fomu zake zitatenganishwa na zile za mahudhurio.
 
mpeni pole na mashikolo mageni ya uongozi..
 
Busara, hekima, coaching zichukue nafasi kwake na katika saga lake hili.
Jazba, udhalilishaji, adhabu na mengineyo...SUBRA ZITAWALE.
 
ni mawazo yake jamani

Mawazo ya kutaka kukivuruga chama si mawazo ambayo Viongozi wa CHADEMA wanastahili kuyavumilia. Hakuna ushahidi wowote unaonyesha kwamba CHADEMA ni Chama Cha Wachagga. Fikiria athari kubwa kwa CHADEMA kama watamuachia Shibuda ambaye ni Mbunge wao kuendelea kumwaga sumu kila kona ya nchi kwamba CHADEMA ni chama cha Wachagga ni si ajabu akaongezea kwamba ni chama cha Wakristo. Sidhani kama atakuwa anakijenga chama chake bali atakuwa anakibomoa.
 
Huyu mtu ni mmoja kati wale wabunge(WACHACHE) waliofikiri BUNGE ni kijiwe cha wazee kusemea mambo yao ya uzeeni.
Hata hivyo wazee wengine huzeeka na busara zao ila huyu uzee umemletea UKICHAA.
 
Fukuza huyo, timua huyo,piga huyo, huyo ni nyoka aende kwa nyoka wenzake walioshindwa kujivua gamba
 
cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka
Na wewe ni mlevi mwingine uliyepotea njia. mada nyingine unachangia kingine hueleweki kama ilvyo jinsia yako 'jikedume'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…