KidNinja
Member
- May 26, 2017
- 27
- 15
Wakati Fulani nikiwa katika mafunzo ya Kijeshi katika chuo cha Mafunzo ya Kijeshi katika Mkoa mmoja hapa Tanzania tulikua tukikusanyika wakati wa jioni kujifunza neno la Mungu pamoja na kutiana Moyo ili tuzidi kua wavumilivu wa kiroho na kimwili.
Nilikua na redio yangu ndogo ambayo Nlikua naweka memory card ambayo nilikua nimejaza mafundisho ya Roho na Unabii. Wanafunzi wenzangu walikua wakisikia mahubiri haya walikua wakinisihi tujifunze zaidi kuelewa maana ya Unabii.
Hakika nilikuwa najiona mwenye furaha kwa sababu ya kueneza injili katika maeneo magumu kama pale tulipokua.
Changamoto kubwa tuliyokutana nayo ilikuwa ni kuzuiwa kufanya ibada siku ya Sabato pmj na kukutana kila siku jioni. mkuu wa mafunzo alitufata akatuonya huku tukiitwa watu wenye machafuko ya kidini. Wachache walisimama na kukubali kuendelea kueneza neno. Tulizidi kukutana chini ya miti tukilisifu neno la Mungu.
Wakati mwingine tulikua tukienda kwenye makanisa ya kipentekosti tukilihubiri neno kupitia nyimbo.
Namshukuru Mungu tulifanikiwa kumaliza mafunzo Salama..... Asante sana Mchungaji Mmbaga kwa mafundisho yako. Amina