LIP STICK ZINGINE hapana aisee

Makubwa mshinga hayo makitu waachie wadada sisi tunapaka lakini nyie wakaka mnayalamba yote so huwezi kuepuka lipstick na utaila sana.
 
jamani inatosha....kashasikia
 
Jamani nimeondoka nawah kununua lipshine kabla duka halijafunga nisikose ya kupaka kesho coz imekwisha........nisindikize basi mume wangu mpezi.............twende mke wangu na hela hii hapa...........nimeshachukua hela mume wangu..............hiyo haitoshi mke wangu ongeza hii au unataka ukanunue ile ya kuganda kwenye glasi na kwenye nguo?......hapana ........basi twende...........
 
Tatizo huyo dem ako anapaka lipstick za bei rahisi that's y zinabakisha alama kwa glass au popote bt akipata za bei wala haziachii alama kivilee
nimerudi.
HIVI NANI MWENYE AKILI
1.anaetumia ukubwa wa bei kuthitisha ubora? au
2.anaetumia mamlaka sahihi kama tbs?
usirudie tena kutamka bei kama kigezo cha ubora,wanawake wengi ni vichwa ngumu,kuna bidhaa ngapi za bei mbaya zimepigwa marufuku na bado munanunua kwa siri?
 
Makubwa mshinga hayo makitu waachie wadada sisi tunapaka lakini nyie wakaka mnayalamba yote so huwezi kuepuka lipstick na utaila sana.

Mie????Nawaachia wale wanaoweza kumeza hizo rangi.
 
JF haitabiriki aisee....

Sikutegemea kama jamaa atakosa wa kumsapoti

(But it is too early to conclude)

Labda watakuja wenyewe

Tatizo akianza mmoja kuiponda mada mara nyingi wengi hufuata upepo unapovuma... teh! Jamaa katolewa kitoweo leo!
 
...loh pole mkuu wamekuvuruga kabsaaa..!
 
Watu mna kumbu kumbu hivi huyu jamaa ndiye alisema hapendi wanawake wanao jichora ina?
Huyu jamaa hapendi gharama nyie hamjajua tu!!!

Lipstick nayo ina gharama???Na nguo za wanawake tusemaje?Na kiwanja tusemaje?Na shamba tusemaje?Na gari tusemajdm?Na nyumba tusemaje?Ushawahi kusikia sitaki mwanamke atakae gari kama naogopa gharama?Ushawahi kusikia sitaki mwanamke anaetaka kujengewa nyumba,kununuliwa kiwanja,kununuliwa nguo ama shamba?????
 
...loh pole mkuu wamekuvuruga kabsaaa..!

Wengi wamekwapuliwa na mada,ukiona wananishambulia ujue wamenaswa,wengi wanatumia na hapa wanajitetea tu,wakikua wataacha,mama na bibi zetu hata hawayajui haya madude.
 
jamani inatosha....kashasikia

Wenzi wengi watumiaji n wapo hapa kutoa uteteziwao.
Akili za watumiaji wa vipodozi haziambiliki,kuna vipodozi hatari vimepigwa marufuku lakini wenzio wananunua pale kariakoo kama biashara ya madawa ya kulevya.
 
hapo ;linakuja swali lileeeeeee 2lojadili mwanamke mrembo kama huwez kuaford gharama sepaaaaaaaaa
wanawake kwa kupenda sifa hata kama ni za kijinga,yaani lipstick ama lipshine inakufanya kuwa wa gharama?Hiyo gharama ya kupaka lipshine kwa mwaka inafikia hata gharama ya kusomesha mtoto mmoja shule ya kayumba kwa mwaka?Lipshine kwa mwezi inafikia gharama ya mafuta ya gari?Hata sifa za gharama ya nyanya kweli zinawafanya wanawake wajiite ni wa gharama!!Hopeless,hatupendi hiyo mirangi ni mibaya,ati mwafikiri ni gharama.
 

hao ni washamba...anapaka lipstick nyingi anajiona amekuwa mzuri kumbe ndiyo anazidi kuwa kibungo!!!
 
 
Najua hawakoti ila napinga hoja ya kitoto kuwa mwanamke ni gharama alafu gharama yenyewe lipstick,ebu watuwekee hapa bei ya hizo ya lipstick uone zilivyo rahisi.siogopi bei mana gharama yake ni ndogo mno.
Kumbe wewe unacheza ngoma ya kupaka wanja au?Sikuhitaji pongezi nataka wajue na waache hiyo mirangi yao yenye hatari.Hata wabwia unga wanapenda ila tunawakataza na si kila upendacho unaihitaji kuachwa.Nani kakwambia kila apakaye mume anafurahia?Acha uongo wa waziwazi mbona kuna mtu kasema alitapika(scatter) ama na huyo anapenda?
 
hao ni washamba...anapaka lipstick nyingi anajiona amekuwa mzuri kumbe ndiyo anazidi kuwa kibungo!!!

Tatizo wanawake hata sifa za kutaniwa tu zinawapumbaza,mwanamke ukimwambia "umependeza"yaani unakosha roho yake na anajiamini zaidi na kuongeza kujipaka akijua anawashika mtaani,ni wangapi wanawatania wanawake kuwa wako mwake lakini wakiondoka wanawashangaa!Mwanamke ukimwambia kawa mbaya haki ya nani ataifuta hiyo mirangi yake.
Tatazo ni wachache wanajitoa mhanga kuwaeleza ukweli.
 
Hata gongo ina wateja wakd lakini watu wanashauriwa wasinywe,haya marangi yenu ni hatari kwa afya yenu.

Lipstick sio mbaya mkuu!Ila sometimes by technical error tu huwa hawa madada wanazidisha bana!

Juzi pale Mliman City nilimuona Lulu kajipaka lipstic ya njano lip yake za juu na nyekundu lip ya chini ahahaha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…