Lissu afunguka kasoro alizofanya RC Makonda

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
LISSU AFUNGUKA KASORO ALIZOFANYA MAKONDA

Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ametaja kasoro kadhaa katika zoezi la vita ya dawa za kulevya lililoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Amesema, Kwanza, Mkuu wa Mkoa hana mamlaka yoyote ya kuelekeza watu kwenda kuripoti polisi. Hii ni licha ya mamlaka yake kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na mamlaka yake ya kipolisi yapo chini ya Sheria ya Tawala za Mikoa.

Pili, kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Jinai, kila mtu ana wajibu wa kutoa taarifa ya kosa la jinai analoona limetendeka kwa polisi. Hii ni ile inayoitwa kufungua RB. Mkuu wa Mkoa Makonda alitakiwa afungue RB kwa wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa. Hajafanya hivyo na ni kosa la jinai kutokufanya hivyo.

Tatu, kwa kutumia mamlaka yake ya kipolisi, Mkuu wa Mkoa Makonda alikuwa na uwezo wa kuamuru wale wote anaowatuhumu kufanya biashara ya madawa kukamatwa na kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 na baadae kufikishwa mahakamani. Badala ya kuamuru 'wahalifu' hawa wakamatwe, Mkuu wa Mkoa Makonda aliwaelekeza wajipeleke polisi kwa mahojiano. Nne, kwa kuzingatia hatari kubwa ya madawa ya kulevya kwa jamii yetu, sheria husika za nchi zimeweka adhabu ya chini kabisa ya kifungo cha miaka 20 kwa wanaothibitika na mahakama kuhusika na biashara hiyo. Aidha, makosa ya madawa ya kulevya hayana dhamana kisheria. Iweje wale wote waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa Makonda wamepelekwa mahakamani lakini wote wamepewa onyo tu au wamepewa dhamana Mahakamani.
Kati ya mapolisi 11 waliotuhumiwa, hakuna hata mmoja aliyepelekwa mahakamani na kushtakiwa kwa tuhuma hizi. Badala yake, tunaambiwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa polisi dhidi yao. Kwa mujibu wa Sheria zetu za ajira, mtumishi anayesimamishwa kazi analipwa mshahara kamili kwa muda aliosimamishwa

Tano, kitendo cha kuwatangaza watuhumiwa kwa namna alivyofanya Mkuu wa Mkoa Makonda, kesi yoyote itakayofunguliwa dhidi yao itaharibika. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba amekamatwa na kushtakiwa kwa sababu za kisiasa na kwa amri haramu za Mkuu wa Mkoa. Kila mtuhumiwa atajitetea kwamba hakuna RB yoyote iliyofunguliwa dhidi yake na kila wakili wa utetezi atataka Mkuu wa Mkoa Makonda aitwe mahakamani kwa ajili ya kuhojiwa. Makonda ataliwa nyama na mawakili kwenye cross-examination. Kwa kifupi, hii sio vita dhidi ya wauza 'unga', hii ni political charade na character assassination inayofanywa kwa mbinu za ovyo kabisa bila kufuata sheria Haitafika popote.
 
Mkuu Chachu Ombara, huyo Bwana Mwanasheria angetufafanulia pia na kasoro zilizofanywa wale waliotutangazia "list of shame" pale Mwembeyanga.

Tunataka tuyatathmini haya vizuri ili tuondoe hii hali ya watu kulia lia kwamba wanaonewa.
 
Kama haya anayosema mwanasheria nguli ni ya kweli. Makonda anayo kazi. Hata hivyo nilitarajia msomi TL angeelezea kwa kifupi kuhusu nini kinatarajiwa kisheria mpaka sasa. Nauliza hivi kwa maana nimesikia wengi wakionshesha utashi wa kufungua kesi dhidi ya huyu Makonda. Tutarajie nini endapo walau nusu tu watafungua kesi on grouds of defamation/character assassination (mara nyingine huwa sielewe tofauti ya maneno haya mawili).

Wanasheria mtudadavulie hili suala, Tafadhali!
 
Makonda ataliwa nyama na mawakili kwenye cross-examination. Kwa kifupi, hii sio vita dhidi ya wauza 'unga', hii ni political charade na character assassination inayofanywa kwa mbinu za ovyo kabisa bilakufuata sheria Haitafika popote.,............anasema rais Mtarajiwa wa TLS
 
Mkuu Chachu Ombara, huyo Bwana Mwanasheria angetufafanulia pia na kasoro zilizofanywa wale waliotutangazia "list of shame" pale Mwembeyanga.

Tunataka tuyatathmini haya vizuri ili tuondoe hii hali ya watu kulia lia kwamba wanaonewa.
Mada inahusu ujinga/makosa aliofanya Makonda. Kama unataka makosa yaliofanya walipo tangaza "List of shame" fungua uzi wako.
 
Lissu ulipaswa uwe mwanasheria mkuu wa serikali tena toka awamu ya tatu.
hana sifa hiyo, pamoja na kuwa na taaluma ya sheria , angetutungia sheria mbovu nyingi tu. huyu anayewatetea wauza unga, anaowatetea wanaomtukana raisi,. ila kwa kuwa wewe na yeye akili zenu zinafanana ndio maana unawaza hivyo. Nafasi za teuzi kama hizi watu huwa hawakurupuki tu kama unavyofikiria . Mzee aliyepita akakurupuka akamteua warioba kuwa mwenyekiti wa tume lakini matatizo aliyoyasababisha kwa nchi ni makubwa kizazi kwa kizazi kitamhukumu
 
Kama haya anayosema mwanasheria nguli ni ya kweli. Makonda anayo kazi. Hata hivyo nilitarajia msomi TL angeelezea kwa kifupi kuhusu nini kinatarajiwa kisheria mpaka sasa. Nauliza hivi kwa maana nimesikia wengi wakionshesha utashi wa kufungua kesi dhidi ya huyu Makonda. Tutarajie nini endapo walau nusu tu watafungua kesi on grouds of defamation/character assassination (mara nyingine huwa sielewe tofauti ya maneno haya mawili).

Wanasheria mtudadavulie hili suala, Tafadhali!
Ninachochukia ni tabia ya woga ya watanzania ya kupenda kuongea sana pasipo kutenda. Ni kwa nini mpaka sasa hivi hawa watuhumiwa hakuna hata mmoja aliyefungua kesi na badala yake wako busy na press conferences. Ninaamini kwamba watakapofungua kesi wala hawatahitaji kuhonga au kulipa waandishi kuelezea hisia zao, vyombo vya habari vitawatafuta wao. Too cheap hata watu wa maana wenye pesa kama wakina Manji, Mbowe, Nicole nao wanajibanabana huko pembeni wakiomba mercy. Take him to the court tuingie mgogoro wa kikatiba kama wanaomtumia watataka kutumia polisi na mahakama zinazoendeshwa kwa hela zetu kumlinda, lazima tukatae upumbavu huu kwa matendo.
 
Back
Top Bottom