MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,605

Ni nini?
Huu ni ushuru ambao unawekwa kwenye Bidhaa zinazoingia nchini ili bei zake zipande na kuwa angalau sawa na bidhaa zinazotengenezwa hapa nchini.
Mfano:

Unabiashara/kiwanda cha kutengeneza MATAIRI ya Gari na Kampuni nyingine iko MALASIA infanya biashara hiyohiyo. Lakini kutokana na kwao Malighafi na Gharama za uzalishaji kuwa chini wanaleta Matairi yao Tanzania Kwa bei rahisi kuliko yako. Na kampuni yako inaelekea kufirisika kwa kukosa wateja. Unaamua kwenda Serikalini kwa ajili ya msaada. Serikali/TRA wanaweka kodi kwa Kampuni ya malaysia kulinda biashara yako ili isife. Kama kodi ni kubwa kiasi cha kutosha, Matairi ya Malaysia itabidi yapande bei na Biashara yako Imelindwa.
Kodi hii ndio PROTECTIVE TARRIF.
MFANO HALISI KATIKA PICHA JINSI INAVYOFANYA KAZI,

ILIANZAJE ANZAJE ?

mmarekani Alexander Hamilton ndio mtu wa kwanza kupendekeza hii kitu ili kulinda viwanda na biashara ya ndani US. Baada ya vita vya 1822 marekani, Bidhaa kutoka UK zilifurika na kuanza kuua viwanda vya ndani na kutishia kabisa uwepo wa viwanda marekani kama kwetu sasa Bidhaa kutoka China. Bunge la Congress 1816 likapitisha.
SIKU HIZI HALI IKOJE?

TUME YA KIMATAIFA YA BIASHARA INARIPOTI KUWA KUNA KODI ZAIDI YA 12000 KWA BIDHAA MBALIMBALI ZINAZOINGIA USA. Mfano karanga ambazo hazijapukuchuliwa zina hadi 163.3% ya kodi. Nyama kutoka ulaya, siagi na bidhaa mbalimbali zina hadi 100% ya kodi. Sekta zote za ndani zinategemea kodi hizi kuwepo kwao sokoni. Bila hii bidhaa za wamarekani zingepata wakati mgumu sana mbele ya macho ya wateja wao.
Kama nchi au mtu mmoja mmoja tuna mengi ya kujifunza kutoka katika historia mbalimbali duniani. Vitu hivi vikiingizwa kwa umakini bila upendeleo wala ubinafsi vitachechea maendeleo katika kila kona ya taifa.