plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,395
- 1,439
Hi Guys.
Moja kwa moja nianze kufafanua kichwa nilichokiweka hapa juu, ni kwamba hivi ni visa mbalimbali ambavyo vimetokea katika maeneo mbalimbali hapa duniani. Lengo la visa hivi kwenye uzi huu ni kwa ajili ya kujifunza kupitia wengine, na visa hivi vinalenga hasa kubadilisha mitazamo yetu kimaisha kwa namna moja ama nyingine pia vitatufunza ni jinsi gani tuishi kwenye jamii.
"Hata wana wa Israel walipokuwa wanataka Yesu awape ishara, hawakupewa ishara yeyote isipokuwa Yesu alizidi kusema nao kwa mifano"
Binafsi nitaanza na visa kadhaa ili kuwakaribisha wengine nao waweze kuchangia visa mbali mbali, lengo hapa ni ili tuweje kujifunza kupitia mambo yaliyotokea. Pia baada ya visa hivi nitarejea tena na tena kuleta visa vingine vyenye kuelimisha , ni matumaini yangu mtapenda na kufurahia. Niwakaribishe sasa katika mada yetu pendwa kama ifuatavyo.
NB: Kuna muda nitaweka majina ya watu kwenye visa, sio majina yao halisi, ili kuficha uhalisia wao.
CEO AMKAMATA OMBAOMBA AKIMWIBIA PIZZA.
"Nenda kakae, nitakuletea order yako", ilisikika sauti ya mhudumu ikizungumza.
"Ashh you shit, unajua ni kiasi gani hii suti inauzwa, unaniparamia tu utaweza kweli gharama za hii suti wewe", ilikuwa ni sauti ya mtu aliyepiga suti yake kali huku ameshika briefcase
inayoonekana ni ya bei mbaya pia akimkemea mtu aliyeonekana kama vile ombaomba aliyeingia kwenye hoteli ile akijaribu kutafuta rizki kwa wateja waliopo hotelini humo.
"Samahani sana, inawezekana upo sahihi", kijana huyo alijibu huku akimtaka radhi mtu yule.
Basi mtu yule, ambaye ameonekana kama vile Manager ni kweli alikuwa CEO kwenye taasisi moja maarufu hapa nchini. Naye alisogea pale kaunta na kuagiza kama ifuatavyo.
"Naweza kupata slices tatu za pizza?"
"Hapana, hapa tunauza slices tano kwa dollar 5", alijibiwa na mhudumu.
"Hilo halina tatizo, nihudumie.", alijibu.
"Nenda kakae, nitakuletea order yako", mhudumu alimalizia.
Basi tajiri yule alienda kukaa kwenye meza yenye viti viwili vinavyoangaliana, akafungua briefcase
yake akatoa taptop na kuanza kuichezea, njiani alimpita kijana yule aliyemdhania ni ombaomba akishangaa kinanda kilochopo hotelini hapo. Na baada ya mda mchache kijana yule akarudi na kukaa meza moja na yeye.
"What the heck", tajiri alisikika akilalamika kwa sauti ndogo huku akijishika kichwa asijue cha kufanya.
"Hii hapa pizza yako mkuu", alikuwa ni sauti ya mhudumu huku akiweka slices tano za pizza kwenye meza waliyokuwepo na kisha kuondoka.
Ikaanza kama ifuatavyo tajiri akaanza kuchukua slice moja na kula huku kijana naye akaamua kuchukua slice nyingine naye akaendelea kula. Tajiri akamwangalia kwa hasira bila kumsemesha chochote.
Baada ya wote kumaliza slice ya kwanza, kijana akawa wa kwanza kuchukua slice ya pili akaendelea kula na tajiri naye akachukua slice ya pili ili naye ale, hapa pia tajiri hakumsemesha chochote, mezani imebaki slice moja tu.
Ghafla tajiri akamwona kijana amenyoosha mkono amechukua slice ya mwisho, guess what, cha mwisho kinauma bana

. Hapa tajiri akaamua kumtolea uvivu.
"Unadiriki kuchukua na slice ya mwisho", tajiri alifoka kwa hasira.
"Unajua ni bora ukaenda kutafuta kazi halali kuliko kuendelea kuiba pizza za watu", tajiri aliendelea kufoka.
"Inaonekana unanjaa sana", kijana alimjibu huku akigawa slice ya mwisho ya pizza na kumpatia tajiri nusu yake.
"Hii hapa pizza yako mkuu", ilikuwa sauti ya mhudumu huku akiweka slices tano zingine za pizza kwenye meza yao huku kijana bado ameshika vipande viwili vya pizza alivyogawa mkononi mwake.
"Hebu subiri, pizza za nini tena?", ilimbidi tajiri kumuuliza mhudumu.
"Ni pizza zako, mmeagiza order sawa", mhudumu alijibu na kuondoka baada ya kuweka pizza mezani.
"Ah.. Kwa..hi..yo zile zilikuwa pizza zako, na.. ume..amua kunikatia pizza ya mwi..sho ili tu..le wote?", tajiri alimuuliza huku akujing'atang'ata sana meno.
"Ndiyo, napenda kushare", kijana alijibu.
"Dah! Samahani sana ni..li..fikiri ni pizza zangu, nakuomba tule na hizi kwa pamoja.", alijibu huku akimtaka radhi.
Basi walikula pia pizza zile kwa pamoja na kwa furaha.
UJUMBE:
"Usiwe mwepesi wa kudhania."
MWANAMKE ALIYE MFRIENDZONE KAKA AMBAYE NI "NICE GUY"
"Huyu mfupi sana",
"Huyu amejazia kupita kiasi",
"Ah, huyu ndo kabisaa mtoto wa mama", iliuwa ni sauti ya Maria akikosoa picha za wanaume mbalimbali kwenye mtandao wa Instagram.
"Vipi kuhusu mimi?", Jackson aliyekuwa amekaa pembeni yake alimuuliza.
"You are too nice", alimjibu kwa kimombo tena kwa dharau.
"Ila sikuzote utakuwa best friend wangu", Maria aliongezea.
Hapa tuwekane wazi kuhusu huu msemo "Nice Guy" au " Mr Nice Guy". Hawa ni wale wanaume ambao wameonyesha kumpenda sana mwanamke hadi kufikia hatua mwanamke amekuwa na nguvu juu ya mwanaume wa haina hii na chochote atakachomwambia mwanaume huyo kiwe kizuri au kibaya, mwanaume huyo hana nguvu ya kukataa. Unaweza ukasema ni limbwata, ila utofauti wa hii na limbwata ni kwamba hii haijatumia uchawi. Hii kitaalamu inaitwa "Nice Guy Trap", nisiingie ndani sana maana hii inafaa kuwa mada kabisa. Ila kiufupi ni kwamba mwanzoni kabisa mwa urafiki mwanamke kabla ya kujihusisha kimahusiano na mwanaume huwa anampima, sitaweza kuanza kuelezea anampimaje ili kuepusha mada kuwa ndefu sana. Sasa mwanaume anapofail ndipo anajikuwa ameingia kwenye mtego unaoitwa "Nice Guy Trap", hapa mwanamke atamtumia mwanaume huyo kimaslahi tu na atakuwa tayari amekwisha kupoteza hisia kabisa na mtu huyo, hivyo humtumia kwa faida zake binafsi.
Sasa turudi kwenye hiki kisa chetu kati ya Jackson na Maria, tayari Jackson yupo kwenye huu mtego "Nice Guy Trap" na tutamwona kabisa jinsi anavyoshindwa kujinasua, na mwisho wa kisa hiki tutakuwa tumejifunza mambo mengi.
Siku moja Jackson na Maria walitoka out kwenda kufurahi pamoja, wakaenda kwenye mghahawa flani wa hadhi kidogo hapa jijini, wakala wakanywa na kufurahi pamoja. Wakiwa katika hali hiyo ya furaha, akaja mwanaume mmoja nadhifu akam-approach Maria, wakajoin wakakaa watatu huku mwanaume huyo akizidi sana kupiga story na Maria kiasi cha kum-ignore Jackson, wakaenda mbali zaidi kiasi cha kufikia kukubaliana kuondoka pamoja. Just imagine, tena mbele ya Jackson.
"Nadhani hautajali sana kurudi nyumbani peke yako. Si ndiyo?", Maria alikuwa akumsemesha Jackson aliyekuwa mda wote amekaa pembeni yao hali ya upweke.
"Ah yah! no no, ni sawa hamna shida", Jackson alijibu, ni kama vile ameamshwa kutoka usingizini, usingizi mzito wa mawazo.
"Asante, you're the best", Maria alijibu.
"Have fun", Jackson alimalizia.
MWEZI MMOJA BAADAE
"Hey, unaweza kuja? Ameniacha... Nakuhitaji sasa.", ilikuwa ni sms iliyoingia kwenye simu ya Jackson ikitokea kwa Maria.
Huwezi amini Jackson alienda tena alinunua na maua kabisa ili ampelekaa kama surprise. Akafika akamgongea mlango huku amezungusha mkono mmoja nyuma uliobeba maua ili amsurprise nayo rafiki yake kipenzi, sasa sijui alikuwa amepanga akamuombe Maria msamaha kwa hayo maua au ni nini, hata sijui.
Mlango ukafunguliwa na Maria na kisha Maria akamuuliza Jackson kama ifuatavyo:
"Hey, unafanya nini hapa?"
"Unamaanisha nini?, umeniambia nije.", Jackson alijibu huku na yeye akiuliza swali.
Akajibiwa tu kirahisi, "Oh, samahani, tulisuluhisha na mpenzi wangu, kwahiyo ntakupigia baadaye", wakati huo yule mwanaume aliyeondoka na Maria ile siku waliyokuwa na Jackson akatoka mlangoni kuchungulia.
"Vipi", alisalimia.
"Safi", Jackson alijibu na kuondoka.
Jackson aliona hata yale maua hayana maana akaamua kuyatupa kwenye ndoo za taka zilizopo katikati ya jiji.
MIEZI MICHACHE MBELENI.
Maria akaanza kupitia changamoto katika mahusiano yake, mwanaume wake akamwacha na kwenda kwa mwanamke mwingine, Maria alibaki mpweke na kuanza kum-miss best friend wake wa zamani, Jackson, alikuja kugundua labda Jackson alikuwa ni mtu sahihi kwake.
"Hey, unaweza kuja kwenye ule mghahawa wetu tuliokuwa tukiupenda? Nakuhitaji sasa hivi...", ilikuwa ni sms iliyoingia kwenye simu ya Jackson, ikitokea kwa Maria.
Jackson alienda ila safari hii sikuona akibeba maua kama awali, sijui ndo alikuwa ameanza kunasuka kwenye huu mtego "Nice Guy Trap".
"Vipi", alisalimia
"Wow, Jackson nimefurahi kukuona", Maria ghafla alimkimbilia Jackson kwa furaha huku akiyasema maneno hayo na kumkumbatia.
"Kila kitu kipo sawa? Au kunatatizo?", Jackson kwa mshangao alijikuta akiuliza maswali mawili kwa mkupuo.
"Umm, mambo hayajaniendea sawa kwa upande wangu", Maria alijibu.
"Unamaanisha nini?", Jackson aliendelea kuuliza.
"Siku zote nimekuwa nikiwapenda watu ambao mwisho wa siku wamekuwa wakiniumiza, na sikuwa nimegundua nilikuwa na mtu sahihi miaka yote hii, ila nipo tayari sasa", Maria alijielezea.
"Nafurahi upo tayari ila..
Unajua, nilikucare sana miaka yote hii lakini hukuona umuhimu wangu, nilikuwa upande wako wakati ukiwa mpweke, nilikusaidia pale ulipohitaji", Jackson alijibu.
"Ila utakuwa best friend wangu siku zote", Jackson alimalizia.
UJUMBE:
"Usimtumie yeyote kwa maslahi, lile utakalomtendea mwenzako, vivyo hivyo na wewe utatendewa."
MWANAMKE ALIYEMZUNGUKA RAFIKI YAKE.
"Mme wangu, Jane atakuwa hapa mda mchache ujao", Suzzy alikuwa akiongea na mme wake Andrew.
"Ni mara ngapi nikuambie kwamba sitaki kukuona na Jane na hunisikii", Andrew alimfokea mke wake Suzzy.
"Tumekuwa marafiki tangu sekondari, unashindwa vipi kumwamini", Suzzy alisisitiza.
"Sikiliza Suzzy, Jane nimesamsoma hakufai, anakutumia kwa faida", Andrew alikuwa akijaribu kumwelewesha.
"Hodii...", ilisikia sauti ya kike nje mlangoni.
"Ingia mlango upo wazi", alidakia Suzzy.
Jane akaingia ndani, Andrew akaonyesha wazi kabisa kutopendezwa na kitendo kile.
"Samahani Suzzy, niazime koti lako nitakurudishia", Jane alimsemesha Suzzy, wakati wote huo, Andrew alikuwa akitazama chini kwa masikitiko.
"Usijali lichukue tu", Suzzy aliruhusu.
"Asante, vipi kuhusu ule mpango wetu wa kutoka out", Jane aliendeleza mazungumzo.
Waliondoka na Suzzy alimuaga mumewe huku akimpa ahadi kwamba atakuwa salama. Wakiwa out wanapatwa kinywaji, akaja mwanaume mmoja mtanashati akawaomba awatoe out awapeleke kwenye part, Suzzy akadakia kwa kumkatisha na kumwambia hapana na hawahitaji. Ghafla Jane akadakia na kumwambia mwanaume huyo kwamba asimsikilize yeye yuko tayari. Suzzy alizidi kusisitiza kwamba hataki lakini rafiki yake Jane alisisitiza kwamba yeye ana gari na ni lazima waende hivyo Suzzy akawa hana chaguzi.
Wakafika wakiwa watatu wakaanza kula na kunywa. Ndipo Suzzy akaamua kuuliza, hiyo part iko wapi, akaambiwa atulie. Basi Jane aliendelea kufurahi na mwanaume huyo wakicheka na kuenjoy. Suzzy akamtumia mumewe sms akimjulisha kwamba kumbe alikuwa sahihi na hapo hajihisi kuwa salama.
Ndipo Suzzy, akaamua kuwaambia yeye anaondoka, rafiki yake Jane akamsisitiza asiondoke, akasisitiza wanywe basi kinywaji kimoja ndipo waondoke, huku akimkumbatia kwa kumwonyesha upendo wa hali ya juu. Wakati huohuo akiwa amemkumbatia alitumbukiza kidonge cha madawa ya kulevya kwenye glass ya Suzzy iliyokuwepo nyuma yake.
Suzzy alipoendelea kunywa akaanza kuona maruerue ndiposa alipojitahidi kuondoka alishindwa na kudondokea mlangoni, huku Jane akiendelea kula bata na mwanaume huyo wakicheka na kufurahi.
Andrew, mume wa Suzzy alipoona ujumbe wake alipiga simu mfululizo bila kupokelewa, Jane alikuwa akiiangalia tu ikiita hadi kukata.
UJUMBE:
"Sio kwakuwa wanakukumbatia au kukuonyesha upendo, eti ndo wanakupenda"
"Just because they hug you, doesn't mean they love you."
Bado sijamaliza visa nitarudi kuendelea, ngoja nipate mapumziko kidogo. Niwakaribishe sasa na ninyi muweze kuleta visa mbalimbali vyenye mafunzo mbalimbali, kumbuka utakaposhare story yako utasaidia kubadili maisha ya wengi.
Utakaposhare pia uzi huu, utasaidia pia kubadili maisha.
KARIBUNI.
Moja kwa moja nianze kufafanua kichwa nilichokiweka hapa juu, ni kwamba hivi ni visa mbalimbali ambavyo vimetokea katika maeneo mbalimbali hapa duniani. Lengo la visa hivi kwenye uzi huu ni kwa ajili ya kujifunza kupitia wengine, na visa hivi vinalenga hasa kubadilisha mitazamo yetu kimaisha kwa namna moja ama nyingine pia vitatufunza ni jinsi gani tuishi kwenye jamii.
"Hata wana wa Israel walipokuwa wanataka Yesu awape ishara, hawakupewa ishara yeyote isipokuwa Yesu alizidi kusema nao kwa mifano"
Binafsi nitaanza na visa kadhaa ili kuwakaribisha wengine nao waweze kuchangia visa mbali mbali, lengo hapa ni ili tuweje kujifunza kupitia mambo yaliyotokea. Pia baada ya visa hivi nitarejea tena na tena kuleta visa vingine vyenye kuelimisha , ni matumaini yangu mtapenda na kufurahia. Niwakaribishe sasa katika mada yetu pendwa kama ifuatavyo.
NB: Kuna muda nitaweka majina ya watu kwenye visa, sio majina yao halisi, ili kuficha uhalisia wao.
CEO AMKAMATA OMBAOMBA AKIMWIBIA PIZZA.
"Nenda kakae, nitakuletea order yako", ilisikika sauti ya mhudumu ikizungumza.
"Ashh you shit, unajua ni kiasi gani hii suti inauzwa, unaniparamia tu utaweza kweli gharama za hii suti wewe", ilikuwa ni sauti ya mtu aliyepiga suti yake kali huku ameshika briefcase
inayoonekana ni ya bei mbaya pia akimkemea mtu aliyeonekana kama vile ombaomba aliyeingia kwenye hoteli ile akijaribu kutafuta rizki kwa wateja waliopo hotelini humo."Samahani sana, inawezekana upo sahihi", kijana huyo alijibu huku akimtaka radhi mtu yule.
Basi mtu yule, ambaye ameonekana kama vile Manager ni kweli alikuwa CEO kwenye taasisi moja maarufu hapa nchini. Naye alisogea pale kaunta na kuagiza kama ifuatavyo.
"Naweza kupata slices tatu za pizza?"
"Hapana, hapa tunauza slices tano kwa dollar 5", alijibiwa na mhudumu.
"Hilo halina tatizo, nihudumie.", alijibu.
"Nenda kakae, nitakuletea order yako", mhudumu alimalizia.
Basi tajiri yule alienda kukaa kwenye meza yenye viti viwili vinavyoangaliana, akafungua briefcase
yake akatoa taptop na kuanza kuichezea, njiani alimpita kijana yule aliyemdhania ni ombaomba akishangaa kinanda kilochopo hotelini hapo. Na baada ya mda mchache kijana yule akarudi na kukaa meza moja na yeye."What the heck", tajiri alisikika akilalamika kwa sauti ndogo huku akijishika kichwa asijue cha kufanya.
"Hii hapa pizza yako mkuu", alikuwa ni sauti ya mhudumu huku akiweka slices tano za pizza kwenye meza waliyokuwepo na kisha kuondoka.
Ikaanza kama ifuatavyo tajiri akaanza kuchukua slice moja na kula huku kijana naye akaamua kuchukua slice nyingine naye akaendelea kula. Tajiri akamwangalia kwa hasira bila kumsemesha chochote.
Baada ya wote kumaliza slice ya kwanza, kijana akawa wa kwanza kuchukua slice ya pili akaendelea kula na tajiri naye akachukua slice ya pili ili naye ale, hapa pia tajiri hakumsemesha chochote, mezani imebaki slice moja tu.
Ghafla tajiri akamwona kijana amenyoosha mkono amechukua slice ya mwisho, guess what, cha mwisho kinauma bana

. Hapa tajiri akaamua kumtolea uvivu."Unadiriki kuchukua na slice ya mwisho", tajiri alifoka kwa hasira.