Ligi ya kwanza soka wanawake Tanzania 2015

Ligi ya kwanza soka wanawake Tanzania 2015

Salamander

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
28,545
Reaction score
15,781
141229134045_wanawake_2015_640x360_bbc_nocredit.jpg





Mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) yanazinduliwa rasmi Januari Mosi mwakani kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwa mechi kati ya wenyeji Mwanza na Mara. Mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya Azam itachezwa kuanzia saa 10 jioni. Mashindano hayo yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin yatachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini katika hatua ya kwanza.

Januari 10 mwakani ndipo zitachezwa mechi kwa mikoa yote ambapo Geita itakuwa mwenyeji wa Kagera (Uwanja wa Geita), Tabora vs Kigoma (Ali Hassan Mwinyi), Simiyu vs Shinyanga (Uwanja wa Simiyu), Arusha vs Manyara (Sheikh Kaluta Amri Abeid), na Kilimanjaro vs Tanga (Uwanja wa Ushirika).

Mechi nyingine ni Lindi itaikaribisha Mtwara kwenye Uwanja wa Ilulu, Ruvuma vs Njombe (Uwanja wa Majimaji), Mbeya vs Iringa (Uwanja wa Sokoine), Katavi vs Rukwa (Uwanja wa Katavi), Dodoma vs Singida (Uwanja wa Jamhuri) na Pwani itakuwa mwenyeji wa Morogoro katika Uwanja wa Mabatini.

Timu hizo zitarudiana Januari 13 mwakani, ambapo baada ya matokeo ya nyumbani na ugenini timu iliyoshinda ndiyo itakayoingia hatua inayofuata ambayo pia itashirikisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke.


Hatua hiyo, mechi zake za kwanza zitachezwa Januari 17 mwakani wakati zile za marudiano zitafanyika Januari 21 mwakani.


Baada ya hapo, hatua itakayofuata ni robo fainali, nusu fainali na fainali ambayo ndiyo itakayotoa bingwa wa michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya kwanza nchini.


Mdhamini atatoa jezi kwa timu zote zinazoshiriki kabla ya kuanza mashindano hayo.


Source BBC-Swahili:
Tanzania:ligi ya kwanza soka wanawake 2015 - BBC Swahili



​
 
Acheni kuuwa soka la w/wake kwa siasa ligi au mashindano? kwanini msingeshirikisha vilabu? DAR pekee kuna timu zaidi 20
 
Acheni kuuwa soka la w/wake kwa siasa ligi au mashindano? kwanini msingeshirikisha vilabu? TUNATAKA LIGI SIO MASHINDANO!
 
Lina muhando usiongoze soka kwa mazoea hiyo TAIFA CUP wachezaji wanatoka wapi? kumbuka vilabu ndio walezi wa wachezaji.
 
KATIBUA katika maendeleo ni lazima uanzie mahali.Taifa cup ina umuhimu wa kipekee kwa mpira wa nchi hii maana inashirikisha nchi nzima.Dar es salaam itaingiza timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.Kuna program nyingine ya kitaifa inakuja ambayo itakuwa ni kutumia vocational centres kufundisha wanawake urefa,ukocha na kucheza mpira.Bila kuweka misingi kwa kufundisha wanawake urefa,ukocha na utawala hatutaweza kuendeleza women football.Ligi itakuja tu ni suala la muda na mipango,kikubwa Taifa zima lishiriki.
 
Last edited by a moderator:
Usikurupuke kujibu nalijua soka la w/wake kuliko ww soka lina zaidi ya miaka 20, Mnawatoa wp? mmewaandaa! Proin mnaibiwa
 
TAIFA CUP si mara ya kwanza imekwishafanyika miaka 10 iliyopita bila mafanikio. Kwanini amtaki kuanzisha ligi ya vilabu?
 
Mikoa karibia yote ina timu za w/wake bara/visiwani ila mmeona fungu basi mnataka kufaidisha matumbo yenu! INUENI SOKA!
 
KATIBUA katika maendeleo ni lazima uanzie mahali.Taifa cup ina umuhimu wa kipekee kwa mpira wa nchi hii maana inashirikisha nchi nzima.Dar es salaam itaingiza timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.Kuna program nyingine ya kitaifa inakuja ambayo itakuwa ni kutumia vocational centres kufundisha wanawake urefa,ukocha na kucheza mpira.Bila kuweka misingi kwa kufundisha wanawake urefa,ukocha na utawala hatutaweza kuendeleza women football.Ligi itakuja tu ni suala la muda na mipango,kikubwa Taifa zima lishiriki.

Hongera sana ndugu rais , hao watu jamii ya katibua ndo ambao huamini soka lipo dar tu....hawataki na sisi wa mikoani dada zetu wapate nafasi.....kwa huku mikoani watu hawana uwezo kuanzisha vilabu hivyo wachezaji hawawezi kupata fulsa ya mashindano... timu ikiwa ni ya mkoa lazima itapata msaada wa serikali ya mkoa....

Hongereni kwa wazo zuri mh jamali malinzi
 
Last edited by a moderator:
Usikurupuke kujibu nalijua soka la w/wake kuliko ww soka lina zaidi ya miaka 20, Mnawatoa wp? mmewaandaa! Proin mnaibiwa

acha wivu wa kike nenda kwa rugemarila nawewe ugaiwe za escrow
 
KATIBUA katika maendeleo ni lazima uanzie mahali.Taifa cup ina umuhimu wa kipekee kwa mpira wa nchi hii maana inashirikisha nchi nzima.Dar es salaam itaingiza timu tatu Kinondoni Ilala na Temeke.Kuna program nyingine ya kitaifa inakuja ambayo itakuwa ni kutumia vocational centres kufundisha wanawake urefa,ukocha na kucheza mpira.Bila kuweka misingi kwa kufundisha wanawake urefa,ukocha na utawala hatutaweza kuendeleza women football.Ligi itakuja tu ni suala la muda na mipango,kikubwa Taifa zima lishiriki.
Jamal Malizni

Mkuu wanaume wanfundishiwa wapi? maana tutofautishe huu mpira wetu wa mchangani na mpira wa darasani?
makocha wetu w amchangani na makocha wa darasani?
marefa wetu wa mchangani na Marefa wa darasani?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom