Licha Ya Uwekezaji Mkubwa Wa MO, Hizi Ni Sababu 5 Kwanini Simba SC Hawawezi Kuacha Ushirikina.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Kama tukiamua kuitaja Klabu Katika Tanzania inayoongiza kwa Ushirikina basi bila shaka ni Simba SC.

Tamaduni hii wamekuwa nayo tangu Kitambo. Na wamekuwa wakitumia Ushirikina Katika Maeneo tofauti tofauti.

Iwe kwa lengo la Kuwapunguzia Uwezo Wapinzani wake au kujiongezea Ushindani wao wenyewe.

Zifuatazo Ni Sababu Kuu 5 Kwanini Ushirikina Umekuwa Sehemu ya Maisha yao ya Kila Siku:-

1. Kushindana na Yanga SC Kimafanikio.

Simba hawaamini tu katika uwekezaji kuwa wana uwezo wa kufanya Makubwa. Bali wanaona tija kubwa sana kuboost jitihada kwa ushirikina kuhakikisha wanafika mbali zaidi kuwashinda wapinzani wao wa jadi Yanga SC.

2. Katiba Ya Klabu Inasupport Na Kutambua Ushirikina.

Ibara ya (4)

Ibara ndogo ya (2)

Kipengele b: Lengo la Klabu ni kushiriki na kishindana kikamilifu katika michuano ya ndani na nje ya nchi kwa kutumia nyenzo zote zilizopo ambazo hazienendi kinyume na taratibu ikiwa pamoja kamati za ufundi za kisasa na kijadi.

3. Pressure Kutoka Kwa Wachambuzi Na Sifa Kutoka Kwa Vyombo Vya Habari.

Vyombo vya habari vimekuwa kipaumbele kusifia na kutoa hoja ambazo kimsingi haziendani na uhalisia. Kwa mfano moja ya Kipindi kinaeleze kuwa ndani ya Miaka 4 Simba wamefanikiwa pakubwa kimataifa ikiwa ili hali kila msimu wanakomea nafasi ile ile walio komea msimu ulopita.

4. Idadi Kubwa Ya Waajiriwa Wasio Na Weledi Kwenye Klabu Yao.

Simba SC inajitapa wameajiri wafanya kazi proffessional katika klabu yao ili hali ukifuatilia kwa kina utagundua kuwa walio wengi ni waswahili mno na wengi wamepitia elimu za michongo michongo na za kuunga unga.

5. Hofu ya Kushindwa Kimafanikio na Yanga SC.

Kihistoria Yanga ndio Klabu yenye mafanikio makubwa sana ndani ya nchi. Hilo halina shaka wala ubishi. Wameshindana kwa kipindi kirefu na kusurrender, hivyo basi matamanio yao yamekuwa makubwa zaidi kuhakikisha wana set standard kwenye uwanja wa kimataifa.

Hilo lina wapa hamasa kubwa katika matumizi ya Ushirikina kuhakikisha lina wafikisha mapema katika eneo hilo.

Kiufupi ni kwamba kama kutakuwa na klabu kutoka Tanzania kushinda taji lolote la kimataifa basi hiyo Klabu itakuwa ni Dar es Salaam Young Africans SC.

ALAMSIKI.
 
Arggghh.
Screenshot_20220425165647.jpg
 
Ukiona mwenzako anatumia uchawi na unamsaidia hata timu iwe bora vipi ikija kwa Mkapa lazima ife basi na wewe tumia huo uchawi.

Ila thread kama hizi mngetafuta majukwaa ya watoto ndio mkawaambie kwamba kuna timu ya mpira hairogi.

Mimi nakumbuka zamani kanisa katoliki Chang'ombe walikuwa na paroko alikuwa anapenda sana mpira, walikuwa na timu ya kanisa inaitwa Ujirani mwema ilikuwa kwenye kombe ukikutana nao hao lazima ufe na walikuwa ni wachawi balaa, ila paroko mzungu hakuwa anashirikishwa kwenye kuroga wala hakuwa anajuwa siri ya timu yake kubeba makombe.
 
Imani ni imani iwe ya jadi ama hii ya wazungu... Nchi ni huru kila mmoja na imani yake... Mnapokua mnaabudu mizimu ya akina yakobo, ibrahim, Suleiman na Mohamed mbona sie hatuwabughuzi...

Waacheni watu na imani yao ndio maana Muslim anamuona mkristo kama mshirikina na mkristo anamuona Muslim hanakitu...

Nchi haina dini na inakubali imani zote
 
Kama tukiamua kuitaja Klabu Katika Tanzania inayoongiza kwa Ushirikina basi bila shaka ni Simba SC.

Tamaduni hii wamekuwa nayo tangu Kitambo. Na wamekuwa wakitumia Ushirikina Katika Maeneo tofauti tofauti.

Iwe kwa lengo la Kuwapunguzia Uwezo Wapinzani wake au kujiongezea Ushindani wao wenyewe.

Zifuatazo Ni Sababu Kuu 5 Kwanini Ushirikina Umekuwa Sehemu ya Maisha yao ya Kila Siku:-

1. Kushindana na Yanga SC Kimafanikio.

Simba hawaamini tu katika uwekezaji kuwa wana uwezo wa kufanya Makubwa. Bali wanaona tija kubwa sana kuboost jitihada kwa ushirikina kuhakikisha wanafika mbali zaidi kuwashinda wapinzani wao wa jadi Yanga SC.

2. Katiba Ya Klabu Inasupport Na Kutambua Ushirikina.

Ibara ya (4)

Ibara ndogo ya (2)

Kipengele b: Lengo la Klabu ni kushiriki na kishindana kikamilifu katika michuano ya ndani na nje ya nchi kwa kutumia nyenzo zote zilizopo ambazo hazienendi kinyume na taratibu ikiwa pamoja kamati za ufundi za kisasa na kijadi.

3. Pressure Kutoka Kwa Wachambuzi Na Sifa Kutoka Kwa Vyombo Vya Habari.

Vyombo vya habari vimekuwa kipaumbele kusifia na kutoa hoja ambazo kimsingi haziendani na uhalisia. Kwa mfano moja ya Kipindi kinaeleze kuwa ndani ya Miaka 4 Simba wamefanikiwa pakubwa kimataifa ikiwa ili hali kila msimu wanakomea nafasi ile ile walio komea msimu ulopita.

4. Idadi Kubwa Ya Waajiriwa Wasio Na Weledi Kwenye Klabu Yao.

Simba SC inajitapa wameajiri wafanya kazi proffessional katika klabu yao ili hali ukifuatilia kwa kina utagundua kuwa walio wengi ni waswahili mno na wengi wamepitia elimu za michongo michongo na za kuunga unga.

5. Hofu ya Kushindwa Kimafanikio na Yanga SC.

Kihistoria Yanga ndio Klabu yenye mafanikio makubwa sana ndani ya nchi. Hilo halina shaka wala ubishi. Wameshindana kwa kipindi kirefu na kusurrender, hivyo basi matamanio yao yamekuwa makubwa zaidi kuhakikisha wana set standard kwenye uwanja wa kimataifa.

Hilo lina wapa hamasa kubwa katika matumizi ya Ushirikina kuhakikisha lina wafikisha mapema katika eneo hilo.

Kiufupi ni kwamba kama kutakuwa na klabu kutoka Tanzania kushinda taji lolote la kimataifa basi hiyo Klabu itakuwa ni Dar es Salaam Young Africans SC.

ALAMSIKI.
We mwenyewe mshirikina halafu unakemea ushirikina. Hii nchi ina watu wa ajabu Sana.
 
Ukiona mwenzako anatumia uchawi na unamsaidia hata timu iwe bora vipi ikija kwa Mkapa lazima ife basi na wewe tumia huo uchawi.

Ila thread kama hizi mngetafuta majukwaa ya watoto ndio mkawaambie kwamba kuna timu ya mpira hairogi.

Mimi nakumbuka zamani kanisa katoliki Chang'ombe walikuwa na paroko alikuwa anapenda sana mpira, walikuwa na timu ya kanisa inaitwa Ujirani mwema ilikuwa kwenye kombe ukikutana nao hao lazima ufe na walikuwa ni wachawi balaa, ila paroko mzungu hakuwa anashirikishwa kwenye kuroga wala hakuwa anajuwa siri ya timu yake kubeba makombe.
Jwaneng Galaxy walimpiga Simba 3 hapo hapo kwa Mkapa.
 
We bwege kweli eti simba inajiri waswahili (ina waajiriwa wasiokuwa na weledi),, akina masingisa, manara na kocha wa magolikipa hujui kwamba wote hao ni scouting ya simba..
 
We chizi kweli waajiri wasio na weledi ndio hawa;
Senzo mlimchukua kutoka simba,
Manara mlimchukua kutoka simba,
Yule kocha wa goal keeper wa yanga ametoka simba,

hivi hao wafanyakazi wasio na sifa ndio wapoje na je simba wameajiri mtu yeyote kutoka yanga nyie endeleeni kujitekenya mtacheka CAF champion's league ikianza mje mseme simba wanaroga wakati nyinyi ndio waasisi.
 
Ni hivi, tumekutana na thread nyingi humu jukwaani, zikimlaani Ahmed Ally kwa kutokujua kazi yake. Badala ya kutoa taarifa za maendeleo ya Simba, amekuwa mtu wa mipasho, vijembe na kuhangaika na Yanga. Ahmed ni kisemeo cha klabu. Ina maana vikao vya klabu na menejiment nzima, ndio wanaozalisha kile ambacho Ahmed analisha public?

Pili, tumeona huyo Baraba akionekana mwana mitindo kwa mavazi na nywele. Huyo ndo utaona, alipotangulizwa South, aliishia kupiga picha na sanamu la Madiba. Yaani kutangaza utalii wa South! Alienda kuifanyia ujasusi Orlando, akaishia alipoishia.

Tatu, utaona kiongozi mkuu, Mo, anakazana kuwaahidi wachezaji mihela na magari. Utadhani klabu ni timu ya Taifa. Kwa hiyo kila mchezaji anaingia uwanjani akiwa anawaza zawadi badala ya trophy. Matokeo yake tunaishia kuona individual skills. Hii ni shida.

Mwisho, kutegemea wachezaji wachache. Tumeona kukosekana kwa Morison kumeyumbisha timu. Proper marking aliyofanyiwa Sakho kulifanya timu ipoteane mbele. Sifa alizopewa Kapombe za mechi ya kwanza zilimlewesha mpaka akasahau nafasi yake na kuanza kukimbilia mbele.

Kwa ujumla hayo yote ni matatizo ya uongozi na kukosa weledi kwa viongozi wa Simba.

Kazi iendelee
 
Kwenye namba moja..Simba SC inashindana na wakubwa wenzake kwenye nafasi ya 12 kwa ubora CAF, jipime mwenyewe upo nafasi ya ngapi hapo..?!

Namba tano, una mafaniko gani kuliko Simba? Kama kwa mpira Kimataifa, Simba amecheza nusu fainali na fainali ya moja ya michuano ya CAF.

Acheni kujipa umuhimu ambao hamna yaani...!
 
Ndo maana hata beki wao inonga alikuwa anatetemeka kama vile anataka kucheza amapiano ya south
 
Back
Top Bottom