Leo tarehe 23 May 2017 sitoisahau.. Yani hapa nanuka pesa tuu!!

Kapena

JF-Expert Member
Apr 9, 2017
376
507
Ukiona tabu zimezidi ujue nini kinafata....
Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi...
Baada ya kuliwa sana vi buku buku vyangu hatimae mambo mswano.

Leo nimetoka kuwekewa mzigo wangu wa Milioni 101.2 baada ya kushinda Perfect 12 siku ya Jmosi, ingawa wamenikata kodi milioni kama 9.3 hivi daah sio mbaya..

Kama haitoshi nafika home naangalia account yangu CRDB internet banking nakuta Salary ya Mwezi May imeingia imejaa tele... Haina kazi....

Kama haitoshi tena, asubuhi nimeweka mzigo wa 45,000 Premier Betting kwenye mechi zangu 3 za uhakika... Mbili zimetiki, moja ilobaki ina 95% za kutiki...
Nina uhakika wa kuvuta 726,000 kesho asubuhi.

Bila kusahau mchana niliweka mzigo wa 30,000 M-bet kwenye mechi nne za U20 Korea. *****, nimeingiza 930,000/= kwenye account yangu ya M-bet mapemaaaaa....

Sijui kesho niamke na Suprize kwa Mama yangu aliyeko Ngokolo Shinyanga.
Sijui niamke na Suprize kwa demu wangu aliyeko Mbezi Tangi Bovu...
Sijui niamkie pale Kinondoni B nikavute Toyota Allex kama nilivopanga...

Mei 23, 2017 sitokusahau. Leo nanuka pesa.
Account yangu Exim nime deposit milioni 101.2
M-bet account nimevuta 930,000 kwa kutumia 30,000.
Premier kesho naenda pale Mwenge kuvuta 726,000.
Salary imejaa tuliii kwenye account yangu CRDB.

Kwa kuwa mie sio mtu wa kujirusha wala pombe basi
Ngoja nikalale huku nawaza kesho niamkaje aisee...
 
Yule jamaa mwenye ndevu zenye vipilipili alijiimbia...

"Unaweza ukaota umejenga angani, angani. Kuhifadhi ndoto ya shida gani?"

Mkuu wewe ni hatari, umekula mil 101.2, wakakukata kodi mil 9. Lakini bado unatumbia account yako ya exim umetia mil 101.2.

Hongera boss!
 
Yule jamaa mwenye ndevu zenye vipilipili alijiimbia...

"Unaweza ukaota umejenga angani, angani. Kuhifadhi ndoto ya shida gani?"

Mkuu wewe ni hatari, umekula mil 101.2, wakakukata kodi mil 9. Lakini bado unatumbia account yako ya exim umetia mil 101.2.

Hongera boss!
hivi kapotelea wapi huyo kijana alikuwa anajua sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom