Lini tutazikataa Siasa Za Soda na Mkate?

duba

New Member
Jul 14, 2011
1
0
Wadanganyika tumeyaona yaliyotokea Igunga wazee wetu, wamekuwa mstari wa mbele kupinga kujiuzuru kwa Mh Mbunge wao, wananchi wetu wamekuwa wakitumiwa na wanasiasa kama madaraja huku, wakiachwa bila kupatiwa ufumbuzi wa kweli wa maisha yao, hii inatokana na jamii kubwa hasa wananchi wengi waishio vijijini kuwa kwenye dimbwi kubwa la umasikini.

Wanasiasa wanapitia kwenye shida zao ili kujineemesha, hizi tunaziita siasa za soda na Mkate, soda ina utamu radha nzuri sana ikinywea iliwa baridi na utility yake hutegemea nguvu ya mnywaji na mkate huyeyuka pindi unapotumbukizwa kinywani, na muda si mrefu mraji huwa anajisikia ameshiba kutokana na gesi ya soda na amira iliyomo kwenye mkate.

Mtuamiaji hujihisi kuwa njaa imeisha kwa muda, lakini baada ya saa moja njaa hurudi pale pale, hizi ndio siasa za soda na mkate, ambazo wanasiasa wetu wanazitumia. Wanasiasa wamekuwa wakiwatumia wazee wetu kwa kuwapa zawadi za pipi, kwa maana kwamba kuwalipia karo za watoto wao na kuwanunulia baikeli huku matatizo yao makubwa hayapatiwi ufumbuzi wa kudumu kama vile barabara, zahanati zikiachwa bila kupewa msukumo wa kutosha.
 
Back
Top Bottom