Mshangazi mdogomdogo
Member
- Sep 23, 2024
- 58
- 32
Asilimia kubwa ya sisi Wafanyabiashara Kisiwani Pemba tunapata wakati mgumu kuhusu suala la kodi na ushuru mkubwa tunaotozwa katika Bandari ya Unguja pamoja na Bandari ya Pemba
Hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya bidhaa kupanda bei tofauti na uhalisia kwa kuwa tunalazimika kufanya hivyo ili angalau turejeshe gharama tulizotumia kuzisafirisha.
Tunaponunua bidhaa kutoka Unguja tunalipa ushuru na kodi kwa mamlaka za kikodi, tukifika Pemba napo kuna gharama za kulipia.
Ushuru na kodi zinapokuwa rafiki zitasaidia bei ya bidhaa kuwa chini na pia itawarahisishia Wananchi kuzinunua kwa bei ya chini.
Hivi karibuni kwenye moja ya Kongamano Afisa Mdhamini Wizara ya Biashara, Ali Suleiman alisema endapo Kodi na Tozo zitakuwa rafiki kwa Wafanyabiashara itasaidia kuchangia ukuaji wa pato la Nchi, hiyo inamaanisha Mamlaka zenyewe zinajua kuna hiyo changamoto.