Leticia Nyerere kakurupuka

Leticia Nyerere kakurupuka

"Viongozi" wengi wanafuata mkumbo kwa matumbo yao. Inawezekana wengi tu hawaelewi kwa nini vyama vyao vinashikilia msimamo wa serikali mbili au tatu. Yaani wapowapo tu ili mradi salary inaingia hawana shida
 
AMESEMA HAYO ALIPOKUWA ANAHOJIWA NA MWANDISHI WA HABARI KUWA ALIFUATA MKUMBO KUTOKA NJE YA BUNGE LA KATIBA NA MPAKA SASA HAJATAMBUA NI KWANINI UKAWA WALIAMUA KUTOKA NJE YA BUNGE LA KATIBA, MOSI AMEENDA MBALI ZAIDI KWA KUSEMA KWAMBA NDANI YA CHADEMA UNAFANYA UNACHOAMRIWA NA WAKUBWA WAKO NA YEYE ALIAMUA KUFUATA MKUMBO WA YALE UKAWA WALIOFANYA KUTOKA NJE. MY TAKE: ndani ya ukawa kuna wajumbe wapo na uzalendo kwa taifa lao na wanahoji kuhusu viongozi wao kugomea kurudi bunge la katiba mpaka sasa,nichukue nafasi hii kumpongeza mheshiwa leticia nyerere,john shibuda,hamad rashid,na ndugu arfi kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.kwenu wadau
Nadhani hata ndani ya CCM wapo wengi tu wanatamani wawe nje ya bunge kama ukawa but wana msimamo mmoja. Kucross party lines sio kitu chepesi. We angalia Democratic na Republicans. Nchi nyingine ukifanya hivyo unapigwa risasi.Rejea definition ya chama cha siasa, neno lengo moja na nia moja ndio basis. CCM wameshupalia Serekali 2, kuna wengi mle wangependa ziwe 3, but msimamo ni 2. Wameungana wote. Ukawa wanagawa na posho. Ruzuku na posho ndio only life line iliyobaki kwa ccm kuwaumiza wapinzani. Ndio maana walifuta Saturday na Sunday kuongeza siku. Ilikuwa strategy ya kuwafanya ukawa waone lol mahela yote hayo tunayaacha. Watu dhaifu kama Shibuda akaona ndio mtaji wa kampeni next year????
 
Bunge la katiba limenifanya kuwaelewa wabunge wenye dhamira ya kweli na watetezi wa wananchi,ni kitu cha ajabu kabisa maneno,matendo,haiba visivyoendana na umri lakini sisi wananchi ndiyo wenye maamuzi juu ya tambo zao.sisi siyo vichaka vyao.
 
Alinichekesha sana kwenye hiyo taarifa ya habari juzi hasa alipokuwa anajitetea kwamba viongozi wa CHADEMA wanamuonea eti hajawahi kusign wala kuingia kwenye vikao vya BMK, nikajua tiari dawa ishamuingia.
 
Amejishushia hadhi sana kujibu maswali kwa uelewa wa chini kiasi kile.Anataka kutuaminisha maamuzi mengi aliyeshiriki amefuata mkumbo!Kama ndio aina ya wabunge tulionao.Hatuwezi kupata katiba sahihi kwa mahitaji ya mtanzania.Naamini wapo maccm wengi wanaofuata mkumbo wa serikali mbili,japo wanataka serikali tatu.
 
10496155_751628468235011_1428781522065951879_o.jpg
 
Back
Top Bottom