singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Katika hali inayozidi kuonesha wanasiasa nchini wamezidi kuweweseka na kasi ya rais, Dr. John Pombe Magufuli katika kukusanya mapato, kusimamia uwajibikaji katika taasisi za Umma, kupambana na rushwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto zinazolikabili taifa kama elimu na afya.
Jana kupitia gazeti la Mwananchi, Professa wa uchumi aliyewahi kuwa mshauri wa rais MWINYI katika maswala ya uchumi kipindi cha awamu ya pili, mshauri wa rais wa Uganda katika maswala ya uchumi na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa chama cha Wananchi(CUF), Prof. Ibrahimu Harouna Lipumba amenukuliwa akimtaka Rais John Pombe Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake kwa kile alichokiita kuwa kwa sababu rais amejivita joho la kuwa rais wa Wanyonge.
Madai haya ya Lipumba yamekuja siku chache baada rais kuwataka Mawaziri, Manaibu mawaziri, na Makatibu wakuu wachangie shilingi za kitanzania milioni moja(1) katika mishahara yao kuchangia elimu huku akiahidi yeye mwenyewe(rais), Makamu wake na Waziri Mkuu kuchangia shilingi milioni sita(6) kila mmoja , ili zifike mil. 100 kusaidia changamoto za elimu bure Mkoani Dar es Salaam. Rais aliyasema hayo wakati akiongea na wazee wa Dar es Salaam.
Sijui Lipumba kayasema haya kama mtanzania wa kawaida mwenye uhuru wa kutoa maoni au kama mtaalam wa Uchumi.
Kama mtanzania wa kawaida, Lipumba anapaswa kujia kuwa:
1. Mshahara wa mtumishi yeyote awe wa Umma au sekta binafsi ni siri, kuwa rais hakuwezi kuwa sababu ya kumuondolea haki hiyo ya mshahara wake kutohafamika. Kufanya hivyo ni kutomtendea haki.
2. Ni dhana potofu sana tena sana kuwaaminisha watu kuwa rais wa wanyonge ni yule aliyetangaza mshahara na marupurupu yake. Mshahara wa rais unaweza kuwa shilingi laki moja lakini kama hana uzalendo na rasilimali za nchi, hana huruma na watu wake ni kazi bure. Rais wa Wanyonge atakuwa wa aina ya Magufuli na siyo wa kutangaza mshahara wake.
3. Siyo rais pekee anayelipwa mshahara ambao pengine unadhaniwa ni mkubwa kwa kodi za wananchi. Wenye viti wa Vyama vya siasa, Wabunge, wakurugenzi wa mashirika na taasisi za Umma nao kwenye kundi hilo. Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa chama cha wananchi(CUF) ) kwa kipindi kirefu sana, nani alijua mshahara wake? Au kwa kuwa yeye hakujipambanua kuwa ni Mwenyekiti wa chama kinachotetea maslahi ya Wanyonge?
4.Rais kuamua kukatwa msahara wake kwa ajili ya kukabiliana na changamoto za elimu ni utashi wake , ni upendo wake kwa wananchi wake, ni uzalendo wake wa kutaka kutumia kidogo alicho nacho kwa manufaa ya wengi, huruma yake kwa watanzania. Maamuzi haya yaliyotokana na moyo wake wa huruma yasiwe sababu ya Lipumba na wanasiasa wengine na watu wengine kutafuta la kusema kamhusu rais. Kufanya hivyo ni kumkatatisha tamaa rais katika juhudi zake za kutaka kuonesha kuwa kiongozi wa kuigwa na wengine ili kumfuata ili kuijenga tanzania yenye watu wazalendo, watu wanaopendana, watu wanaojali wengine na wenye hurma.
Kama mtalaamu wa Uchumi nawiwa kuyasemma haya kumhusu Lipumba, najua siyo mazuri sana lakini inapobidi tunalazimika kuyasema.
1. Watanzania hatuna la kujivunia kutoka kwa Prof. Lipumba kama mtaalam wa Uchumi zaidi ya kubaki tunaimba ni mtaalam wa uchumi aliyebobea. Kila anapopita anaimbiwa wimbo huo huo, mtaalam wa uchumi huyo anapita, lakini tukirudi kwenye uhalisia sina kumbukumbu ya nini cha kujivunia kutoka kwake.
2. Amekuwa mshauri katika masuala ya uchumi kwa marais Alhaji Ali hassan Mwinyi wa Tanzania, na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda kwa nyakati tofauti. Nini cha maana sana cha kujivunia kutoka kwa viongozi hawa wakati yeye akiwa mshauri wao? Angekuwa mshauri wa rais yeyote wa Kenya, leo hii tungeweza kujigamba hata kama hakuhusika kuifanya nchi hiyo kufikia kuwa yenye uchumi wa kati.
Kila zama zina mambo yake, Lipumba amuache Dr. Magufuli afanyekazi yake labda atatufikisha kule ambako Lipumba alishindwa kuwashauri mabosi wake vizuri ili watufikishe huko.