Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimewasilisha Shauri la Rufaa Na. 56/2025 katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), kikipinga uhalali wa kuzimwa kwa mtandao kote nchini Tanzania kilichotokea kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 4, 2025. Kuzimwa huko kulisababisha usumbufu mkubwa wa huduma muhimu za kidijitali ikiwemo benki mtandaoni, huduma za afya kwa njia ya mtandao, mawasiliano ya dharura pamoja na upatikanaji wa taarifa muhimu za umma wakati wa upigaji kura, hali iliyoleta hasara kubwa za kiuchumi kwa siku na kuathiri ustawi wa kijamii, kiraia na kiusalama wa wananchi.
Katika shauri hilo, LHRC inaomba Mahakama itoe tamko kwamba hatua hiyo ilikiuka Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kusababisha madhara makubwa kwa umma. Aidha, Kituo hicho kinaomba zuio la kudumu kuzuia kuzimwa kwa mtandao siku zijazo bila kuwepo kwa msingi mahsusi wa kisheria au amri ya mahakama. Kesi hii inasisitiza umuhimu wa kulinda haki ya kupata taarifa, uhuru wa mawasiliano na uwajibikaji wa serikali katika jamii ya kidemokrasia.