Ligi kuu bara: Mbeya city Vs Yanga (0-2)

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari wakuu,
Leo ni mechi ya ligi kuu Tanzania bara kati ya mabingwa wa Tanzania bara, Yanga(kama rufaa ya Azam itatupwa) dhidi ya timu ya jiji la Mbeya, Mbeya city. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri.
=====




90+3' Mwamuzi anapiga filimbi kuashiria mwisho wa mchezo, Mbeya city 0-2 Yanga
84' Tabweeeee, shuti kali lililomshinda Juma Kaseja kutoka nje ya 18, Mbeya city 0-2 Yanga

75' Mbeya city wanakosa goli baada ya mshambuliaji kushindwa kumalizia pasi nzuri kutoka winga
59' Donald Ngoma anakosa goli baada ya kubaki na Kaseja hata hivyo alipiga pembeni
56' Deus Kaseke naupata mpira baada ya mabeki kujichanganya, anakosa goli baada ya kupiga shuti hafifu
45' Mpira unarejea kutoka mapumziko

45+2' Refa anapuliza kipenga kuashiria mpira unaenda mapumziko
43' Mbeya city wanacheza pasi nzuri kuelekea goli la Yanga hata hivyo offside inaharibu mpango wao
40' Selemani Mangoma wa Mbeya city anakosa goli baada ya kuachia shuti lililombabatiza mlinda mlango
28' Deus Kaseke anakosa goli baada ya kupiga juu kidogo ya goli
27' Kevin Yondani anaingia kwa upande wa Yanga kwa kutoka Vincent Bossou alieumia
23' Juma Abdul anapiga mpira wa adhabu ndogo na Ngoma kupiga kichwa ambapo kipa Juma Kaseja alijitahidi kuudaka hata hivyo aliumia
15' Yanga wanafunga bao la kuongoza kupitia mpira wa kona(Vincent Bossou)
08' Mbuyu Twite anatoka nje kumpisha Telela baada ya kuumia
00' Muamuzi kapuliza kipenga kuashiriria mwanzo wa mchezo
 
SUB Dk 8, Telela anaingia kuchukua nafasi ya Twite aliyeumia

Dk 5 Twite anatolewa nje baada ya kuanguka. Anatibiwa ingawa dalili zinaonyesha huenda akabadilishwa

Dk 3, Juma Abdul anaachia shuti kali la mpira wa adhabu, Kaseja anadaka, unamtoka lakini anadaka tena

Dk 2, Chombo anajaribu kuachia mkwaju lakini hata hivyo hakulenga lango

Dk 1, mechi imeanza taratibu huku ikionekana kila timu inaosoma nyingine
 
Dk 31, Redondo anajaribu kupiga shuti, hata hivyo linaonekana ni dhaifu, goal kick

SUB Dk 30, Yondani anaingia kuchukua nafasi ya Bossou aliyeumia
 
Simba watakuwa kama yule mbunge aliesema bangi ihalalishwe maana watu wake wakivuta wanapata nguvu san
 
Back
Top Bottom