Lipi lililowashinda CC ya CCM Kipindi cha JK?

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Katika kipindi chetu cha siasa za Tanzania Kutokea Hapa Zapa Fm ndio wachambuzi wa kisiasa walikua wanaongelea hivi

Tangu mwaka 2005-2015 , JK aliingia madarakani akiwa na falsafa ya " Ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya." Hakuishia hapo alitumia pia " Maisha bora kwa kila mtanzania.

Wakati huo, Tanzania ilikuwa inasumbuliwa na tatizo la;

* uchumi tegemezi uliokuwa unachagizwa na Sera za IMF na World bank. Masharti yao yaliifanya Tanzania chini ya Mkapa, kushusha dhamani ya shilingi dhidi ya dola,

* kuanguka kwa huduma za jamii kama maji, umeme , Afya , kilimo, viwanda na uwekezaji. Vijana wengi wakapunguzwa kazi,Elimu ikashuka!

* mikataba ya nje iliyoingiwa ndio iliyozalisha Richmond, Escrow, na ufisadi wa Meremeta, kagoda na kadhalika.

* Maadili ya uongozi yaliendelea kuwa tete wizi, uteuzi wa upendeleo na kutokusanya kodi na kulipa ikawa kawaida.

Hivi kesho ya watanzania ikawa ndoto,uvunjifu wa haki za binadamu, kuondoa utumishi unaozingatia Uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora.

Umaskini uliongezeka. Ccm ikaendelea kuimba wimbo wa ccm ni chama imara chenye dira na kutupilia mbali dira iliyotolewa na time ya Warioba juu ya haja ya katiba mpya!

Uchaguzi wa 2015 kwa mizengwe mikubwa ccm ikamtangaza kupitia tume yake ya Taifa ya uchaguzi bwana John Pombe Joseph Magufuli.

Ni miezi 3 sasa.ccm inadai kurejesha nidhamu ya wafanyakazi na kuimarisha utawala bora.

Ccm haijatuambia kwa mini pamoja na makusanyo ya trioni 1.4 ;

Kwa nini?

* walimu wakiendelea kupewa barua za mishahara mipya bila kubadilisha ?hela za likizo miaka 3 na hakuna nyumba za walimu na miundombinu kama madawati?

* kwa nini bado watu wananunua Dawa?

* kwa mini bado tunaona hakuna utawala bora?

Aidha unapotoa kiasi cha tsh. 399000, ili zitumike mashuleni kwa mgawo huu unamaanisha nini?

30% vifaa vya kujifunzia

30% ukarabati

20% mitihani

10% michezo
10% utawala

Je,kwa mgawanyo huo, ni darasa gani litajengwa?, ni kifaa gani cha mwanafunzi kitanunuliwa?, je , ni mitihani IPI ya wanafunzi 789 ya mwezi, au wiki( upimaji wa kila wiki au mwezi au muhula wa mwanafunzi?)

Aidha ni vifaa gani vya michezo kama mpira zitanunuliwa au jezi za watoto wa kike na kiume?), tumejiandaa kuimarisha michezo kishule ili tuwapate akina Filbert bay au Mbwana Samatha?

Watanzania ndio maana watoto wa wakubwa Hawa mnaowaendekeza watoto wao wanatibiwa nje, wasoma nje ila nyie wapiga ramli za kuwa ccm imebadilika, mkiendelea kusaga lami huku umaskini wa akili, ukipandwa na ccm kwa kupitia radio, magazeti, mitandao ya kijamii na maigizo mbalimbali.

Ccm ni ileile, lazima tuzinduke, chama kisichopenda ushindani wa nguvu ya hoja, ubabe kikategemea ni chama hatari.

IPO siku wajinga HawA wataelewa, ngoja ahadi ya umeme massa 24 na maji masaa 24 tusubiri hadi 2020 barabara za flyover zitakuwepo.
 
Haki ya Demokrasia imebakwa kwa nguvu zote na tume ya uchaguzi na wanafikiri ya kwamba Watanzania hawajatambua hili la ubakaji wa Demokrasia,wanawaaminishia Watanzania kelele ya hapa na pale bila ya kuwepo utendaji wowote wa haki

Chondechonde na nawaambia ya kwamba Watanzania siyo kwamba hawaoni kinachoendelea hakika wanaona ila tushukuru uvumilivu Mungu akiyetupatia na tuendelee nayo na mwisho wa siku hata huu uvumilivu utatoweka na ccm itang'ooka madarakani na Watanzania watafurahia matunda ya Nchi yao!
 
Ninachokiona kwa sasa serekali ya ccm inawaongezea hasira Watanzania kwa sababu ni usani wa kiwango kilicho pitiliza kwa kinacho endelea mf. Muhimbili kila leo ni hahadi hewa zinatolewa alafu kwani hawahoni JK hakufanya lolote?
 
Tatizo la CCM ni unafiki na uoga,hawa hawa wanaompamba JPM ndiyo hawa hawa waliokuwa wanatoa povu kumtetea JK pindi wapinzani walipogusa maeneo haya ambayo Rais Magufuli anayatumbua sasa.CCM ni janga.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Tatizo la CCM ni unafiki na uoga,hawa hawa wanaompamba JPM ndiyo hawa hawa waliokuwa wanatoa povu kumtetea JK pindi wapinzani walipogusa maeneo haya ambayo Rais Magufuli anayatumbua sasa.CCM ni janga.
Ndio maana wanasiasa wanasema kilichokufa ccm siyo mtu ni mfumo ambao kwanzia baba mpaka mjuku ni jibu hakuna msafi na ccm ni ileile
 
Hivi Kigwangala yupo wapi? Au muhimbili ipo chini ya wizara ya ikulu chini ya waziri Magufuli?
 
Toka lini CHICHIEM ikaleta maendeleao, hilo haliwezekani hata kwa tunguli za babu. Kinachotakiwa ni kuswept away this government yote ianze na moja (chama kingine kinatikiwa)
 
Ccm wanataka kutoa watu wasijadili kiendeleacho Zanzibar
 
heri ya serikali ya ccm mara mia moja kuliko kuongozwa na chadema ambayo wanashindwa hata kuweka taratibu za ugawaji wa viti maalumu, pia hawaamini wabunge wao wanasema sio makini waliowekwa kwenye kamati za pac, wameshindwa kuchagua katibu mkuu na kama wameuza chama wangepewa nchi tayari wangekwisha gawana
 
Sidhani unachokiongea unakijua hao vita maalumu uwaoni? JITAMBUE
 
Toka lini CHICHIEM ikaleta maendeleao, hilo haliwezekani hata kwa tunguli za babu. Kinachotakiwa ni kuswept away this government yote ianze na moja (chama kingine kinatikiwa)
Kama ujaona Chadema kimefanya nini basi wewe utaona hata ufalme wa Mungu
 
Katika kipindi chetu cha siasa za Tanzania Kutokea Hapa Zapa Fm ndio wachambuzi wa kisiasa walikua wanaongelea hivi

Tangu mwaka 2005-2015 , JK aliingia madarakani akiwa na falsafa ya " Ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya." Hakuishia hapo alitumia pia " Maisha bora kwa kila mtanzania.

Wakati huo, Tanzania ilikuwa inasumbuliwa na tatizo la;

* uchumi tegemezi uliokuwa unachagizwa na Sera za IMF na World bank. Masharti yao yaliifanya Tanzania chini ya Mkapa, kushusha dhamani ya shilingi dhidi ya dola,

* kuanguka kwa huduma za jamii kama maji, umeme , Afya , kilimo, viwanda na uwekezaji. Vijana wengi wakapunguzwa kazi,Elimu ikashuka!

* mikataba ya nje iliyoingiwa ndio iliyozalisha Richmond, Escrow, na ufisadi wa Meremeta, kagoda na kadhalika.

* Maadili ya uongozi yaliendelea kuwa tete wizi, uteuzi wa upendeleo na kutokusanya kodi na kulipa ikawa kawaida.

Hivi kesho ya watanzania ikawa ndoto,uvunjifu wa haki za binadamu, kuondoa utumishi unaozingatia Uhuru wa vyombo vya habari na utawala bora.

Umaskini uliongezeka. Ccm ikaendelea kuimba wimbo wa ccm ni chama imara chenye dira na kutupilia mbali dira iliyotolewa na time ya Warioba juu ya haja ya katiba mpya!

Uchaguzi wa 2015 kwa mizengwe mikubwa ccm ikamtangaza kupitia tume yake ya Taifa ya uchaguzi bwana John Pombe Joseph Magufuli.

Ni miezi 3 sasa.ccm inadai kurejesha nidhamu ya wafanyakazi na kuimarisha utawala bora.

Ccm haijatuambia kwa mini pamoja na makusanyo ya trioni 1.4 ;

Kwa nini?

* walimu wakiendelea kupewa barua za mishahara mipya bila kubadilisha ?hela za likizo miaka 3 na hakuna nyumba za walimu na miundombinu kama madawati?

* kwa nini bado watu wananunua Dawa?

* kwa mini bado tunaona hakuna utawala bora?

Aidha unapotoa kiasi cha tsh. 399000, ili zitumike mashuleni kwa mgawo huu unamaanisha nini?

30% vifaa vya kujifunzia

30% ukarabati

20% mitihani

10% michezo
10% utawala

Je,kwa mgawanyo huo, ni darasa gani litajengwa?, ni kifaa gani cha mwanafunzi kitanunuliwa?, je , ni mitihani IPI ya wanafunzi 789 ya mwezi, au wiki( upimaji wa kila wiki au mwezi au muhula wa mwanafunzi?)

Aidha ni vifaa gani vya michezo kama mpira zitanunuliwa au jezi za watoto wa kike na kiume?), tumejiandaa kuimarisha michezo kishule ili tuwapate akina Filbert bay au Mbwana Samatha?

Watanzania ndio maana watoto wa wakubwa Hawa mnaowaendekeza watoto wao wanatibiwa nje, wasoma nje ila nyie wapiga ramli za kuwa ccm imebadilika, mkiendelea kusaga lami huku umaskini wa akili, ukipandwa na ccm kwa kupitia radio, magazeti, mitandao ya kijamii na maigizo mbalimbali.

Ccm ni ileile, lazima tuzinduke, chama kisichopenda ushindani wa nguvu ya hoja, ubabe kikategemea ni chama hatari.

IPO siku wajinga HawA wataelewa, ngoja ahadi ya umeme massa 24 na maji masaa 24 tusubiri hadi 2020 barabara za flyover zitakuwepo.

Kila siku huwa nasema jpm akitaka kufanikiwa amtemeshe mzaramo mkwanja alioupiga na wenzake
 
Chadema walisema elimu bure mpaka chuo kikuu sasa tatizo ni nini hapo?
 
Tatizo la CCM ni unafiki na uoga,hawa hawa wanaompamba JPM ndiyo hawa hawa waliokuwa wanatoa povu kumtetea JK pindi wapinzani walipogusa maeneo haya ambayo Rais Magufuli anayatumbua sasa.CCM ni janga.

Hao hao waliokuwa wanatuambia Ufisadi wake wa Richmond na kusema wanao ushahidi Mzito mpaka wakatengeneza List of shame ndio hao walikuja tena Kutuambia tumpe Ukuu wa Nchi amiliki mpaka Hazina kuu ya Nchi! Wakaifuta ile List of shame kwny tovuti ya chama
Kama huu sio unafiki basi hakuna Mnafiki Tanzania
 
Back
Top Bottom