Lipumba: Mgawo wa umeme JK alaumiwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Mgawo wa umeme JK alaumiwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 20, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,430
  Trophy Points: 280
  Lipumba: Mgawo wa umeme JK alaumiwe


  na Neema Kishebuka, Tanga
  Tanzania Daima


  [​IMG]
  WAKATI Watanzania wakiendelea kukabiliwa na tatizo la mgawo wa umeme, Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema hali hiyo imechangiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa kushindwa kutoa maamuzi kuhusu nini kifanyike ili kulinusuru taifa.
  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wakati akihutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika katika mji mdogo wa Pongwe, nje kidogo ya Jiji la Tanga.
  Profesa Lipumba alisema, Rais Kikwete analifahamu vizuri tatizo la mgawo wa umeme nchini tangu alipokuwa Waziri wa Nishati na Madini, lakini kutokana na kukosa ujasiri wa kufanya maamuzi, tatizo hilo limekuwa la kudumu na kuwafanya Watanzania waendelee kuishi katika mazingira ya giza.
  “Suala la mgawo wa umeme, limekuwa tatizo la kudumu licha ya serikali kuahidi kulitatua bila kujua kuwa kupuuzwa kwa suala hilo kunawaathiri Watanzania kiuchumi, kielimu na kiafya,” alisema Profesa Lipumba.
  Alisema kuwa Machi 3, mwaka huu, Rais Kikwete alifunga mjadala kwamba serikali haitanunua mitambo ya kufua umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Dowans na kujigamba kuwa tatizo la mgawo wa umeme, halitatokea tena, lakini cha kushangaza ni kwamba tatizo hilo limekuwa la kudumu.
  Profesa Lipumba alisema kushindwa kutatuliwa kwa tatizo hilo, kunatokana na udhaifu mkubwa uliopo ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Hivi sasa, makali ya mgawo wa umeme, yameongezeka kutoka megawati 90 hadi kufikia 150 kutokana na kupungua kwa kima cha maji katika vituo vya kuzalisha umeme vya Kihansi, Pangani na Kidatu.
  Kwa upande mwingine, Profesa Lipumba alilaani kitendo cha polisi kumkamata Mbunge wa Viti Maalumu, Nuru Bafadhil (CUF) na kumfikisha mahakamani kwa madai ya kumkashifu Rais Kikwete, kwamba anachekacheka badala ya kushughulikia changamoto zinazolikabili taifa. Alisema maneno aliyoyatamka mbunge huyo ni ya msingi na kwamba kama ni suala la kushitakiwa, angeanzwa yeye kwani amekuwa akiyatamka maneno hayo mara kwa mara. Lipumba alisema tatizo la kuchekacheka, limesababisha kuzorota kwa maendeleo ya wananchi, huku baadhi wakiendelea kutaabika wakati Tanzania ina fursa nyingi za kuwawezesha kuondokana na umasikini.
   
Loading...