Link angalia Young Africans na Al Ahly live

Link angalia Young Africans na Al Ahly live

Mkuu chanel ipi hawa jamaa naona wanaongea tu tena kiarabu hata kujua wanachosema shida wakati game inakaribia

dakika 30?..

walianza kuonyesha,nashangaa wamekata,wanaongea tu,wahuni sana hawa
 
Azam TV
Tumepokea maswali na simu nyingi
sana zikiuliza kama Azam TV
itaonesha mechi kati ya Yanga na Al
Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA...
ukweli ni kwamba tulipokea maombi
toka kwa agent aliyenunua pambano
kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye
aliomba Azam TV impe gharama za
kuzalisha ili kuweza kupeleka feed
yenye ubora wa kimataifa North Africa
& Middle East na ikiwezekana
kuonesha nchini Tanzania. Katika
vikao vyote na Agent Azam TV iliweka
wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na
hata kama ikibidi kuonesha delayed
sawa kwa kuwa Yanga walionesha
wazi kuzuia Live Coverage nchinikwa
kuhofia mapato kupungua.
Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam
TV na kuamua kutoa pesa waliyolipwa
kukilipa kituo kimoja nchini ambacho
ndicho kilichopewa kandarasi kwa
malipo licha ya kutokidhi vigezo vya
watu wa Egypt ambao walitaka angala
8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10
Camera OB with HD Feed
Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu
wateja wetu kuwa Azam TV ilikuwa
tayari kuwapa Yanga na Agent
ushirikiano wote ili pesa yote
waliyopewa na Watu wa Misri iingie
klabuni lakini wao wameamua kuitumia
kulipia production iliyo sub-standard ili
mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
Pamoja na haya yote Azam TV
inaitakia kila la kheri klabu ya Yanga
kwenye mchezo wake wa leo, na
inaamini matatizo hayapo kati ya Azam
na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja
mwenye nguvu ndani ya Yanga
 
Azam TV
Tumepokea maswali na simu nyingi
sana zikiuliza kama Azam TV
itaonesha mechi kati ya Yanga na Al
Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA...
ukweli ni kwamba tulipokea maombi
toka kwa agent aliyenunua pambano
kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye
aliomba Azam TV impe gharama za
kuzalisha ili kuweza kupeleka feed
yenye ubora wa kimataifa North Africa
& Middle East na ikiwezekana
kuonesha nchini Tanzania. Katika
vikao vyote na Agent Azam TV iliweka
wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na
hata kama ikibidi kuonesha delayed
sawa kwa kuwa Yanga walionesha
wazi kuzuia Live Coverage nchinikwa
kuhofia mapato kupungua.
Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam
TV na kuamua kutoa pesa waliyolipwa
kukilipa kituo kimoja nchini ambacho
ndicho kilichopewa kandarasi kwa
malipo licha ya kutokidhi vigezo vya
watu wa Egypt ambao walitaka angala
8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10
Camera OB with HD Feed
Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu
wateja wetu kuwa Azam TV ilikuwa
tayari kuwapa Yanga na Agent
ushirikiano wote ili pesa yote
waliyopewa na Watu wa Misri iingie
klabuni lakini wao wameamua kuitumia
kulipia production iliyo sub-standard ili
mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
Pamoja na haya yote Azam TV
inaitakia kila la kheri klabu ya Yanga
kwenye mchezo wake wa leo, na
inaamini matatizo hayapo kati ya Azam
na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja
mwenye nguvu ndani ya Yanga

Haya ndiyo matatizo ya hizi timu zetu za Tanzania,yaani dunia nzima tunaangalia mechi hizi kila kona ya dunia na hata sasa tunaangalia CAF kwa timu ambazo si za Tanzania,lakini inapofika kwa yanga na simba huwa sielewi ni kwanini wanategemea sana mapato ya getini na si vyanzo vingine vya mapato? je hao wa misri si walikuwa tayari kuwalipa kwanini walikataa?
angalia hii http://www.alahlytv.net/LiveBroadCast.aspx
nao wameshindwa kutuonyesha mpambano huu,nadhani ni kwaajili ya ukilitimba usio na mbele wala nyuma.
 
Ndio maana soka letu halitakaa liendelee kamwe! FITNA TU..wako busy kutafuta pesa za kumalizia magorofa yao..! Wanaudhi..
 
Tatizo pesa zinazoingia kwa kununua haki ya kuonesha live zinakuwa documented hivyo jinsi ya kuzichota inasumbua kidogo, bora waboreshe mapato ya mlangoni ili makomandoo wazichote kiurahisi.
 
Kwanini hata goli la kulazimisha haliingii yanga na waarabu kunani?
 
[h=6]Young Africans Sports Club
[/h]Naona Kazi imebakia kuisema Young Africans vibaya, SGM waliingia mkataba na Yanga, Yanga nao walichagua kituo cha kufanya nacho kazi, sasa tunashangazwa na Taarifa zinazoenezwa kwamba tumekataa kuwapa wao nafasi ya kuonyesha mpira leo.

Kama wana uhakika na wanachokisema waonyeshe barua ya hao waliowaomba kutumia kituo chao kuonyesha mchezo wa leo.

Walianza na kusema wameombwa Uwanja wa mazoezi, Balozi wa Misri akakanusha na kuleta barua ya maombi ya uwanja kwetu tukashirikiana nao kupata IST.

Hivyo ni bora tukawa tunatoa taarifa zenye uhakika wa maandishi kama ni kweli kudhibitisha kauli hizo, vinginevyo ni kuendelea kujipunguzia thamani kwa taarifa za Uongo.

Tukutane Uwanja wa Taifa tukamnyoe Al Ahly
 
Mmezoea kutajirika kupitia migogongo ya wanyonge. Kwa Yanga mmekwama.
 
Back
Top Bottom