Leo nimeenda Mlimani City kwa mara ya kwanza

Zekidon

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,903
566
Wakuu habarini jamani,

Baada ya kujipanga mwaka mzima , nikaamua kutumia kajibonasi kangu kufanya ziara mlimani city. Huwa napitaga tu nikitoka Mwenge kwenda Ubungo. Sijawahi kuingia.

Basi bwana kufika mule ni viinglishi tu vinaendelea. Ila nimepakubali sana maana kuna mabinti warembo kweli kweli na wengi wao wamevaa miwani mikubwa, sketi za kubana mapaja nje, na vikuku. Wamependeza haswa.

Nikala aiskrimu, nilifurahi sana.

Nitarudi tena wikiend ijayo.
 
hahahhahahahahhaaaaaa...ndugu asubuhi hii umenichekesha sanaaaa,asante..rudi tena bwana utuambie ziara ilivyoenda
 
Hapo hapo mlimani city...siku jitupe ndani ya cinema... alafu tupia marejesho...
 
Wakuu habarini jamani,

Baada ya kujipanga mwaka mzima , nikaamua kutumia kajibonasi kangu kufanya ziara mlimani city. Huwa napitaga tu nikitoka Mwenge kwenda Ubungo. Sijawahi kuingia.

Basi bwana kufika mule ni viinglishi tu vinaendelea. Ila nimepakubali sana maana kuna mabinti warembo kweli kweli na wengi wao wamevaa miwani mikubwa, sketi za kubana mapaja nje, na vikuku. Wamependeza haswa.

Nikala aiskrimu, nilifurahi sana.

Nitarudi tena wikiend ijayo.

Kwahiyo mkuu kabonasi kako umenunua Ice cream tu?
 
Kikubwa ilikuwa ni hao watoto uliowaona mengine ni blabla tu ila angalizo usijaribu kuwatupia ndoano maana kama unafamilia utailetea matatizo
 
Back
Top Bottom