Ligi Kuu Bara : Young Africans SC vs Mwadui FC

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,780
10,710
Baada ya Simba SC kugongwa jana na Azam FC (Lambalamba), leo hii machampioni wa kabumbu Tanzania watakuwa na kazi moja tu, kuwathibitishia Simba kuwa nafasi yao ni mkiani!

Tuwe pamoja mwanzo hadi mwisho wa mtanange huu.
=======

Mechi itaanza kuchezwa mishale ya saa kumi na nusu alasiri uwanja wa Uhuru ambapo Yanga atakuwa mwenyeji kuwakaribisha timu ya Mwadui kutoka Shinyanga.

Dk 57 Msuva anaingia vizuri tena, anaachia shuti kali hapa, goal kick
DK 56, krosi safi ya Msuva, Cholo anatokea na kuokoa hapa


Dk 54 Mwadui wanashambulia hapa lakini wanaamua kurudi nyuma huku Yanga wakiwa wachache mbele, mashabiki wanazomea hapa
SUB Dk 52 Kaseke anakwenda benchi nafasi inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 50 Yondani anautoa mpira nje na MWadui wanapata kona
KADI 49 Mwamuzi Jonesia Lukyaa anamlamba kanavalo kadi ya njano kwa kucheza kindava
Dk 45, Yanga wanaanza kwa kasi, wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Mwadui. Goal kick

MAPUMZIKO
-Msuva anaachia mkwaju mkali hapa, Kado anapangua vizuri inakuwa kona hapa. Hata hivyo haina matunda

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Yondani analazimika kupiga kichwa akiokoa krosi ya Kabunda. Kona ya pili kwa Mwadui, Kona ya Seseme, Dida anadaka kwa ulaini
Dk 44 sasa, Mwadui wanaendelea kugongeana vizuri lakini katikati ya uwanja
Dk 42, Dida anatoka nje na kuutoa mpira, inakuwa konaa ya kwanza ya Mwadui FC
Dk 41, Malika tena anaokoa mpira na kuwa kona. Inachongwa, Kamusoko anaunganisha shuti kali lakini goal kick
Dk 40, Malika anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Msuva, inazaa kona hapa. Yanga wanaichonga lakini haina faida
KADI Dk 37, kadi ya kwanza ya njano, Aiye wa Mwadui FC anazawadiwa baada ya kumfanyia madhambi Yondani
Dk 35, bado mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 31, Mustappha anatoa mpira nje, inakuwa kona langoni kwa Mwadui FC


Dk 26, Kado anafanya kazi ya ziada, anaruka na kuudaka mpira wa Zulu
DK 20 sasa, Mwadui FC wanaonekana wamejipanga kujilinda sana na mashambulizi ya kushitukiza
Dk 20, Nonga anaingia vizuri hapa lakini Mwinyi analazimika kumuangusha
Dk 16, Mwadui FC wanaonekana wakiwa wametulia, angalau wanagonga hata pasi tano. Lakini Yanga wanaendelea kufika langoni mwa Mwadui FC
Dk 12, Kado yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 10, Mwadui wanafanya kazi ya ziada kuokoa, inakuwa kona na Yanga wanapiga. Hakuna kitu
Dk ya 8, Kado anafanya kazi ya ziada kuudaka mkwaju wa Msuva. yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi


Dk 7, Msuva anaingia vizuri na kumtengenezea Tambwe lakini anaachia shuti kuuubwaaa
Dk 5, Msuva anauwahi mpira wa krosi ya Juma Adul lakini anashindwa kulenga lango
Dk 4, krosi maridadi ya Mwinyi Haji lakini Kado anaruka juu na kupangua
DK 2, Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
Dk ya 1 Mechi imeanza Mwadui wakianza kusukuma mashambulizi ingawa, lakini Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwa Mwadui na kipa Shabani Kado anaondosha hatari


1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Justin Zullu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Haruna Niyonzima
11. Deusi Kaseke

Akiba
- Beno Kakolanya
- Oscar Joshua
- Yusufu Mhilu
- Emanuel Martin
- Juma Saidi
- Obrey Chirwa
- Geofrey Mwashiuya

Kwa hisani ya Saleh Jembe
 
Hiyo jana mambo yalikuwa hivi :

586e319dd61b2f9510ecc8f5413e03cb.jpg
 
Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Mwadui leo
1. Deogratius Munishi
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Nadir Haroub
5. Kelvin Yondani
6. Justin Zullu
7. Saimoni Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Haruna Niyonzima
11. Deusi Kaseke

Akiba
- Beno Kakolanya
- Oscar Joshua
- Yusufu Mhilu
- Emanuel Martin
- Juma Saidi
- Obrey Chirwa
- Geofrey Mwashiuya
 
Dk ya 8, Kado anafanya kazi ya ziada kuudaka mkwaju wa Msuva. yanga wanaendelea kushambulia kwa kasi

Dk 7, Msuva anaingia vizuri na kumtengenezea Tambwe lakini anaachia shuti kuuubwaaa

Dk 5, Msuva anauwahi mpira wa krosi ya Juma Adul lakini anashindwa kulenga lango

Dk 4, krosi maridadi ya Mwinyi Haji lakini Kado anaruka juu na kupangua

DK 2, Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango

Dk ya 1 Mechi imeanza Mwadui wakianza kusukuma mashambulizi ingawa, lakini Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwa Mwadui na kipa Shabani Kado anaondosha hatari
 
Back
Top Bottom