Leo ndio naikumbuka kauli ya Lowassa alopata kuninong'oneza katika Uwanja wa Majimaji huko Songea

Tinde nsalala

JF-Expert Member
Feb 12, 2017
248
253
Namnukuu;
"Dogo,ktk kufanya siasa,usiwe mfanya siasa MTAKA SIFA!Bali SIFA NDIYO IKUTAKE ww.SIFA ya siasa ikikutaka ww hata wafanye nini kamwe hawawezi kukufuta ktk kufanya siasa.

Hata wangetumia bulldozer kukufukia lkn madongo yale yatatawanywa na wengine ili tu ww uokoke kutokea kifusi kile."

Huku tukiendelea kumsikiliza Mwenyekiti wa chama kipindi hicho ndg Jakaya,alipokuwa akihutubia hadhala ya wana-CCM ktk maadhimisho ya sherehe za chama kutimiza UMRI wa miaka...Edward aliendelea..."Maisha ya mwana siasa ni sawa na taa ya chemli.Kioo kikipasuka upepo huufifisha moto uwakao ktk utambi.Na kioo kisipopasuka,moto uwakao ktk lile tambi,huendelee kumlika kwa heri kabisa!"...

Aliendelea..."SIFA ya siasa ikikufuta ww hadi mwisho wa isha lako wapenda siasa watakupenda tu!Pesa si kila kitu ktk siasa. Bali,HAIBA ndilo hasa hitaji lililo kuu kwa mfanya siasa-na si MABAVU na kuvimbia wengine eti uwaonyeshe kwamba ww ni mfanya siasa!"...Alitabasamu!

Kisha akaendelea..."Ukiwa na HAIBA ya siasa ww ndiwe mfanya siasa wa kweli na wapenda siasa lazima watatamani tu ufanye siasa na utakuwa si KINAI kwao."

Bahati mbaya sana maongezi yetu yakakatishwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma,Oddo.Aliniita na kunielekeza nifanye jambo fulani.Na kwalo nikawa nimetenganishwa na EL na sikupata tena wasaa wa kumsogelea na hata pale nilipo rejea.

Lkn,maneno ya EL sikupata kuelewa alikuwa anamaanisha nini!Nieleweke tu,mm sikuwahi kabisa kuwa mshabiki wa EL ktk lolote.Itoshe tu kusema,mm sikuwa SHABIKI wake.

Leo ghafla nayakumbuka maongezi yale.Najaribu kupata maanisho,lkn nashindwa!

Nakualika mwa jf hebu na pengine jaribu kunisaidia,ni nini labda mheshiwa huyu alikuwa akimaanisha?

Karibu.
 
Back
Top Bottom