Lijue basi la mwendo wa haraka

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,809
34,193
LIJUE BASI LA MWENDO HARAKA.jpg

MRADI wa mabasi yatakayo kwenda mwendo wa haraka katika barabara teule mpya jijini Dar es Salaam unaweza kuwa na ufunguo wenye sulushisho dhidi ya foleni na misongamano ya magari jijini humu.
Matarajio ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni kwamba kuzinduliwa kwa mradi huu kutakuwa ndio mwisho wa tatizo sugu la foleni katika barabara zake nyembamba ambazo nyingi mtindo wake ulijengwa na Wakoloni zaidi ya miaka 100 iliyopita.
Pamoja na kuwahi kuwepo aina hii ya mabasi katika miaka ya 1980, sasa mabasi haya yamerudi tena katika ubora wa kipekee na tofauti hasa katika suala zima la uundwaji wake wa kuvutia zaidi na ulio na mapambo mengi kama vile televisheni, kiyoyozi, kamera za usalama(CCTV Camera) ambazo zitasaidia kuonyesha usalama ndani ya basi, endapo utatokea uhalifu wowote muhusika ataonekana mara moja. Pamoja na kuwepo vyote hivyo pia kuna na viti kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum ambao ni walemavu wa viungo pamoja na mama wajawazito.

TUANGALIE BAADHI YA SEHEMU KATIKA BASI HILI;

A. STELINGI - STEERING WHEEL
Mfumo wa stelingi ni ZF ya Ujerumani, wenye ubora wa kimataifa na unaozingatia usalama wa basi liendeshwapo barabarani muda wote. Pia kiti cha dereva kina uwezo wa kumpunguzia uchovu wa kukaa kwa muda mrefu ili kumsaidia kuwa makini aendeshapo basi husika ili kuepukana na ajali.

B. TAIRI - TYRE

Matairi bora yaliyothibitishwa na viwango vya kimataifa (ISO) ili kuweza kukabiliana na mabadiriko ya tabia nchi.

C. KIZIMIA MOTO - FIRE EXTINGUISHER
Mitungi maalum ya kuzimishia moto utokanao na vimiminika (mafuta), gasi, hitilafu za umeme n.k

D. INJINI - ENGINE
Aina ya injini ni CUMMINS iliyotengenezwa nchini Marekani (USA) ndio inayotumika katika mabasi yaendayo kwa haraka, injini hii kwa kiasi kikubwa imepunguza uchafuzi wa mazingira, imedhibiti uchafuzi wa mazingira (air pollution), makelele (noise pollution)

E. KAMERA ZA USALAMA - CCTV CAMERAS
Skrini ndogo yenye ukubwa wa inchi saba inayo dhibiti kamera 16 zilizomo ndani ya basi zinazo onesha yote yanayojiri ndani ya basi na kwa kupitia teknolojia iliyowekwa ndani ya kila basi yenye uwezo wa kutuma picha za matukio yote yanayojiri ndani ya basi liwapo barabarani kwenda kituo kikuu cha udhibiti na uchunguzi na matukio ya kihalifu na uharibifu wa samani.

F. VITI - SEATS
Ndani ya basi haki za walemavu, wazee, wajawazito zimezingatiwa kwa kutengewa viti maalum kulingana na mahitaji husika ikiwemo vikuju vya kushika kwenye bomba kwa abiria wanao simama.
 
View attachment 341751

Asante kwa taarifa mkuu
 
Shukrani kwa Elimu ustaadh. Sijajua tuna mpango gani endelevu wa kuhakikisha huduma hii inakua ya kudumu. Yatanunuliwa mengine mapya ndani ya muda gani? Yatafanyiwa service kama yanavyohitaji au wajanja watatumia fursa kujinufaisha? Tumeona mfano wa mabasi ya UDA, huwa yanakuja mapya, yanachakaa na kupotea kabisa lakini sijawahi kusikia MTU kawajibishwa.
Huduma hii nzuri itakua ya kudumu na endelevu?
 
Back
Top Bottom