Mnapotoa mapendekezo pia muwe mnafahamu katiba ya JMT inasemaje, Vinginevyo hili litakuwa sio jukwaa la GTs.
**** mtu mwingine aliwahi ku propose kwamba Lipumba awe mgombea mwenza wa Dr. Slaa or vice versa. This is a wishful thinking. Under our constituttion this CAN NOT HAPPEN. Ni sawa na kuomba mbingu na dunia zishikamane.
Turudi kwenye topic yetu ya Lipumba kuwa WM. Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inaelekeza jinsi ya kumpata WM (Waziri Mkuu)
Ibara 51 (1) - (2). Rais Mteule atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la uchaguzi kutokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi kuwa WM wa JMT. Naye hatashika madaraka hayo mpaka uteuzi wake uwe umethibitishwa na bunge.
Nini maana yake
- Ili Lipumba awe WM, kwanza lazima awe mbunge wa kuchaguliwa
- Ili Lipumba awe WM, lazima CUF iwe na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vingine vya siasa
Baada ya kufahamu hayo naomba sasa uje tujadiliane!
Hiyo inajulikana si kila kitu lazima kiandikwe. Aliye sema awe PM ana maana kuwa kama ukawa watakubaliana mgombea wa urais basi Lipumba akagombee ubunge ili ukawa ikishinda ateuliwe kuwa PM kwenye serikali ya ukawa.
Na mimi pia ni hivyo kuwa akagombee ubunge ili ateuliwe kuwa waziri wa fedha kama ukawa itashinda.
Cuf wakiona post yako hii wanaweza kukutwanga na mawe hujui kuwa lipumba kule cuf ndiyo mungu wao.kuwa professa na uwaziri wa fedha kuna uhusiano gani? Lipumba ni professor wa uchumi sio fedha au biashara. Finance inataka mtu mwenye uzoefu wa kuongoza sio kusoma bali kuongozi kitengo cha finance kama Bank, investment company au Central bank kama BOT. Ukiweka wasomi ambao hawajawahi kufanya kazi tutaona pumba tu kwani watu si vitabu
Kwa mujibu wa katiba iliyopo waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pia atokane na wabunge walio wengi bungeni!
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inahitaji waziri mkuu imara katika serikali ijayo! Mtu ambaye anaweza kusimamia nidhamu ya watendaji wa serikali na uchumi wa nchi! Mtu ambaye atapandisha heshima ya serikali kitaifa na kimataifa!
Hivyo kwa hitaji hili muhimu, UKAWA wana kila sababu ya kumshawishi Mhe. Lipumba agombee ubunge ili Rais ajaye kutoka UKAWA aweze kumteua kuwa waziri mkuu wa Tanzania!
Mungu ibariki Tanzania!
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inahitaji waziri mkuu imara katika serikali ijayo! Mtu ambaye anaweza kusimamia nidhamu ya watendaji wa serikali na uchumi wa nchi! Mtu ambaye atapandisha heshima ya serikali kitaifa na kimataifa!
Hivyo kwa hitaji hili muhimu, UKAWA wana kila sababu ya kumshawishi Mhe. Lipumba agombee ubunge ili Rais ajaye kutoka UKAWA aweze kumteua kuwa waziri mkuu wa Tanzania!
Mungu ibariki Tanzania!
Kwani kuna tatizo gani Lipumba kuwa PM hata kama siyo Mbunge. Si Rais Slaa atamteua kuwa Mbunge kisha PM?