Leo kidogo nivunjike mguu Ferry Kigamboni

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
571
204
Jamani pale Ferry upande wa Kigamboni sehemu inapopaki pantoni kuna shimo kubwa kutokana na zege lililobomoka na nondo zimejitokeza zikiwa tayari kumuumiza mtu.Leo asubuhi na mapema ikiwa bado kuna kigiza nilijikuta mguu umetumbukia hapo nikajitahidi nisianguke, baada ya kujinusuru kwa mbele yangu nakuta tena nondo ya mm12 ambayo ilibaki kidogo niivae.

Nawatahadharisha watumiaji wenzagu wa kivuko na hali hiyo.

Tuwe makini hasa nyakati za usiku na asubuhi.
 
Nakushauri utumie daraja la NSSF kwa faida ya afya yako hadi utakapojidhirishia kwamba wahusika wamefanya sehemu hiyo kuwa salama.
 
HA Ha ha ha...dah kumbe ndio wewe eh pole sana ndugu yangu... sio kwa mdumbukio ule
 
Yeah mkuu pole sana!

asante ndugu, nilipita jioni nikakuta kuna mtu kasimama pembeni ya hilo shimo akiwaelekeza watu wasipite upande huo. Nadhani ni mfanyakazi wa pale feri.
 
Pia mnaotumia Basi za mwendo kasi kuweni waangalifu mnapoingia na wakati wa kutoka kwani kuna uwazi kati ya basi na ukuta ambao unaweza ukakubadilishia jina pindi ukifanya uzembe wa kutokuwa mwangalifu
 
Pia mnaotumia Basi za mwendo kasi kuweni waangalifu mnapoingia na wakati wa kutoka kwani kuna uwazi kati ya basi na ukuta ambao unaweza ukakubadilishia jina pindi ukifanya uzembe wa kutokuwa mwangalifu
haswa kwa watoto wadogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom