Lingang: Mji uliotengenezwa kutoka sehemu ya bahari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Takriban miaka saba iliyopita hapa nchini kulizinduliwa mradi mkubwa wa kuchukua sehemu ya bahari ya Hindi na kuigeuza kuwa nchi kavu kuanzia eneo la daraja la Selander hadi Ocean Road, ambapo kungejengwa makazi ya watu, hoteli, maeneo ya michezo, bandari, maduka 200 na huduma za kijamii.

Katika mradi huo ujulikanao Salama Water Front ulikuwa na lengo la kuibadili Dar es Salaam iwe kama miji mingine ambayo imechukua sehemu ya bahari na kuijaza udongo kisha kujengwa majengo kama ilivyo kwa sehemu kubwa ya Mji wa Helsinki huko Finland na nchi nyingine kama jiji la Cape Town, Afrika Kusini, Washington, Marekani, Uholanzi na Japan.

Bandari ya Zeebrugge ya Ubelgiji pia ni mfano wa eneo lililokuwa bahari na kugeuzwa nchi kavu. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kansai wa Osaka, Japan na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong ni mifano ya sehemu mojawapo ambazo nchi husika zililazimika kutumia teknolojia hiyo kuvitengeneza viwanja hivyo.

Katika uwanja wa Kansai, inasadikiwa kuwa kutokana na majengo kujaa waliona ni vema kuingia baharini zaidi ya kilomita 10 na kujaza udongo eneo la bahari na kujenga uwanja huo.

Kwa upande wa mradi wa Salama Water Front nakumbuka mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mradi huo uliojulikana kama Ufukweni Water Front alikuwa Waziri Mkuu wa wakati huo, Frederick Sumaye na uzinduzi ulifanyika katika ukumbi wa Msimbazi Centre Dar es Salaam, ambapo ahadi nyingi nzuri zilitolewa na nikiwa kama mwandishi baada ya hapo nikawa nafuatilia maendeleo yake lakini ilikuwa maneno matupu na ‘chenga’ nyingi na hadi leo hakuna kilichofanyika.

Mbali na hilo pia kwenye miaka ya 1970 kulianzishwa Mamlaka ya Ustawishaji wa Makao Makuu Dodoma (CDA), lengo likiwa kuhamishia makao makuu ya nchi kuwa mkoani humo sambamba na kuuendeleza mji huo ambapo mipango mingi mizuri ilipangwa lakini utekelezaji hafifu.

Nimeamua kukumbushia miradi hiyo kama mfano kuona jinsi miradi yetu ya maendeleo inavyoishia kwenye makaratasi au utekelezaji kuwa hafifu huku watu wakiajiriwa na kula mishahara ya bure tofauti na China ambayo imekuwa na miradi ya aina hiyo mingi na inatekeleza katika muda iliyojiwekea.

Mradi mmoja wa mafanikio ambao unafanana na huu wa Dar es Salaam nimeushuhudia katika jiji la Shanghai ambapo ndani yake kumeanzisha mji wa kisasa unaoitwa Lingang ambapo kuna sehemu ya bahari imegeuzwa kuwa nchi kavu na kujengwa majengo kadhaa.

Ni mji unaovutia sana, una bandari ya kisasa; viwanda vikubwa na vidogo; makazi ya watu; maeneo ya biashara; maeneo ya huduma za kijamii; hoteli za kimataifa, ofisi mbalimbali; miundombinu ya kisasa kama barabara, reli na madaraja na kubwa zaidi wameweza kutengeneza Ziwa kubwa liitwalo Dishui ambalo tulibahatika kulitembelea kwa boti.

Uamuzi huu wa kuutengeneza mji wa Lingang ulifikiwa na Serikali ya Manispaa ya Shanghai na ujenzi wake ukaanza Novemba mwaka 2003 ikiwa katika mpango wa 2020 ambapo lengo ni kuinua uwezo wa viwanda, kuongeza maendeleo na kuongeza ushindani wa kimataifa.

Licha ya muda uliokusudiwa ni hadi mwaka 2020, lakini hadi mwaka huu ikiwa miaka sita imepita tayari asilimia 90 ya mradi umeshakamilika na sehemu kubwa itakamilika mwaka huu isipokuwa baadhi ya maeneo kama ujenzi wa hoteli zenye hadhi ya nyota tano.

Eneo hili la Lingang kulikuwa na bandari yenye kina kirefu ya Yangshan na Bandari ya kimataifa ya Pudong huku watu wa kawaida wakiwemo wavuvi walikuwa wakiishi eneo hilo, lakini serikali ikaamua kuliendeleza zaidi kwa kuchukua sehemu ya bahari na kuigeuza kuwa nchi kavu na pia kuchimba ziwa lenye kina cha urefu wa meta 5.6 ambapo sasa muonekano unaonyesha katikati ya eneo hilo kuna ziwa na pembeni kumezungukwa na bahari.

Mji huo wenye umbo la duara upo katika ukingo wa bahari ya Mashariki ya China na ghuba ya Hangzhou kusini mashariki ya mji wa Shanghai. Eneo lote la mji huo lina ukubwa wa kilometa za mraba 311.6 ambapo kilometa za mraba 80 ya hizo zimechukuliwa kutoka baharini.

Mji huo umepangwa kuwa na watu 800,000 na umegawanyika katika maeneo ya makazi, viwanda vikubwa, utawala, viwanda vya kati, sehemu ya teknolojia ya bahari ambako pia kumeshajengwa Chuo Kikuu kiitwacho Shanghai Maritime na wanafunzi wameshaanza masomo na makumbusho ya masuala ya usafiri wa baharini. Pia sehemu ndogo za wilaya Nicheng, Shuyuan, Wanxiang na Luchaogang.

Katika wilaya ya Nicheng ina eneo lenye kilometa za mraba 7.12 ambapo wakazi watakaoishi eneo hilo ni 100,000 na lengo la eneo hilo ni kwa ajili ya makazi na huduma za kibiashara ambapo kutakuwa na viwanda vikubwa.

Wilaya ya Luchaogang yenye ukubwa wa kilometa za mraba 3.32 limepangwa kuishi watu 30,000 na eneo hilo linakabiliana na bandari yenye kina kirefu ya Yangshan. Limepangwa kuwa na msitu pamoja na majengo ya kiutawala ya manispaa.

Kwa upande wa wilaya ya Wanxiang ambayo nayo imeingia sehemu ya mji wa Lingang kumetengwa kilometa za mraba nane kwa ajili ya viwanda huku wilaya ya Shuyuan imepangwa kuishi wakazi 80,000 katika eneo lenye kilometa za mtaba 10.9. Hapo kutajengwa bandari, eneo la kilimo cha kisasa, viwanja vya gufu .

Katika mji huo wa kisasa kumeshaanza kujengwa viwanda kadhaa vikiwemo vya kutengeneza magari, vifaa vya bandarini kama mashine mbalimbali, vipuri vya magari, mashine za mitambo ya umeme, vifaa vya reli nk.

Kutokana na kuchimbwa ziwa hilo la Dishui, kumepatikana visiwa vitatu ambavyo kila kimoja kutajengwa hoteli kubwa za kimataifa zenye hadhi ya nyota tano kwa ajili ya kuvutia watalii kutembelea eneo hilo. Tayari kisiwa kimojawapo kilicho Kusini katika eneo hilo kimeshapangwa kujengwa hoteli iitwayo Dishuihu Holiday Inn.

Katika eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 74 kumejengwa majengo marefu ya makazi na kampuni ya Ujerumani iitwayo GMP ambapo wakazi 450,000 watapata makazi katika eneo hilo baada ya kuuziwa nyumba hizo na nyingine kupangishwa.

Katika maeneo hayo ya makazi kumetengenezwa maziwa madogo madogo yanayopendezesha mandhari ya eneo hilo. Kiujumla kwa mgeni anayefika eneo hilo atabaini utaalamu, ubunifu na umakini wa serikali katika kuhakikisha inaendeleza miji yake katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia. Maendeleo ya aina hiyo ni changamoto kwa Tanzania, ambayo iliwahi kuwa na mradi wa aina hiyo ambao hadi sasa haueleweki kama utatekelezwa au umekufa.

http://www.habarileo.co.tz/makala/?n=3372
 
Good story mkuu.
 
Back
Top Bottom