Mwizi akiiba anakatwa mkono,so what?? Mwanamke akifanya uzinzi wazinzi wanaume wanampiga mawe??? allah Ni shetani sio Mungu
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kwa mantiki yako unafikiri kila anayeiba ni wa kukatwa mkono tu? Kuna wengine wanaiba kutokana na ugumu wa maisha, kuna wengine dhiki ya ghafla iliyowakumba na kiasi kadhaa cha mali kinahitajika ama tuseme hela ya lupango au Ada ya watoto na yeye hana na hajapata sehemu nyengine unafikiri atafanyaje huyo kama akipata fursa?
Ama Mali nyengine au vitu vyenye thamani vinawekwa katika hali ya ushawishi, mathalani vito vya dhahabu kama unaviweka kiholela mwengine anaweza akaingiwa na tamaa ya ghafla na akapita nacho.
Sasa unafikiri mtu akiiba tu ana katwa mkono? Hayo yote yanaangaliwa na mengineyo, kwa maana ni kipi kimemfanya mtu aibe? Ikiwa kama ni masuala ya kimaisha basi serikali itawajibika yenyewe ili kutengeneza mfumo bora wa maisha kwa raia wake. Ila kama ikithibiti mtu ni mienendo yake ni wizi tu hapo sheria itachukua hatma yake.
Na suala la mzinifu kupigwa mawe unaona ni baya!! Kwanza kwa nini uzini? Si umeruhusiwa kuoa/kuolewa sasa kwa nini uzini? Tena kwa wanaume mpaka wake 4 halafu unazini tena! Kama ni haki za ndoa hazitimilizwi kuna taratibu za talaka na unaruhusiwa kuoa/kuolewa tena.
Yakupasa ufahamu ni wajibu juu ya mamlaka husika kujiwekea utaratibu wa kuenzi na kuishi katika maadili. Kiuslam asiyeoa/kuolewa ukizini adhabu yako ni kucharazwa viboko 100.
Ila kama umeoa/umeolewa ukibainika imekula kwako. Kubainika kwenyewe wawepo mashahidi 4 tena wafahamike ni wasema kweli, wakiwa 3 umechoropoka aisee! Sasa ndugu yangu mpaka udakwe yaani umekubuhu kwenye kuchepuka na adhabu ya kupigwa mawe itakudondokea.
Kwa uchache Uislam upo hivyo.