kilwakivinje
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 5,999
- 9,089
Baada ya kula ng’ombe mzima katika mechi 26 zilizopita, leo ni fursa muhimu kwa Yanga kumalizia mkia utakaowapa rasmi ufalme wa Ligi Kuu msimu huu, watakapoikaribisha Coastal Union katika Uwanja wa Mkapa kuanzia saa 2:30 usiku.
Matokeo ya ushindi huo yataihakikishia Yanga ubingwa na kuhitimisha utawala wa misimu minne mfululizo ya watani wao, Simba ambao ndio walikuwa wababe wakitwaa mara nne mfululizo.
Kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Coastal Union, Yanga itafikisha pointi 67 ambazo HAZITAFIKIWA na timu nyingine yoyote.