Habari wakuu,
Tunaelekea kuhitimisha msimu na hali inamtabiria bashiri njema Yanga kuelekea kuutwaa ubingwa kwa kukalia kiti ikiwaacha wapinzani wake wa karibu, Azam FC na mtani wake Simba.
Kutoka Shinyanga tuwe sote pamoja niwajuze yale yatakayojiri uwanjani kwa chama la wana kuwakabili wazee wa Jangwani.
====
00' Kipenga kimepulizwa na Yanga ndio wameaza kusukuma gozi kutokea dimba la kati
02' Donald Ngoma anaandika goli la mapema baada kuwazidi mbio mabeki wa stand na kumchungulia mlinda mlango.
16' Mpira wa adhabu ndogo unapigwa kuelekea lango la stand na kuzaa kona ambayo haikuzaa matunda.
17' Maguli anapanda na mpira wa kushtukiza hata hivyo anapiga mpira hafifu
23' Telela anakosa goli baada ya kujaribu mpira wa mbali ambao unaenda nje
25' Maguli anapiga mpira wa adhabu ambao unababatiza ukuta wa Yanga na kuzaa kona
29' Maguli anakosa goli baada mabeki wa Yanga kushindwa kujipanga, unambabatiza mlinda mlango.
44' Donald Ngoma anaiandikia Yanga goli la pili baada kumzunguka kipa
45+2' Mpira unaenda mapumziko, Stand 0-2 Yanga
45' Mpira umerejea kumalizia ngw'e ya mwisho ya mchezo
63' Yanga wanaandika bao la tatu kupitia kwa Tabwe kwa kupiga kichwa mpira wa kona
81' Stand wanapata goli kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Maguli, Stand 1-3 Yanga
90+3' Refa anapuliza kipenga kuashiria mwisho wa mchezo. Stand United 1-3 Yanga