LINDI: TANESCO yakwama kufanya shughuli zake sababu ya madeni

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Lindi, linakwama kufanya shughuli zake kwa ufanisi kutokana na kuzidai Taasisi za serikali pamoja na watu binafsi zaidi ya shilingi Milioni Miasita.

Meneja wa TANESCO, mkoani Lindi, Johnson Mwigune, amesema taasisi za serikali zinadaiwa zaidi ya shilingi milioni mia tano, huku watu binafsi wakiwa wanadaiwa zaidi ya shilingi milioni sabini.

Amesema deni hilo ni la mwisho wa mwezi huu, huku akisisitiza ili shirika liweze kujiendesha na kufanya huduma za kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika maeneo yenye maitaji linakwama kutokana na fedha nyingi kuwa mikononi mwa taasisi za serikali.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ameomba taasisi za serikali na watu binafsi, kulipa fedha hizo kwa wakati ili shirika hilo liweze kujiendesha.


Chanzo: ITV
 
RC 'anaziomba' taasisi za Serikali zilipe? Anazibembeleza ili iweje? Na hao Tanesco waache kulalamika.WAKATE umeme kwenye hizo taasisi zinazembea kulipa.Muda wa kubembelezana ulishapita.
 
Nawapongeza Tanesco Ruangwa wanajitaidi sana pongezi kwa uongozi Wa Ruangwa safi sana,ila waongezeeni magari na wafanyakazi jamani Makao Makuu Tanesco plzzzz
 
Back
Top Bottom