Lini Utanipa

Lini Utanipa

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,080
Reaction score
1,452
NI LINI UTANIPEA ?
Imenijaa ashiki, sikia mpenzi wangu
Naomba hili afiki, usinifanyie pungu
Sinipe ahadi feki , umeshaiva mkungu
Sema nisikie Switi, siku gani utanipa

Nimeiweka nadhiri, viugho kukupatia
Napa itakuwa siri, kwa Mola tutatubia
Nionyeshe umahiri, sifa ntazikumwagia
Nataka yako ahadi ati lini utanipa


Sijui huniamini, nipee sitakimbia
Mie sio mhaini, ndoa itafuatia
Ndiwe ulo kwa maini, penzilo mekumbatia
Hali zote sikuwachi, ni lini utanipea

Jawabu nalitaraji, nitapokea azizi
Kujua langu hitaji, fuadini nimaizi
Uje unipe masaji, miguu itoke ganzi
Kunjua chako kifua, ni lini utanipea

Abuuabdillah[emoji1621]
0718569091
0744883353
 
Oops.,!

Subiri baada ya ndoa, ndiyo utapewa.
Sasa zamu ya Goa, mpk utapojielewa
Atazidi kukubania, bila hata kufosiwa.
Ukiona demu hakupei, ujue hakupendi.
 
Doctor ninakuusia, zinaa si kitu bora.
Dini zimetuzuia, zikataja na khasara.
Zinaa kukumbatia, vingi vitakudorora.
Tafadhali anza ndoa, mengine yatafatia.

Naimani unajua, kwa faida na khasara.
Ndoa ikitangulia, kwa mola ni jambo bora.
Ukizini tukajua, ni mawe au bakora.
Tafadhali anza ndoa, mengine yatafatia.

Shemeji namuambia, ajifiche mpaka sura.
Akatae kukupea, mola ampe stara.
Aisubirie ndoa, asiogope mikwara.
Tafadhali anza ndoa, mengne yatafatia.
 
Imeandikwa vitabuni, ndoani ndipo patamu
Ikakolezwa usizini, usiende jehanamu
Ukikaidi motoni, ndipo kwako hatamu
Zinaa kitu gani, badilisha zako njia.
 
Nimeiweka nadhiri, viugho kukupatia
Napa itakuwa siri, kwa Mola tutatubia
Nionyeshe umahiri, sifa ntazikumwagia
Na mwendo wake kama Ngiri,
Akitikisa matako Bandia.
Tunaoa Mwisho wa Safari,
Tukichoka na kujifia.
Wanawake na roho ya Mbigiri,
Ukimla anakuita Kibamia.
#wanawake wa Leo wote ni Bembela tu.
 
Na mwendo wake kama Ngiri,
Akitikisa matako Bandia.
Tunaoa Mwisho wa Safari,
Tukichoka na kujifia.
Wanawake na roho ya Mbigiri,
Ukimla anakuita Kibamia.
#wanawake wa Leo wote ni Bembela tu.
😂😂😂Aisee
 
Back
Top Bottom