mzee wa kasumba
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 1,432
- 2,892
NIMEPOTEZA KIBARUA
Binafsi sikuwa muajiriwa serikalini, lakini nilikuwa kibarua katika kampuni flani. Hii ni sehemu ambayo imenilea kwa muda mrefu kiasi kisichopungua miaka mitatu. Hii ndio sehemu ambayo nilikuwa naitegemea kwa asilimia kubwa kulisha familia yangu.
Wiki iliyopita kuna mambo hayakuwa sawa upande wangu kama mtunza stock. Kiukweli ni kwamba kuna tamaa tulipandikizana na afanyakazi wenzangu na baadhi ya mzigo tukauiba na kuuza. Lengo ni kupata pesa nyingi kwa mkupuo na kusahau kuwa kuna kitu kinaitwa KUUMBUKA.
Daaah, ebwana kama Muvi. Sijui bosi alipenyezewa za chini chini na nani aisee.. Mara akaibuka ghafla eneo la kazi. (Hua anaishi nje ya Mkoa tuliyopo)
Alipofika cha kwanza alitaka tuchukue stock yote. Kiukweli mapungufu makubwa yalionekana. Mtu wa kutakiwa kujibu maswali yale nilikuwa ni mimi, nami sikuwa na cha kuongea zaidi ya kuomba radhi na kuomba kukatwa katika mshahara wangu.
Pamoja na msamaha wangu wote lakini mwarabu yule hakutaka kunielewa na kuanzia muda alinitimua kama mbwa na kutaka nirudi nyumbani na ndio mwisho wa kazi.
SIKUAMINI MASIKIO YANGU WALA MACHO YANGU... Kwakweli nilichanganyikiwa sana sana.
Tangu hapo ndio nikawa nimepoteza kibarua changu na ni wiki ya pili sasa naishi kwa kuungaunga.
Daaah najua nitalaumiwa lakini hiyo ndio hali iliyonikumba ndugu yenu.
Naomba msaada wa kimawazo, ushauri, kazi, kibarua au deiwaka.
Asanteni sana. Ni mimi ndugu yenu mzee wa kasumba zisizokuwa na madhara

- Familia inanitegemea (Mke, watoto na ndugu)
- Tamaa zimeniponza
- Sina pa kushika
- Kichwa kimechanganyikiwa sana sielewi cha kufanya