Lipumba amlipua Chenge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba amlipua Chenge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuandamane, Sep 1, 2009.

 1. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  [​IMG] MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameeleza kusikitishwa na kigugumizi cha serikali cha kushindwa kumchukulia hatua aliyekuwa waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge, kwa madai ya kuhusika katika kashfa ya ununuzi wa rada.
  Alisema inashangaza hadi sasa kuona serikali imekaa kimya kuhusu suala hilo, licha ya Taasisi ya kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai nchini Uingereza, (SFO), kuwasilisha ripoti yake serikalini.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, baada ya kuwasilisha mada ya Dira ya Maendeleo ya Taifa kuelekea mwaka 2010 katika semina iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Profesa Lipumba alisema Chenge alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, aliingia mikataba mingi isiyo na tija, ambayo inaendelea kuigharimu nchi.
  “Nashangaa mpaka sasa serikali haijachukulia hatua zozote dhidi ya Chenge, licha ya SFO kuwasilisha ushahidi serikalini, ambao unamhusisha yeye na mfanyabiashara mwenye asili ya Kiasia, Saileth Vithlani,” alisema Profesa Lipumba.
  Hata hivyo, alisema pamoja na kuwapo kwa mikataba mingi ya kifisadi, serikali inaweza kutumia kura ya turufu kuyataifisha mashirika yanayoendelea kuneemeka na mikataba hiyo pamoja na kuwa na uwezo wa kubadilisha sheria, ili kuweza kuchukua hatua kujinusuru katika mikataba hiyo mibovu.
  “Mikataba mingi ya madini ina harufu ya rushwa, lakini serikali inaweza kuondokana na mikataba hiyo kwa kutumia kura ya turufu kuyataifisha mashirika hayo,” alisema.
  Februari mwaka huuu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema bungeni kuwa uchunguzi kuhusu ununuzi wa rada, haujakamilika na kwamba utakapokamilika wabunge watajulishwa.
  Pinda alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya papo hapo bungeni. Swali hilo aliulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, ambaye pia ni Mbunge wa Wawi (CUF).
  Chenge, ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Miundombinu Aprili mwaka jana, kutokana na kuwa chini ya uchunguzi wa SFO, akituhumiwa kwamba fedha alizojiwekea katika Kisiwa cha New Jersey zilitokana na mgawo wa rushwa ya ununuzi wa rada.
  Hata hivyo Chenge, maarufu kama ‘Mzee wa Vijisenti’ mara kadhaa amekanusha kuhusishwa na rushwa katika manunuzi ya rada.
  Aliwahi kukaririwa akisema kwamba fedha alizojiwekea benki katika kisiwa hicho ni vijisenti, lakini mara mbili ametoa kauli za kutatanisha juu ya vyanzo wa dola milioni 1.5 katika akaunti yake, akieleza ni malipo yake halali kwa kazi za uanasheria.
  Pia aliwahi kusema fedha hizo zimetokana na urithi na akiba ya familia, na katika fedha hizo mkewe anamiliki asilimia 25.
  Kabla ya rada hiyo kununuliwa, kuliibuka mjadala mkali nchini, wengi wakipinga, kwa sababu ilikuwa ya gharama kubwa, wakati Tanzania ingeweza kupata rada mbadala kwingineko kwa gharama nafuu.
  Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa, ilisisitiza kununuliwa kwa rada hiyo, kwa sababu za kiusalama, ambayo ilinunuliwa kwa dola za Marekani milioni 40.
  Hadi sasa ni Vithlani pekee aliyefunguliwa mashitaka rasmi mahakamani kutokana na kashfa ya rada, lakini wakati mashitaka hayo yanawasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mshitakiwa hakuwapo na tangu wakati huo anasakwa kuja kujibu mashitaka yake.
  Awali akitoa mada katika semina hiyo, Lipumba alisema ingawa takwimu zinaonyesha uchumi nchini unakua, lakini katika malengo ya milenia Tanzania haijafanya lolote.
  Alisema hadi sasa kuna watu bado wanaishi maisha ya umaskini wa kutupwa na kwamba maskini nchini wameongezeka kutoka milioni 11.4 mwaka 2001 hadi kufikia milioni 12.9 mwaka 2007.
  Alisema kutokana na hali hiyo, ni muhimu kwa wadau, vikiwamo vyama vya siasa kukubaliana na dira ya maendeleo ya nchi na kila chama kitakachoingia madarakani kitekeleze sera zitakazokuza uchumi unaoleta tija na neema kwa wananchi wote.
  Pamoja na hayo, alishauri serikali iwekeze kwa kiasi kikubwa katika miundombinu (barabara), nishati, reli, bandari, mawasiliano, elimu na afya.
  “Uwekezaji katika miundombinu umekuwa mdogo na hutegemea fedha za misaada kutoka nje, sasa tunapaswa kutoka huko,” alisema mwenyekiti huyo wa CUF.
  Kuhusu kilimo, alisema ingawa serikali imetoa kaulimbiu ya ‘Kilimo Kwanza’, lakini utekelezaji wake unaonekana kuwa mgumu kutokana na mkulima kutopewa motisha na uhuru wa kuuza mazao katika masoko bila kutozwa kodi za juu
   
 2. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Albert Einstein once said, "you can not solve the problem at the same level when the problem was created." Same people who created the messes are the same people to solve them. I believe they will solve the problem in the same way they created....and that way is to tell people lies all the time.
  The current set up can not come with an answer to the corruption problems we face because they created this problem
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Sasa hapa aliyelipuliwa ni Chenge au serikali
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Serikalini wooote wanalindana.....siku zipite....tusitegemee jipya milele amina
   
 5. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kuna mambo mengi ambayo, Serikali ya JK imeamua kuyafumbia macho tena kwa makusudi ambayo JK mwenyewe anayajua. Suala la akina Hosea, Mwanyika na wengineo kwenye issue ya Richmond, BOT na suala la EPA, Meremeta, Kiwira na mengineyo mengi ni sehemu tu ya mambo machafu ambayo JK na wenzake wachache kwenye Serikali yake wameamua kutoyashughulikia. Kwa suala la Chenge naamini halitakaa lijadiliwe na mwaka 2010 Chenge atarudi Bungeni kama mbunge wa Bariadi na atarudishiwa posti ya uwaziri kama mtu msafi na mwadilifu kwa CCM na rafiki yake JK.

  Watanzania tumefanywa mbumbu ndani ya nchi yetu na viongozi wachache wanaendelea kuneemeka kwa matendo yao ya kifisadi.
   
 6. T

  Tuandamane JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 2, 2008
  Messages: 1,220
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  ajabu na kweli tutawachagua tena hao hao 2010, soo pitty!
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hili la chenge kurudi tena bungeni nalo tuilaumu serikali
   
 8. K

  Kinyikani Member

  #8
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 65
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtanzania anayechaguwa kiongozi wote wanachaguliwa na na nec ya taifa.

  huwezi kuwa fisadi bila ya kuwa ccm wala huwezi kuwa ccm bila yakuwa fisadi
   
Loading...