Lipumba: Lindi, Mtwara wana hoja nzito

Lipumba: Lindi, Mtwara wana hoja nzito

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kuwa wananchi wa Lindi na Mtwara kukataa gesi asilia isisafirishwe kwenda Dar es Salaam kwa njia ya bomba ni hoja ya msingi ambayo chama chake kinaiunga mkono.
Lipumba alitoa kauli hiyo mjini Lindi juzi wakati akaihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili.
CUF walikusudia kufanya maandamano kabla ya mkutano ili kupinga gesi hiyo kusafirishwa kwenda Dar es Salaam lakini maandamano hayo yalisogezwa mbele na polisi hadi Aprili 15.
Akiwahutubia wananchi hao, Lipumba alisema CUF inakubaliana na hoja ya wananchi hao ya kutaka gesi asilia ibaki huko kwani viwanda hivyo vitakapokuwa tayari kujengwa kusini wananchi watapata ajira mbalimbali.
"Mimi ni mzaliwa wa Tabora, nalizungumzia suala hili kama mzalendo sio kwa uzawa wa mikoa ya kusini. Nalizungumzia suala hili kiuchumi na kiuchambuzi kwamba madai yenu ni halali na ya kuungwa mkono," alisema.
Lipumba aliongeza kuwa kuna maeneo makubwa yenye nafasi ambayo yakitumika vizuri, gesi itakuwa malighafi katika kufua umeme wa viwanda mbailimbali.
"Rais Jakaya Kikwete aliwadanganya, siku ya sikukuu ya Mashujaa ambayo ilifanyika kitaifa Mtwara mwaka 2011, alieleza mpango mkubwa wa kutumia gesi na kuweza kuanzisha viwanda na kuhakikisha bandari ya Mtwara inakuwa kubwa na mambo mazito yatakayokuja kwa sababu ya gesi," alisema.
Alisema kuwa baada ya muda mfupi tangu atoe ahadi hiyo, ghafla wananchi wa Mtwara wakasikia unazinduliwa mradi wa kusafirisha gesi hiyo kutoka huko kwenda Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.
Lipumba pia alilitaka Jeshi la Polisi kutozuia maandamano yao kwa kuwa ni ya amani na kwamba nchi hii ni ya wote huku akionya kuwa kuyazuia kunaweza kusababisha vurugu.
Naye mbunge wa Lindi Mjini, Salum Baruani, akitoa tamko la kuahirisha maandamano hayo, alisema kuwa serikali lazima itoe tamko kuhusu swala la gesi asilia na hoja nyingine ya viwanda vya gesi kujengwa sehemu ambayo gesi imegunduliwa.


​



[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Fatuma Mnyeto, Lindi



[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
[/TD]
source: Tanzania daima
 
kiuchumi zaidi na wala si propaganda za kisiasa,kaza buti lipumba ww ndio tumaini letu wana kusini
 
Back
Top Bottom