Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,589
- 28,755
Viongozi wa harakati inayopigania utawala wa ndani mashariki mwa Libya jana walitangaza serikali mpya ya eneo la Barqa linalojumuisha nusu ya eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Viongozi hao wamesema serikali hiyo ya ndani itakuwa na jukumu la kuratibu maenedeleo ya eneo hilo. Pia wamesisitiza kuwa, pato la mafuta katika eneo hilo lenye visima vingi vya mafuta litasimamiwa na serikali hiyo ya ndani.
Serikali kuu ya Libya imepinga uamuzi huo na kusema nchi nzima ya Libya iko chini ya Waziri Mkuu, Ali Zeidan.
Wachambuzi wengi wanaamini kuwa, hatua hiyo ya viongozi wa Barqa imeanika wazi udhaifu wa serikali kuu na ni kengele ya hatari kwa serikali ya Ali Zaidan.
Makundi yenye silaha yameendelea kupata nguvu nchini Libya tangu kupinduliwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi miaka miwili iliyopita. Hali hiyo imepelekea Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Kijeshi ya nchi za Magharibi NATO kufikiria uwezekano wa kupeleka kikosi cha kimataifa nchini Libya ili kudhibiti hali ya mambo. ---
Source: Radio Tehran.