Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,143
Mkuu,umeiona hoja yangu. Hongera!Mm nashangaa sana kwa mkulu kusema mtu akikutwa na kitu haramu awekwe ndan hata kama mtetez wake nae awekwe hivi kwa stail hii ya kubambikiwa kesi siwataenda wasio na hatia?
Mageuzi ya kweli ya kidemokrasia yalianza na nyie watu wa sheria na wafanyakazi, mpaka leo dunia inaendelea kudhihirisha umuhimu wa wanasheria katika kujenga usawa. Rejea walichofanya Marekani dhidi ya ubabe aliotaka kuja nao Trump. Ofkoz, hatupo level sawa ya kidemokrasia lakini bado mnatakiwa muonyeshe japo kwa kutoyumbishwa katika kutoa hukumu na mtoe hukumu za haki bila kujali vimemo vya wanasiasa. Sasa nimemsikia Kamishna wa Madawa ya kulevya akiagiza kupitiwa mafaili yote ya kesi za madawa ya kulevya mlizohukumu.Imekuwa ikisemwa sana kuwa wapo askari polisi wasio waaminifu wanaowabambikia wananchi kesi kwa lengo la kuwaomba rushwa au kuwakandamiza. Ndiyo maana,sisi Mawakili hujitokeza kuwatetea watuhumiwa kwakuwa si wote waliotenda kweli
Huko mkoani Arusha,askari polisi mmoja amekamatwa kwa kuwabambikia wananchi madawa ya kulevya kama bangi kwa lengo la kuomba rushwa. Askari huyo aliyekamatwa,kwa mujibu wa ITV Habari,ni kielelezo na uthibitisho kuwa kubambika kesi kupo
Kimsingi,kutaja au kuhoji au hata kushtaki mwananchi kwa tuhuma fulani si mwisho wa mambo. Ni mwanzo tu unaoficha mambo mbalimbali yakiwemo ya watu kusingiziwa kesi au vizibiti. Ndiyo maana, ipo haja ya kuwa makini na kesi za wananchi na kuacha mapambano ya kimahakama yaseme na kutenda haki.
Lakini hajasema atakayekuja kumdhamini naye awekwe ndani.kutetea maana yake fasaha ni kumsaidia, kumficha, kuiingilia, mamlaka inayohusika kuishawishi ili isimtie hatiani,kuharibu ushahidi kwa lengo makusudi,mimi nilielewa hivyo.Mm nashangaa sana kwa mkulu kusema mtu akikutwa na kitu haramu awekwe ndan hata kama mtetez wake nae awekwe hivi kwa stail hii ya kubambikiwa kesi siwataenda wasio na hatia?
Hali kama hiyo inasemwa kuwepo Tanzania nzima
Una mtetea vipi WEMA ili hali ali CONFESS mwenyewe????Masikini Wema Sepetu akasumbuliwa buuure.
Nchi ya viongozi wanaoongozwa na SIFA ZA KIJINGA
Unajuaje aliconfess ili tu kuondoa usumbufu na kupotezewa muda?Una mtetea vipi WEMA ili hali ali CONFESS mwenyewe????
We mpuuzi KWELI kwa utetezi unaosema.......Yaani ukubali tu kisa MUDA wako.....VIROBA vya asubuhi asubuhi hivi....Unajuaje aliconfess ili tu kuondoa usumbufu na kupotezewa muda?
Kuna mtu mkubwa hapa nchini anafanya mambo ya kichochezi, sijui nani atamchukulia hatua mtu huyu? Anatakiwa aache mambo ya kijinga kijinga! Hivi hao raia waliomkamata huyo aliyewabambikia madawa ya kulevya kwa nini hawakumwua?Hali kama hiyo inasemwa kuwepo Tanzania nzima
Wewe kisukule unashangaza sana...huelewi hata ninachomaanisha pimbi jike wa Lumumba wewe.We mpuuzi KWELI kwa utetezi unaosema.......Yaani ukubali tu kisa MUDA wako.....VIROBA vya asubuhi asubuhi hivi....
Avatar na unayoandika asubuhi hii inathibitisha WEWE ni either ni mbwia MADAWA YA KULEVYA au MNYWA VIROBA ASUBUI KUPATA MZUKA......Wewe kisukule unashangaza sana...huelewi hata ninachomaanisha pimbi jike wa Lumumba wewe.
Unajua unapomsikiliza mkulu anapoongea na vyombo vyetu vya usalama unapatwa na woga, askari wetu hawapigiwi wanacheza sasa mkuu anapowapigia zumar hivi sijui tunataka ku-achive nini. Mungu atupe salama lakini hii safari naiona nzito huko tuendako.