LHRC: Kupinga Kuongezwa Muda wa Leseni ya Uzalishaji Umeme kwa Kampuni ya IPTL

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARI
legar.jpg

Kupinga Kuongezwa Muda wa Leseni ya Uzalishaji Umeme kwa Kampuni ya IPTL

Ndugu Wanahabari,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni shirika lisilo la kiserikali lenye maono makuu ya kuona Jamii yenye Haki na Usawa Tanzania. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimejikita katika utetezi wa Haki za Binadamu ikijumuisha haki za maendeleo.
Ndugu Wanahabari,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa mshangao na masikitiko makubwa kinapingana na hatua ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kupokea na kutangaza kupitia gazeti la serikali la Daily News, la siku ya Jumatano Juni 7, 2017 kusudio la kuiongezea leseni ya uzalishaji umeme kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kampuni ambayo inahusishwa na kashfa nzito ya uchotwaji wa mabilioni kupitia akaunti ya ESCROW. Ikumbukwe kwamba Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mwaka 2014 ilitoa mapendekezo mbali mbali juu ya umiliki wa mitambo ya IPTL ikiwemo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi juu ya umiliki na uwepo wa rushwa katika utendaji kazi wa IPTL na wabia wake. Mapendekezo ambayo mpaka sasa hayajafanyiwa kazi huku umma wa watanzania ukiachwa katika bumbuwazi. Ndugu Wanahabari,
Mbali na kutokuwepo kwa taarifa sahihi juu ya upotevu mkubwa wa fedha za watanzania katika sakata la ESCROW, tumeshangazwa na kitendo cha EWURA kutaka maoni ya wadau huku ikiwa inafahamu fika kuwa mikataba kati ya Serikali na IPTL ni ya siri na hivyo wadau hawana sababu za kimkataba za kutoa mapingamizi au maoni.
Kutokana na sintofahamu hii, Chombo hiki chenye mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Madini kilipaswa kujiridhisha juu ya mapendekezo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Hesabu za Serikali juu ya utata wa umiliki wa IPTL na kashfa za rushwa zinazoizunguka badala ya kutaka maoni au mapingamizi kutoka kwa wananchi na wadau ambao hawajui undani wa mkataba wa IPTL na Serikali
Ndugu Wanahabari,
Kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji wa Serikali na makampuni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa mapendekezo yafuatayo:
1. EWURA kusitisha mara moja kusudio hili la kukusanya maoni ya kuiongezea muda kampuni ya IPTL mpaka serikali itakapotekeleza mapendekezo yote ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati yake ya mwaka 2014.
2. EWURA kujiridhisha uhalali wa kisheria juu ya umiliki, kujiridhisha pasipo shaka ushiriki wa IPTL katika suala zima akaunti ya ESCROW na tuhuma za rushwa kwa wamiliki wake.
3. EWURA kuomba radhi watanzania na wabunge kwa kujaribu kuirudisha IPTL kwa jamii huku ikitambua wazi miaka 3 iliyopita IPTL ilikuwa kwenye kashfa nzito iliyozua mtafaruku ndani na nje ya Tanzania.
4. LHRC, inaikumbusha jamii nzima ya watanzania, waheshimiwa wabunge, viongozi wa dini na vyama vya siasa kuungana pamoja kwa ajili ya maslahi ya umma katika kukata kusudio hili la kuongezewa leseni ya kuzalisha umeme nchini wakati kampuni tajwa imetiliwa shaka ya kuwa na dosari nyingi.
5. Serikali kutoa majibu na ufafanuzi wa utekelezwaji wa maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kampuni ya IPTL.
6. Serikali kupitia taasisi zake kuacha kufanya mazingaombwe kwa wananchi kwa kuwashirikisha katika shughuli ambazo hawajui misingi yake na badala yake wawe wazi katika hatua zote za makubaliano na wawekezaji.
Mwisho; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaamini vyombo vya habari vitakuwa mstari wa mbele kukumbusha namna Bunge na wadau wengine walivyosimama kidedea kuipinga kampuni ya IPTL baada ya kuibuka kwa sakata la ESCROW.

Imetolewa Alhamisi Juni 8, 2017

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
 
huu sasa ndiyo tunaouita uzalendo wa kweli - kuzuia uovu usifanyike.

siyo mtu unasubiri uwe rais au waziri kuonyesha "uzalendo wa maigizo"!

ACT-Wazalendo nao sio Wazalendo???
 
TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARIView attachment 521255

You have my card.
 
Kwenye hili la IPTL kuomba kuongezewa muda,, wabunge wapo kimya kabisa, haya hao TLS nao siwasikii kabisa.. bila shaka wanasubiri ishu za kisiasa.. nadhani ni vema tukaweka mambo ya vyama pembeni na kuungana kwa maslahi ya Taifa..
 
Hawastahili kabisa hawa matapeli, lakini watakuwa wameshatembeza rushwa ya kufa mtu katika sehemu nyeti mbali mbali nchini. Hakukuwa hata na sababu ya hewa EWURA kuweka hilo tangazo gazetini. Hawa ni wa kuwaambia sasa basi imetosha fungasheni virago vyenu.

Serikali inayojinasibu kupambana na Rushwa inawezaje kuwaongezea IPTL mkataba???

Hawa IPTL hawastahili kuongeza hata sekunde moja .....
 
TAMKO KWA VYOMBO VYA HABARIView attachment 521255

Kupinga Kuongezwa Muda wa Leseni ya Uzalishaji Umeme kwa Kampuni ya IPTL

Ndugu Wanahabari,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni shirika lisilo la kiserikali lenye maono makuu ya kuona Jamii yenye Haki na Usawa Tanzania. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimejikita katika utetezi wa Haki za Binadamu ikijumuisha haki za maendeleo.
Ndugu Wanahabari,
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa mshangao na masikitiko makubwa kinapingana na hatua ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kupokea na kutangaza kupitia gazeti la serikali la Daily News, la siku ya Jumatano Juni 7, 2017 kusudio la kuiongezea leseni ya uzalishaji umeme kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), kampuni ambayo inahusishwa na kashfa nzito ya uchotwaji wa mabilioni kupitia akaunti ya ESCROW. Ikumbukwe kwamba Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mwaka 2014 ilitoa mapendekezo mbali mbali juu ya umiliki wa mitambo ya IPTL ikiwemo, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi juu ya umiliki na uwepo wa rushwa katika utendaji kazi wa IPTL na wabia wake. Mapendekezo ambayo mpaka sasa hayajafanyiwa kazi huku umma wa watanzania ukiachwa katika bumbuwazi. Ndugu Wanahabari,
Mbali na kutokuwepo kwa taarifa sahihi juu ya upotevu mkubwa wa fedha za watanzania katika sakata la ESCROW, tumeshangazwa na kitendo cha EWURA kutaka maoni ya wadau huku ikiwa inafahamu fika kuwa mikataba kati ya Serikali na IPTL ni ya siri na hivyo wadau hawana sababu za kimkataba za kutoa mapingamizi au maoni.
Kutokana na sintofahamu hii, Chombo hiki chenye mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Madini kilipaswa kujiridhisha juu ya mapendekezo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Hesabu za Serikali juu ya utata wa umiliki wa IPTL na kashfa za rushwa zinazoizunguka badala ya kutaka maoni au mapingamizi kutoka kwa wananchi na wadau ambao hawajui undani wa mkataba wa IPTL na Serikali
Ndugu Wanahabari,
Kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji wa Serikali na makampuni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa mapendekezo yafuatayo:
1. EWURA kusitisha mara moja kusudio hili la kukusanya maoni ya kuiongezea muda kampuni ya IPTL mpaka serikali itakapotekeleza mapendekezo yote ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia kamati yake ya mwaka 2014.
2. EWURA kujiridhisha uhalali wa kisheria juu ya umiliki, kujiridhisha pasipo shaka ushiriki wa IPTL katika suala zima akaunti ya ESCROW na tuhuma za rushwa kwa wamiliki wake.
3. EWURA kuomba radhi watanzania na wabunge kwa kujaribu kuirudisha IPTL kwa jamii huku ikitambua wazi miaka 3 iliyopita IPTL ilikuwa kwenye kashfa nzito iliyozua mtafaruku ndani na nje ya Tanzania.
4. LHRC, inaikumbusha jamii nzima ya watanzania, waheshimiwa wabunge, viongozi wa dini na vyama vya siasa kuungana pamoja kwa ajili ya maslahi ya umma katika kukata kusudio hili la kuongezewa leseni ya kuzalisha umeme nchini wakati kampuni tajwa imetiliwa shaka ya kuwa na dosari nyingi.
5. Serikali kutoa majibu na ufafanuzi wa utekelezwaji wa maazimio ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya kampuni ya IPTL.
6. Serikali kupitia taasisi zake kuacha kufanya mazingaombwe kwa wananchi kwa kuwashirikisha katika shughuli ambazo hawajui misingi yake na badala yake wawe wazi katika hatua zote za makubaliano na wawekezaji.
Mwisho; Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaamini vyombo vya habari vitakuwa mstari wa mbele kukumbusha namna Bunge na wadau wengine walivyosimama kidedea kuipinga kampuni ya IPTL baada ya kuibuka kwa sakata la ESCROW.

Imetolewa Alhamisi Juni 8, 2017

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
kweli ni mazingaumbwe. iptl imegubikwa na shutuma nyingi za ufisadi na maswali na maazimio ya bunge ambayo hayajapatiwa ufumbuzi. iptl ingekua haikugubikwa na udanganyifu mkubwa ingekua haipo tanzania kwani ingekua imekabidhi mitambo yake tanesco miaka mingi iliyopita baada ya mkataba wake kumalizika. yafaa wanasheria wenye uzalendo kutumia fursa hii kuhakikisha kuwatimua na kurejesha haki zote walizodhulumiwa wananchi na hao wawekezaji bandia wakishirikiana na vigogo serikalini.
 
Serikali inayojinasibu kupambana na Rushwa inawezaje kuwaongezea IPTL mkataba??? Hawa IPTL hawastahili kuongeza hata sekunde moja .....
Itatusikitisha sana kama IPTL wakipewa tena mkataba kama mengi yaliyotajwa hayajapatiwa majibu..
 
IPTL MFE MILELE NA PESA MLIZOTUIBIE ZOTE ZIWATESE NYINYI NA VIZAZI VYENU MILELE YOTE!
 
Uzalendo wa Dr Magufuli na uonekane ktk hili la sivyo mashombo bandarini nayo yaachiliwe tu.
 
Back
Top Bottom