Leo Bunge linajadili Mpango mpya wa Maendeleo wa 2016/2021, je 2011/2016 umetekelezwa?

Huey P jr

JF-Expert Member
Apr 26, 2015
347
134
Mpango wa Maendeleo wa 2011/2016 umetekelezwa?

Leo Bunge linajadili Mpango mpya wa Maendeleo wa miaka mitano 2016/2021. Hata hivyo tunapaswa kujiuliza kama tulitimiza malengo ya Mpango wa Maendeleo uliomalizika. Tuangalie sekta ya Elimu na Afya.

Mpango wa 2011/2016 unasema " .... Sekta ya Elimu pekee inahitaji walimu 900,000 wenye ujuzi ikilinganishwa na Walimu 238,000 waliopo sasa ( 2011 ). Katika Sekta ya Afya, idadi ya wataalam 110,000 waliopo sasa italazimika kuongezeka mara nne kufikia wataalam 476,000 .... " ( uk 35 ).

Mpango unaweka malengo " ... Tanzania inalenga kwamba kufikia Mwaka 2015 kuwa na wanasayansi 26,000; wasanifu na wahandisi 88,000; wanasayansi wa afya 22,000; na wanasayansi tabibu wa meno na mifugo 64,000; wataalam wa masuala ya kiuchumi 30,000; wataalam wa uhasibu na usimamizi wa fedha 63,000; walimu 320,000 na wataalam wa ngazi za umeneja130,000. Ili kufikia Malengo haya ya wataalam ifikapo Mwaka 2015/16, italazimu kuanzia Mwaka 2011 kiasi cha wanavyuo 80,000 wawe wanahitimu kila mwaka kutoka taasisi za Elimu ya Juu.
Wafanyakazi wa 635,000 wenye ujuzi wa ngazi ya VETA watahitajika ifikapo mwaka 2015". ( uk 36 )

Tumefikia malengo haya?

Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa iliyotolewa mwezi Juni, 2015 inaonyesha kuwa;

Wanafunzi katika Vyuo vyote vya VETA nchini kote walikuwa 164,077 tu.

Wanafunzi katika Vyuo vikuu vyote nchini walikuwa 204,175 na wahitimu Mwaka 2015 walikuwa takribani 30,000 tu.

Mpango uliweka malengo mahususi Kwa sekta ya Elimu, ikiwemo

1 Kujengwa Kwa Kampasi ya Mloganzila ya Chuo Kikuu cha Muhimbili.

Utekelezaji

Ujenzi haujaanza kabisa.

2 Taasisi 5 za Elimu ya Juu kukarabatiwa na kuwa na wafanyakazi wenye utaalamu wa VETA 635,000

Utekekezaji

Watu wenye ujuzi wa VETA wapo 200,000 tu. Taarifa za ukarabati wa Taasisi za Elimu ya Juu haijulikani.

3 Walimu 133,000 diploma na daraja A wawe wamefundishwa

Utekelezaji

Walimu 150,000 wamefundishwa. Lengo limefikiwa na kupitiliza.

4 kupunguza athari za malaria Kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2015.

5 kupunguza vifo vya wajawazito kutoka 578 hadi 175 Kwa kila vizazi hai 100,000 na vifo vya watoto chini ya miaka mitano kutoka 112 hadi 45 Kwa kila vizazi hai 1000

Utekelezaji

Sijafanikiwa kupata takwimu za malengo namba 4 na 5.

Utaona kuwa wakati tunaandaa Mpango mpya wa 2016/2021 ni muhimu kwanza kutafakari na kutathmini utekelezaji wa malengo ya Mpango wa 2011/16. Malengo mengi hayajafikiwa kiasi kwamba kuundwa Kwa Mpango mpya kunaonekana hakuna maana.

Like
 
naitabiria makubwa hii kamati ya guantanamo, huenda ndio ikawa kamati maarufu kuliko kamati zote za bunge
 
Back
Top Bottom