Leo nimekutana tena na classmate na jirani yetu nyumbani nilikozaliwa, ni muuza mgahawa Dar!

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,462
Dah! Kuna dada ni jirani yetu home nilikozaliwa. Wazazi wake walifariki so alilelewa na bibi. Huyu dada nilisoma naye O level, alikuwaga wa kwanza class siku zote. Baadaye ikawa ikitokea mkakutana na huyu dada akakupa no yake ya simu itapatikana siku hiyo tuu.

Alikuwa na tabia ya kutoroka sana shule akapewa adhabu ya kukaa nyumbani mwezi. Ghafla yupo kibosho Girls na bibi hakuwa na uwezo alikuwa anatwambiaga alipataga wafadhili wa kumsomesha. Ok akasoma UDSM akaenda nje sijui kusoma nini!Eti namkuta anauza mgahawa manzese Dar es salaam tena kaajiriwa mshahara waweza usizidi laki.

Haonyeshi kuchoka, eti hana simu. Hapendi nijue anakoishi wala hataki mazoea. Home kwa bibi pale pamejegwa kigorofa, pickup ya majani, wafanyakazi kibao na dereva juu. Bibi alikuwa na watoto 3 mmoja alikufa , 2 ni walimu MOSHI hukohuko na nawajua na najua maisha yao tuu. Bibi ni Mzee sana kwa sasa na haoni hata.

Dah! classmate muuza mgahawa kanifurahisha leo.
 
Ok akasoma UDSM
Akaenda nje sijui kusoma nini!

Duuh hapo bwana Temba sijakupata kabisaa umepiga mixer ya hatarii
 
Dah! Kuna dada ni jirani yetu home nilikozaliwa
Wazazi wake walifariki
So alilelewa na bibi
Huyu dada Nilisoma naye O level
Alikuwaga wa kwanza class siku zote
Baadaye ikawa ikitokea mkakutana na huyu dada Akakupa no yake ya simu itapatikana siku hiyo tuu
Alikuwa na tabia ya kutoroka sana shule
Akapewa adhabu ya kukaa nyumbani mwezi
Ghafla yupo kibosho Girls
Na bibi hakuwa na uwezo alikuwa anatwambiaga alipataga wafadhili wa kumsomesha
Ok akasoma UDSM
Akaenda nje sijui kusoma nini!
Eti namkuta anauza mgahawa manzese Dar es salaam tena kaajiriwa mshahara waweza usizidi laki
Haonyeshe kuchoka
Eti Hana simu
Hapendi nijue anakoishi wala hataki mazoea
Home kwa bibi pale pamejegwa kigorofa, pickup ya majani, wafanya kazi kibao na dereva juu,
Bibi alikuwa na watoto 3 mmoja alikufa , 2 ni walimu MOSHI uko uko , na nawajua na najua maisha yao tuu
Bibi ni Mzee sana kwa sasa na haoni ata
Dah! classmate muuza mgahawa kanifuraisha leo

Uwe unajiongeza na wewe bwana, ni mtu wa mfumo na hapo yupo kazini, na akishajua unamfatilia sana atapotea hapo
 
Kwahiyo umefurahia kumuona katika hali hiyo ya shida? Na je elimu yake kubwa na kazi ndogo anayofanya vinakuhusu nini? Kwani unamfahamu saana huyo dada? Maana kuna watu MNAWAZA haraka na kufika hitimisho bila KUFIKIRI! ANZA KUFIKIRI ACHA KUWAZA TU.
 
Jifunze kwa huu mfano: mwaka juzi tuliletwa Dar kwa shughuli maalumu ambapo tuligawanywa kwenye makundi haya: mmoja akaanza kujifanya kushona viatu hapo jijini, mwingine kuhubiri kumbe hata sio mhubiri wa kweli na mwingine shoe shiner LAKINI WOTE HATUKUWA NA LENGO HILO TULITUMWA KWA LENGO LINGINE KABISA. Kwahiyo kuwa makini na kuwachukulia watu kirahisi rahisi hata hivyo maisha hupanda na kushuka! (NI MFANO TU SIYO HALI HALISI) ila jifunze.
 
Huyu Jamaa anaishi Dar.
Na ndio walee wenye kulewa muda wa Kazi.
Hongera kwa kuitendea haki Weekend yako,haya ndio matokeo ya bia za pesa ya mshahara.
Ili mtu akuelewe lazima awe mlevi tena wa roba
 
Back
Top Bottom