Lissu achana na Promota Msando wewe deal na Wanasheria

Decree Holder

JF-Expert Member
Jul 19, 2015
2,559
3,745
Salamu kwanza wanabodi
Nimeona humu ndani maoni ya watu mbalimbali wengine wakijiita mawakili wanaishauri TLS na zaidi Rais kipenzi cha wanasheria Tundu Lissu amchukulie hatua za kinidhamu Wakili Msomi Albert Msando kwa kile wanachoamini ni utovu wa kimaadili na kukiuka maadili ya uanasheria hivyo kuitia doa noble professional mbele ya umma!

Wameitaka TLS imchunguze na imchukulie hatua za kinidhamu Msando. Mimi kwangu huu ni mtego kupima busara za Tundu Lissu juu ya kuliendea hili swala. Nimeibuka na mambo kadhaa kuhusiana na jambo hili.

1. Ni kweli kabisa alichokifanya Msando ni kinyume na maadili ya jamii ya kitanzania na kimemdhalilisha yeye binafsi, familia yake na jamii yake inayomzunguka.

2. Ni kweli kuwa Wakili anatakiwa ku-behave vyema katika jamii as a matter of ethics kama mwanasheria ili kutunza haiba yake kwa jamii. Mwanasheria anashauriwa kutokufanya baadhi ya mambo mabaya na maovu ambayo yanafanywa na common men huko nje mfano kunywa na kulewa chakali, ndiyo maana jaji anashauriwa ikiwezekana anunue vilevi akanywe kwake akiwa peke yake kulikoni kunywa mbele ya hadhara ambapo anaweza tindikiwa na akafanya mambo ambayo yanaweza kumuondolea heshima yake kwa jamii hivyo watu kutilia shaka weledi na maamuzi yake anapokuwa mahakamani.

3. Nimesoma katika kanuni alizotuwekea humu ndani Msomi Wakili Mselewa sijaona sehemu yeyote ambapo maadili aliyoyakiuka Wakili Msomi Msando na wala sijaona kifungu chochote kilichovunjwa kwenye kanuni tajwa. Kanuni nyingi zinaonekana kujikita zaidi kumbana wakili kimaadili pale anapokuwa anatekeleza majukumu yake ya kiuwakili na si vinginevyo.

4. Kutokana na kwamba kanuni za mawakili zinacover maadili ya wakili pale anapokuwa anatekeleza majukumu yake ya uwakili tu nashawishika kuamini kwamba lengo lilikuwa kutofautisha maisha binafsi ya wakili na kazi yenyewe ya uwakili.

Ndugu wanajamvi ni kwa findings hizi namshauri Tundu Lissu na TLS iachane na Msando wafanye shughuli zingine kwani hajavunja kanuni wala sheria za uwakili, hajavunja sheria nyingine yeyote na hata kama kutakuwa kuna sheria imevunjwa japo sidhani utakuwa sheria ya mitandao (japo sidhani)

Ndugu wasomi na wanajamvi kwa ujumla alichokifanya Msando ni kinyume cha maadili ya jamii lakini si kinyume cha sheria. There is a known belief that law cannot enforce morality, something may be moral wrong lakini kisheria kikawa sawa. Kama tutaruhusu TLS kuwachukulia hatua mawakili hata pale wanapokuwa wanafanya mambo yao mengine tofauti kabisa na uwakili it will be to open a Pandora box and or floodgates ambapo TLS itashindwa kufanya mambo yake mengine. Inajulikana kwamba once an advocate always an advocate na tuna mawakili zaidi ya elfu sita na idadi inaongezeka kwa kasi lakini zaidi ya nusu ya mawakili hawapractice uwakili wengine ni wafanya biashara, wengine wamejiajiri na Kilimo wengine ni wasanii etc sasa sidhani kama ni busara kusema kanuni za uwakili ziapply mutatis mutandis hadi kwa wakili ambaye anajilimia kule usangu no no no. Kanuni ziapply kwa wakili anayefanya misconduct in the course of practicing.

Swala la kusema Wakili Msomi Albert Msando amewadhalilisha wanasheria ni too remote and absurd, anawadhalilisha vipi? Hivi mawakili wana alama? Kila anayefanya jambo baya anatajwa kwa taaluma yake? Ni lazima tuchore msitari kwamba jambo fulani limefanywa katika mazingira gani, lile analolifanya kama wakili litadhalilisha taaluma lile analolifanya kama mfanya biashara litadhalilisha wafanya biashara, lile analolifanya kama mkulima litadhalilisha wakulima. Hebu tujiulize pale mtu amesoma uwakili baadaye akasoma udaktari halafu ikatokea akiwa hospitali akihudumia wagonjwa akamchoma mgonjwa sindano kwenye mfupa mgonjwa akadhulika hivi TLS au wanasheria watasema daktari huyu ambaye ni mwanasheria pia kwamba amewadhalilisha sana wanasheria? Let say the same person akiwa mahakamani kama wakili akamtukana judge je madaktari watasema wakili huyu ambaye ni daktari amewadhalilisha madaktari?

Ni lazima muktadha wa jambo husika uzingatiwe for all purposes kwangu mimi sioni kama Wakili Msomi Albert Msando amewadhalilisha wanasheria kwa sababu hajafanya hayo katika muktadha wa kisheria bali Msando ni promota wa wasanii na anamiliki Club nadhani watu wa kumchukulia hatua ni chama cha mapromota na wamiliki club ndiyo kimshughulikiea kama nipo na si TLS kwani aliyoyatenda ameyatenda katika muktadha huo.

Msando ni Promota si wakili Tundu Lissu atadeal na wanasheria wanaokiuka maadili wakiwa katika majukumu ya uanasheria.
 
Mkuu kama ni mwanasheria ndio haruhusiwi kuwa na personal life?? Hujaona video flani ya Trump akishika papuchi za madada mtaani akipiga nao picha?

Watanzania tunapenda sana kujifanya tunajua what's right and what's not☹..wamuache na Maisha yake kama kuhusu familia yake wamuache atamalizana nayo yeye mwenyewe
 
Ndiyo shida ya kuongozwa na less intelligent people!
 
Mkuu kama ni mwanasheria ndio haruhusiwi kuwa na personal life?? Hujaona video flani ya Trump akishika papuchi za madada mtaani akipiga nao picha?

Watanzania tunapenda sana kujifanya tunajua what's right and what's not☹..wamuache na Maisha yake kama kuhusu familia yake wamuache atamalizana nayo yeye mwenyewe
Haujasoma ukaelewa uzi wangu
 
Wakili wa Instagram

Aisee Leo nimeamini Kuwa Taaluma ya Sheria ni ya Hovyo hapa Nchini Kumbe hawana Professional Board Kama (NBAA) ,(CRB), (TIOB),( PSPTB) n.k

Kumbe pamoja Na Kuvaa Visuti vyenu vyeusi Hamna Professional Board?
 
Mkuu kwenye professions nyingi kuna kitu kinaitwa "profession ethics" hiki ni kitu muhimu sana ikiwemo how to conduct yourself in public. Sijui hizi za wanasheria zikoje lakini hizi zinaweza kabisa kusababisha mtu kufukuzwa kwenye profession husika na hivyo kutokuwa na kibali tena cha kufanya lolote lile kuhusiana na profession hiyo.

hapo ndipo mtakapoteleza. Tena yuko anakula bata halafu mnataka kumuwekea uzibe, acheni hizo
 
Mimi sidhani alichokifanya Msando ni tatizo la TLS.

Kama alichokifanya ni tatizo basi labda ni tatizo kwa mkewe na ndoa yao.

Nje ya hapo sioni tatizo kwa sababu wahusika wote ni watu wazima na binafsi sijali mambo wafanyayo watu wazima, mambo ambayo wote wameridhia.
 
Mkuu kwenye professions nyingi kuna kitu kinaitwa "profession ethics" hiki ni kitu muhimu sana ikiwemo how to conduct yourself in public. Sijui hizi za wanasheria zikoje lakini hizi zinaweza kabisa kusababisha mtu kufukuzwa kwenye profession husika na hivyo kutokuwa na kibali tena cha kufanya lolote lile kuhusiana na profession hiyo.
Za wachungaji unazijua mkuu? Maana kuna mmoja namjua anapiga mlegezo kichizi.
 
  • Thanks
Reactions: 247
Wakili wa Instagram

Aisee Leo nimeamini Kuwa Taaluma ya Sheria ni ya Hovyo hapa Nchini Kumbe hawana Professional Board Kama (NBAA) ,(CRB), (TIOB),( PSPTB) n.k

Kumbe pamoja Na Kuvaa Visuti vyenu vyeusi Hamna Professional Board?
IPO Mkuu.. Sema umeropoka bila kuuliza
 
Back
Top Bottom