Lini Tanzania itakuwa nchi moja?

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Naogopa kuiona nchi yangu ikisambaratika!
Wanasiasa wanavunja umoja na mshikamano wetu kama taifa!
Nchi hii sasa si moja maana bado tunaishi kama tupo kwenye kampeni!
Nani anaweza kutuunganisha tena?
Nini kinaweza kutufanya turejee umoja wetu ambao ndio sifa kuu ya UTaznania wetu!

Sehemu kuu ya Mtafaruku inajengwa na viongozi wa serikali ktk ngazi zote, pia baadhi ya idara nyeti za umma nazo zinachochea kusambaratika kwa umoja wa kitaifa!

Ukirejea kauli kadhaa za baadhi ya viongozi hasa mkuu ni kama hizi.....
"wapinzani wetu wantaka tufanye mabaya......"
"wapinzani wanatuombea tushindwe..."
mifano ya aina hizi za kauli havipaswi kusikika toka ktk kinywa cha kiongozi wa serikali!
kimantiki serikali haina mpinzani, maana hii haina itikadi!
viongozi wa serikali wanapokuwa wanahudumia chama chao cha ccm wanaruhusiwa kutoa kauli za aina hii, lkn wakiwa wanapeperusha bendera yenye rangi nne, wanapaswa kujua kuwa hiyo itakuwa ni matumizi mabaya ya ofisi!
wapinzani wa ccm pia wanapaswa kutofautisha kati ya serikali ikiwa inatekeleza majukumu yake, kwa manufaa ya umma na chama cha mapinduzi kama taasisi!
Kukweli toka July 2015 Tanzania haijawahi kuwa moja, na kwa style hii ya sasa gap linazidi kuongezeka!
Viongozi fanyieni kazi jambo hili mapema kabla jua halijazama!

inanifanya nikumbuke (just titles sio contents za kina Chinua Achebe na wenzake)
The river between....
Things fall apart...
No longer at Easy....
kila moja ingeweza kututengenezea movie/story ya Tanzania ya leo
 
mwenyewe nashangaa kusema upinzani.. upinzani..upinzani.. upinzani wenyewe hawaongei ila kuna watu mitandaoni ambao pengine hata hawapo hivyo vyama vya upinzani, ni watu walikuwepo tangu kipindi cha Kikwete, hata kipindi cha Mkapa ila sema kulikuwa hakuna mitandao
Rais afanye kazi matokeo yataonekana ukiwa kiongozi lazima utapingwa na kubezwa tu...sasa ukiwa unajibizana na comments za mtandaoni kila kwenye mikutano yako labda hujui maana ya uongozi na price ya uongozi
 
Angekuwa anaijua maana ya uongozi asingejivunia kusimama na kuanza kuwasimanga watu anaowaongoza, asingekuwa na kauli za kebehi. Ipo siku Mungu atakaa upande wa watesi wake.
 
Angekuwa anaijua maana ya uongozi asingejivunia kusimama na kuanza kuwasimanga watu anaowaongoza, asingekuwa na kauli za kebehi. Ipo siku Mungu atakaa upande wa watesi wake.
Sio lazima Mungu amlipizie, lakini hata kuwa na huitaji wa baadhi ya watu wa team B!
inauma unapofanya kazi na ccm tu!
hata kiongozi wa kambi ya upinzani hana nguvu yeyote, wala si wa msaada Bungeni na nje ya Bunge!
wananchi tunakaripiwa na kutishwa kila leo!
hofu imetanda ktk nafsi za watu, hakuna anayeshauri, anayekosoa wala anayeuliza!
 
Back
Top Bottom