Lipumba: Hali ya uchumi ni mbaya, Serikali ichukue hatua

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,207
2,000
Lipumba: Hali ya uchumi ni mbaya, Serikali ichukue hatua


Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza na waandishi wa Habri jijini Dar es Salaam jana wakati akitoa tamko la kulaani kwa kitendo cha Naibu Spika wa Bunge la Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuwanyanyasa na kuwazalilisha Wabunge wa upinzani akiwepo Kiongozi wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe. Picha na Venance Nestory

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameitaka Serikali kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo ya kiuchumi, kwa kuwa hali ilivyo sasa ni mbaya.

Profesa Lipumba ambaye pia ni profesa wa uchumi alisema hivi karibuni Dar es Salaam kuwa hali ya uchumi imezidi kudorora na kusababisha maisha ya wananchi wengi kuwa magumu.

“Vijana wa siku hizi wengi hawana simile kushughulika na mambo yanapokwenda sivyo, ajabu ni kwamba wanaofanya mambo hayo yawe magumu wamekuwa wepesi wa kutetea kwa hoja zisizo na msingi kwa masilahi yao binafsi,” alisema.

Akizungumzia maazimio yaliyofikiwa kwenye Kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF kilichofanyika Desemba 21-22 mwaka huu Dar es Salaam, alisema hatua ya kupandishwa kwa gharama za umeme iliyotangazwa hivi karibuni na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ni miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi, jambo ambalo lingeweza kuzuilika kwa shirika hilo kudhibiti wizi wa nishati hiyo.

Kuhusu hali ya kisiasa nchini, Profesa Lipumba alisema Baraza Kuu limetoa wito kwa vyombo vya Dola kuwa na weledi na uadilifu na kuacha kutekeleza amri za wanasiasa zisizojali utawala wa sheria na haki za binadamu ili vipunguze uhasama baina yao na raia.

“Serikali pia isitumie Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika kushughulikia masuala ya uvunjifu wa sheria katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, badala yake kazi hiyo ifanywe na Jeshi la Polisi kwa mujibu wa taratibu za kisheria. Nao pia waongezewe uwezo wa kiutendaji,” alisema.

Alisema CUF inaona si vyema kutumia JWTZ kudhibiti vurugu kwa kuwa wanajeshi hao hawana mafunzo ya kukamata wananchi wenye tuhuma za uhalifu isipokuwa wamefundishwa jinsi ya kulinda usalama wa nchi katika mipaka.
 

tofyo

JF-Expert Member
Jul 18, 2013
2,690
2,000
maneno mazuri

mbowe na wafuasi wake hawanyanyaswi ila hawana hekma bungeni.
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,853
1,250
kila siku huwa najiuliza ni lini serikali hii itafumbua macho na kutumia watu kama Lipumba kwa maendeleo ya taifa hili. wakati ufike siasa zisizidi mahitaji ya maendeleo katika Nchi hii
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,155
2,000
Profesa mnafiki na alieishiwa hoja na busara,Uchumi wake yeye ni wa kwenye Makaratasi tuu. Sababu haiwezekani na haiingii akilini kila siku yeye kuhubiri hali ya Uchumi ni mbaya huku the sametime akiendelea kuunga mkono visababishi/serikali na watu wanaosababisha Uchumi wetu kudidimia kila uchwao. Sometimes namuonaga hana tofauti na yule wa Gambani anaejiita first class economist.
 

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
14,155
2,000
kila siku huwa najiuliza ni lini serikali hii itafumbua macho na kutumia watu kama Lipumba kwa maendeleo ya taifa hili. wakati ufike siasa zisizidi mahitaji ya maendeleo katika Nchi hii

Acha kujitoa ufahamu ndugu au unataka kusema kuwa umezaliwa au unapata ufahamu leo? Ni Maprofesa,Phd Holders na wasomi wote wa kada hiyo ambao walishawahi kufanya/wanafanya kazi Serikalini nini cha maana walicho-deliver kwa Watanzania kikawa na Positives Impact au unataka tuanze kuorodhesha hao Maprofesa?
 

myhem

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
932
500
ukitaka kujua kuwa maisha yamekuwa magumu sasa hivi, angalia jinsi majambazi siku hizi yanavyovamia hata vibanda vidogo vidogo vya mpesa au tigo na hata maduka ya kawaida huku wakitumia silaha nzito ambazo thamani yake inazidi bei ya bajaj.zamani tulizoea kusikia wanavamia bank au ofisi kubwa zinazotunza fedha
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,784
2,000
maneno mazuri

mbowe na wafuasi wake hawanyanyaswi ila hawana hekma bungeni.
Hoja iliyopo mezani ni hali ya uchumi,suala la Mbowe linaingiaje hapo?hakika wewe ni kilaza wa nguvu sana,hujui kinachoendelea!
 

TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,784
2,000
kila siku huwa najiuliza ni lini serikali hii itafumbua macho na kutumia watu kama Lipumba kwa maendeleo ya taifa hili. wakati ufike siasa zisizidi mahitaji ya maendeleo katika Nchi hii
Teh teh teh!it is easier said than done!
 

Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,815
2,000
Hali ni mbaya na serikali imeshikwa pabaya, kumekosekana ubunifu kwa serikali ya sasa ambapo asilimia kubwa ya mapato yanaishia kwenye shuguli za kuendesha serikali na kiduchu sana ndio kinaelekezwa kwenye shughuli za maendeleo directly. Kibaya zaidi ni pale ambapo wahusika wanapokosa utu na kujipima hili kupunguza gharama ambazo hazina ulazima, waweze kusaidia sehemu zingine za jamii.

Serikali hipo madarakani sasa ni miaka nane, hivi wahusika wanaweza kuja mbele na kuelezea mafanikio ya kiuchumi kwenye sector za ajira au kwenye kuwawezesha watanzania hata huko kwenye kutengeza juisi. Wao sana sana mwarobaini wa kipato chao ni kwenye ongezeko la kodi za bidhaa zile zile sana sana magari bandarini. Watu wengi sana waliokuwa kwenye biashara hii sasa naona wameanza kupunguza kasi labda mteja alete hela yake mwenyewe na adili na TRA yeye mwenyewe. Hapo tena nimesoma mwakani kodi inaenda juu for 50%, hata sijui akili hipo wapi. Huwezi ku-limit the growth of car ownerships wakati wewe mwenyewe huna service ya kutosha kupeleka watu 'A to B' during 'rush hours' na daladala kwa kweli nyingi sana zinahitaji uboreshaji, vilevile bado sana asilimia kubwa yetu wanasafiri na magari binafsi kwenda mikoani.

Ukirudi kwenye sector za ajira ndio kabisa unless the government comes clear on what terms SME's contribute in the employment hii biashara ya mikopo inabidi isitishwe (sisemi wajasiriamali wasisaidiwe in general), maana kutwa sijui serikali inadai hela tuliyotoa tumerudisha kwenye mikopo ya kampuni ndogo ndogo (so far kuna watu wangapi wanafanya kazi huko). Maana ukute mtu hana mpango wowote sanasana akipata mkopo anenda huko 'Gounzong' or some ananunua vibwebwe na duka lake shughuli imeisha. Au mtu anaenda ananunua magari anauza shughuli imeisha na kulipa madeni, lakini zero employment created. Kunahitajika muonekano wa njia sahihi za SME lazima wawekeze kwenye jamii, hili serikali inapotoa mikopo ya bei rahisi ijue kuna watu between 5 to 20 are gonna get a salary. Mbona kuna sehemu nyingi bado un exploited in the service sector machines, equipments and the sector segmentation. Huko kwenye manufacturing pia bado sana people need to get bold si kila mtu awe na saloon any ya nguo, nywele or as in kiosk.

Hawa wanasiasa ni wababaishaji tuache kusikiliza vitu ambavyo tunavijua we should ask how are they going to solve those problems which we can all see. Hizi hadithi za kutukumbusha kumbusha kila mara zinachosha, nyie wa upinzani given the opportunity how would you go about solving the existing problmes in details, considering rushwa, ujambazi et al to do with the protection of small businesses and nurturing the sector.

Sasa mwanasiasa anakwambia kupanda kwa bei ya gesi kuta athiri matumizi mengine ya mtumiaji (true) wakati mtatiro anapinga gesi isitoke Mtwara, at the same time serikali inagharamia almost more than half the unit your paying currently, hili wewe upate umeme kwa bei che. Halafu watanzania hawana hata habari kama jamaa wanatumia millioni $30 kila mwezi kwa Mr Symbion ku subsidize gharama za umeme mpaka lini wakati gesi tunayo, mkiambiwe mchangie wenyewe ndio hayo malalamiko haiwezekani, jamaa wakizima mitambo serikali inadaiwa (siafiki ongezeko, but people need to pay attention to politics, there were other altenatives).
 

Nabihu

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
283
225
Profesa mnafiki na alieishiwa hoja na busara,Uchumi wake yeye ni wa kwenye Makaratasi tuu. Sababu haiwezekani na haiingii akilini kila siku yeye kuhubiri hali ya Uchumi ni mbaya huku the sametime akiendelea kuunga mkono visababishi/serikali na watu wanaosababisha Uchumi wetu kudidimia kila uchwao. Sometimes namuonaga hana tofauti na yule wa Gambani anaejiita first class economist.

Wanafiki Huwaoni Kule Mjengoni Wanaobadilisha Matumizi Ya Pesa Za Bunge Kuwa Matumizi Yao Binafsi Wanakwendea Dubai Acha Chuki za Kigango
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,853
1,250
Acha kujitoa ufahamu ndugu au unataka kusema kuwa umezaliwa au unapata ufahamu leo? Ni Maprofesa,Phd Holders na wasomi wote wa kada hiyo ambao walishawahi kufanya/wanafanya kazi Serikalini nini cha maana walicho-deliver kwa Watanzania kikawa na Positives Impact au unataka tuanze kuorodhesha hao Maprofesa?

tatizo lako unakariri
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,995
1,500
Tunaambiwa ni profesa wa uchumi aliyebobea lakini hatujasikia kaanzisha hata KIKOBA cha mfano,

hamuoni mwenzake mamvi anampango wa kutununulia bodaboda vijana wote wa dar ila sijui nani atakuwa abiria.
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,308
2,000
Tunaambiwa ni profesa wa uchumi aliyebobea lakini hatujasikia kaanzisha hata KIKOBA cha mfano,

hamuoni mwenzake mamvi anampango wa kutununulia bodaboda vijana wote wa dar ila sijui nani atakuwa abiria.
Dr.Slaa ni dr wa kanisa ana vigango vingapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom