Lissu alaani agizo la Magufuli kwa Wakuu wa Mikoa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, ametoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwaagiza wakuu wa mikoa kawakamata vijana wanaocheza pool muda wa kazi.

Mwanasiasa huyo maarufu, alisema ni wazi kuwa agizo la Rais Magufuli linataka kuchochea matumizi mabaya ya madaraka kwa wakuu wa mikoa na wilaya nchini.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambayo ndio inasimamia agizo hilo, inawapa mamlaka ya kipolisi wakuu wa mikoa na wilaya kukamata watu wanaovunja sheria pale ambako hakuna polisi.

Alisema sheria hiyo pia inaeleza kuwa mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 na aliyemkamata anapaswa kuandika maelezo ya sababu za kumkamata.

“Sifahamu kama maelekezo hayo wamepatiwa au wameelekezwa tu wakamate wanaovunja sheria? Lakini pia wafahamu sheria hii inaruhusu kiongozi huyu kumkamata mtu kama hakuna polisi na kama wapo, sheria hii haimruhusu kufanya hivyo.

"Siku hizi kila tukio mkuu wa wilaya anaongozana na OCD (mkuu wa polisi wa wilaya), je ni wakati gani atakamata watu kama si kutaka kuvunja sharia?” alihoji.

Lissu alieleza agizo hilo ni wazi litasababisha wakuu hao wa mikoa na wilaya kukamata hata wasio na hatia.

“Wameelezwa tu kuwa wakamate watu wawaweke polisi, lakini hawajapewa maelezo ya sheria hii inayowasimamia, hivyo ni hatari kwa jamii, matokeo yake ni muendelezo wa matukio kama kukamatwa kwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Konondoni,” alisema.

Chanzo:Nipashe
 
Mwanasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu, ametoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwaagiza wakuu wa mikoa kawakamata vijana wanaocheza pool muda wa kazi.

Mwanasiasa huyo maarufu, alisema ni wazi kuwa agizo la Rais Magufuli linataka kuchochea matumizi mabaya ya madaraka kwa wakuu wa mikoa na wilaya nchini.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ambayo ndio inasimamia agizo hilo, inawapa mamlaka ya kipolisi wakuu wa mikoa na wilaya kukamata watu wanaovunja sheria pale ambako hakuna polisi.

Alisema sheria hiyo pia inaeleza kuwa mtuhumiwa anapaswa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 48 na aliyemkamata anapaswa kuandika maelezo ya sababu za kumkamata.

“Sifahamu kama maelekezo hayo wamepatiwa au wameelekezwa tu wakamate wanaovunja sheria? Lakini pia wafahamu sheria hii inaruhusu kiongozi huyu kumkamata mtu kama hakuna polisi na kama wapo, sheria hii haimruhusu kufanya hivyo.

"Siku hizi kila tukio mkuu wa wilaya anaongozana na OCD (mkuu wa polisi wa wilaya), je ni wakati gani atakamata watu kama si kutaka kuvunja sharia?” alihoji.

Lissu alieleza agizo hilo ni wazi litasababisha wakuu hao wa mikoa na wilaya kukamata hata wasio na hatia.

“Wameelezwa tu kuwa wakamate watu wawaweke polisi, lakini hawajapewa maelezo ya sheria hii inayowasimamia, hivyo ni hatari kwa jamii, matokeo yake ni muendelezo wa matukio kama kukamatwa kwa Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Konondoni,” alisema.

Source:Nipashe
Asante
 
Kuna miners [wafanyakazi wa migodini] na walinzi wa usikuwanaotinga kazini usiku na asubuhi ndio muda wao wa kupumzika,je nao wasicheze pool au wasinywe bia mchana?kwani mchana wa wengine ndio usiku kwao na usiku wa wengine ndio mchana kwao.
 
Tundu Lissu anatafuta kick. Tulizoeshwa kuona wakuu wa mikoa wakiwa ni wapambe wa viongozi wa juu. JPM anataka waende wakaifanyie kazi mishahara yao, na wasiishie kuwa wapambe na watu wa majungu. Uzembe unaolisababishia umasikini taifa hili una mwisho wake. Zile akili za awamu ya nne wakati watu walizoea kumuona rais akitabasamu kwa kila mtu, lazima zibadilike. Tuwe serious kwa faida ya kulikomboa taifa hili, ule muda wa kuchekeana hovyo umeshakwisha, Tundu Lissu na wenzake wanapaswa kuufahamu ukweli huo.
 
Back
Top Bottom