Leticia Nyerere kakurupuka

Leticia Nyerere kakurupuka

Mazoko

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2009
Posts
674
Reaction score
186
Nimejaribu kutafakari maneno aliyokuwa anayatoa mbele ya mtangazaji wa Star TV kuwa hajuwi kilichosababisha UKAWA wagome hili si tatizo maana kila mmoja anauwelewa tofauti. Shida yangu nipale aliposema YEYE KAFUATA MKUMBO hapa ndipo najiuliza hivi kweli huyu nikiongozi mbunge au nimtu wa mitaani

Haiwezekani mbunge akasema anafuata mkumbo hivi niviongozi wangapi wanafuata mkumbo je kama wapo taifa letu tunalipeleka wapi mbunge yupo kwaajili yakuwakilisha wananchi leo anafuata mkumbo mtunga sheria huyu

Hili ni njaa iliyokithiri anaona anakosa posho inamlazimu kuropoka bilakujuwa anaongelea nini. Pili kutokujuwa nini maana ya kiongozi nawajibu wake kama kiongozi( mbunge) tatu yeye na wabunge wengine heshimu mawazo yako na maamuzi yako kama unaona yako sahii

Mwisho kama nikiongozi kwa mfumo wa sasa CHAMA kikitoa msimamo huna budi kufuata kama hutaki unahiari kabisa kuachia ngazi
 
Mwanzo sana nilisema huyu mmama IQ yake iko chini sana! haya anayo ongea hayanishangazi kabisa...lakini na kuendekeza njaa ni kitu kibaya sana, utu wako unapotea kama mchezo
 
Huyu mama anapandia hilo jina la NYERERE tu lakini huko juu ya masikio hamna kitu!!
 
Nakubaliana na wanasema ana hongeka kirahisi mno, zero brain huyo mama! Nadhani akina Mwigulu wamesha jua udhaifu wake ulipo utaufanyia kazi.
 
AMESEMA HAYO ALIPOKUWA ANAHOJIWA NA MWANDISHI WA HABARI KUWA ALIFUATA MKUMBO KUTOKA NJE YA BUNGE LA KATIBA NA MPAKA SASA HAJATAMBUA NI KWANINI UKAWA WALIAMUA KUTOKA NJE YA BUNGE LA KATIBA, MOSI AMEENDA MBALI ZAIDI KWA KUSEMA KWAMBA NDANI YA CHADEMA UNAFANYA UNACHOAMRIWA NA WAKUBWA WAKO NA YEYE ALIAMUA KUFUATA MKUMBO WA YALE UKAWA WALIOFANYA KUTOKA NJE. MY TAKE: ndani ya ukawa kuna wajumbe wapo na uzalendo kwa taifa lao na wanahoji kuhusu viongozi wao kugomea kurudi bunge la katiba mpaka sasa,nichukue nafasi hii kumpongeza mheshiwa leticia nyerere,john shibuda,hamad rashid,na ndugu arfi kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.kwenu wadau
 
This is rubbish and hogwash. Hao wote ukimtoa Hamad wamefuata Posho tu hakuna uzalendo. Kwa nini nasema hivyo.? ukimuacha Hamad si Arfi, Leticia, wala Shibuda aliye na uwezo wa ku-influence mjadala kwenye BMK. Uwepo wao hauna tija ya maana kwetu sisi wenye mtizamo mbadala juu ya rasimu ya katiba. They add no value whatsoever! Subiri muone michango yao kwenye Bunge. Ni wasindikizaji tu.
 
sasa kama unawapongeza wako mjengoni au wameufyata? unacheza na rungu letu la kamati kuu:
 
Hivi unajua kuwa Leticia Mageni Nyerere na John Magale Shibuda ni mtu na Mjomba wake ? Tafakuri zao la damu moja DNA .........
 
Simshangai kwa sababu hata wabunge wengi wafuata mkumbo. Wabunge wengi wa CCM dhamira zao zinataka Serikali 3 lkn njaa inawafanya wakubali serikali 2
 
Msaka tonge huyo kaja akitokea US kudaka posho
 
Mimi ambaye sio mwanachama wala kiongozi wa CHADEMA nimesikia wakieleza sababu zilizowafanya wakatoka kwenye bunge la katiba inakuwaje huyu mbunge wa CHADEMA ambaye ni kiongozi wa wananchi kwa hiyo nafasi yake na alikuwa ndani ya bunge aseme amefuata mkumbo kutoka bungeni na wala hajui kilichomtoa? Kama watu wa aina hii ndio watunga sheria wetu basi kama nchi tuna safari ndefu kufikia maendeleo tunayoyatarajia.
 
Hivi inakuwaje MTU anampongeza mpumbavu siamini kiongozi wa wananchi anafuata mkumbo nakutelekeza wananchi wake kama anaamini yuko sawa arudi bungeni yeyote anayempongeza napata wasiwasi kama anatumia akili
 
chakula cha lukuvi hicho hasa awapo bungeni!!!!
 
Back
Top Bottom